Nimeacha rasmi kushabikia Manchester United

Nimeacha rasmi kushabikia Manchester United

sasa we unaona bora vipi, ukose makombe kabisa uwe coke zero au uchukue angalau ya mapinduzi?

na kama makombe ni hela basi Man u ndio timu bora ulimwenguni kwa sasa, sababu wana hela kushinda timu zote.
Mkuu kumbe huwa unafika mpaka huku. Ukweli ni kwamba united era yake imekwisha. Kwa sasa inapita kwenye kipindi kigumu. Pamoja na gharama kubwa mnazowekeza bada hamwezi kuwa na timu nzuri kama chelsea spurs city.

City kwa sasa ni [emoji91] wa kuotea mbali. Hawa ni sawa na psg barcelona na madrid. Itawachukuwa muda mrefu kurudi kwenye reli. Mnapita wanakopita Ac Milan, Liverpool, na hata Aseno.
 
karibu sana chama kubwa man city mzeebaba..umefanya maamuzi sahihi kabisa na nakuahidi hutokaa kujutia maamuzi yako..mpira wetu sisi ni full burudani kama unavyojua,mtu anatafuta mpira kwa tochi na bado anapokea kichapo kizito kwenye upande wakikosi dah...nisiongee sana hilo ndo jiji la wanaume(man city) [emoji123]
 
Mimi ndio mara ya kwanza kusikia shabiki wa mpira anahama timu na kwenda timu nyingine. Wewe sio shabiki wala mpenzi wa mpira ila unafuata timu inayoshinda wala sio ajabu msimu ule Leicester City kuchukua ubingwa wa EPL wewe pia ulikuwa shabiki wa hiyo timu.
 
Huyu jamaa mwanzisha uzi hana tofauti sana na pengine ni pacha na mwenye ID ya Sergio5 sio kwa majibu ya kitoto hivi.
Anafahamika baada ya kupigwa ban amefungua akaunti nyingine kuandika pumba mwambie tutamripoti akaunti zake ziunganishwe au apigwe IP ban
 
Umeichambua vyema sana Man U.., msimu huu imekuwa mbovu/butu haijawahi kutokea.., kwa kifupi Morinyo hana jipya zaidi ya kubahatisha!!
 
We ni arsenal wewe.. washabiki wa Man u hatunaga roho nyepesi hvo...
 
Hakuna timu kubwa kuliko zote uk yenye mafanikio
zaidi ya Man U.T.D wewe ni mtoto wa juzi unaishabikia
Man city pole bwana mdogo utakuwa ulizaliwa miaka
Ya 2000
 
Umeichambua vyema sana Man U.., msimu huu imekuwa mbovu/butu haijawahi kutokea.., kwa kifupi Morinyo hana jipya zaidi ya kubahatisha!!


Mkuu mimi nashabikia Man U ila huyo Jose sikuwahi kumkubali toka anachukua hii timu kuifundisha. Yeye sio Kocha ila ni mzuri wa kuhudhuria mazoezi na kupanga nani acheze. Ndio maana akipewa timu kitu cha kwanza huwa anaomba pesa nyingi ili akusanye wachezaji ambao ni viwango vya juu kama CR7, Messi na wanaofanana na hao ili apate urahisi wa kuhudhuria mazoezi na kupanga timu. Kifupi ni kuwa Jose hana ujuzi wowote wa kufundisha zaidi ya mbinu yake ya kucheza mchezo wa kujihami na kupaki BUS. Angalia timu zote alizofundisha alikuwa anapata ushindi ni kwa sababu alikuwa ana bahati ya kupata wachezaji a viwango ambavyo hata bila kocha wanaweza kucheza. Msimu TOH wanacheza vizuri zaidi kuliko hao Man U.

Kitu kingine pale Man U kuna wachezaji wanapata namba kwa kuwa tu ni Waingereza, mfano Smalling mimi sioni kama ni beki wakuweza kudhibiti washambuliaji wenye njaa ya magoli. Pale Man U panahitajika ukarabati wa hali ya juu pamoja na kumleta kocha mpya huyu aliyepo hawezi kazi.
 
Back
Top Bottom