Nimeachana na mpenzi wangu

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Huyu rafiki yangu (mchepuko) ana ujauzito wa miezi miwili; baada ya kumuona jana jioni hana mishe, nikaamua kumpigia simu ili nimtoe 'out' angalau tukapige kitimoto na maji ya dhahabu.

Tukakubaliana tukutane kiwanja fulani; baada ya kufika tukapiga kilo mbili za kitimoto pamoja na vinywaji, bahati nzuri sisi wote ni wanywaji.

Baada ya kupiga maji sana, tukawa tunajiandaa tuondoke, ile nataka kusimama tu, bi mkubwa (wife) akanipigia simu, tukabadilishana abc na kumuambia kesho nitakutumia kiasi fulani cha salio.

Ile mchepuko kusikia naongea na bi mkubwa kuhusu mikakati, akajawa na wivu na kuanza kulalamika na kusema, ''anayependwa hapa ni mtu mmoja tu''. Nikamuuliza kwa nini unasema hivyo, hakunijibu,matokeo yake akawa ananipa pochi yake nibebe. Nikamwambia mimi ni mwanaume siwezi kubeba pochi/mkoba wako.

Alikuwa ameshikilia chupa ya maji akatupa kule, tukavutana mpaka tukafika nyumbani; ile tumelala kitandani hataki kuguswa, akaamka kwa hasira usiku huo na kusema hatonitafuta tena na anaenda kwake; ikabidi nimwambie sawa hakuna shida.

Baada ya kuondoka usiku huo, nikamtumia ujumbe na kumwambia; mimi niko huru sasa kuwa na mtu mwingine,nawe pia kuwa huru kuwa na mwanaume mwingine.

Mpaka sasa hajajibu huo ujumbe; na sitegemei kumbembeleza arudi kwenye mahusiano.​
 
Kwahiyo uko wapi......
 
Mimba ni yako au yake au yenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…