Nimeachwa na mpenzi sababu anataka tuishi pasipo ndoa (sogea tuishi)

"..... anataka tuishi pasipo ndoa.. ". Mbona tayari mnaishi pasipo ndoa? Unampatia huduma za mke wa ndoa, afu unakuja hapa kulialia. Kwa mtazamo wako unadhani hivyo unavyofanya sasa kugawa uroda kienyeji tu hauwasonineshi wazazi? Badilika, acha ukahaba.
 
Good ridance!
 
Pole mkuu, pana shida kidogo hasa huo msimamo wake wa kutotaka kujitambulisha kwa ndio tatizo kubwa!
Ila binafsi kwa uzoefu nilouona mtaani kwa ndoa nyingi za sasa ningeshauri hata makanisa yangeangalia namna ya kubadili utaratibu ikibidi waonaji wamamlizane na wawzazi wa pande zote tu kisha waoane bila kufunga ndoa ila warudi kanisani kufunga ndoa baada ya kuishi pamoja miaka 3 !

Kuna ndoa nyingi sana hivi sasa zinafungwa na kuvunjika zikiwa hata mwaka 1 hazijamaliza, shida ni kuwa wengi wanaingia kwenye ndoa bila kujana sawasawa Matokea yake mnashindana pahovyo mnavunja ndoa mnabaki na vifungo!
 
Uamuzi wako ni sahihi.Na hawez kukuacha huyo atarudi tu.

Mkishindwa kulindiana heshima zinazowa involve mpaka wazaz basi hata huko ndani wawili heshima na taratibu mtavunjiana daily.

NB
Hapo sasa akikuotea akakupiga mimba bas ndio kwisha habar yako
 
Uamuzi wako ni sahihi.Na hawez kukuacha huyo atarudi tu.

Mkishindwa kulindiana heshima zinazowa involve mpaka wazaz basi hata huko ndani wawili heshima na taratibu mtavunjiana daily.

NB
Hapo sasa akikuotea akakupiga mimba bas ndio kwisha habar yako
Hata akirudi kwa sasa hana nafasi tena kwangu nilisha move on muda mrefu sana.
X hata akifa sitahudhuria mazishi yake!
 
Umeshawahi kuishi nae hata mwezi mmoja au wiki 2?? Simtetei lakini Labda anataka kujaribu kukaa kidogo kabla ya kukuoa kuona je mnaweza kweli kuwa pamoja hadi kuoana, yaani mnaendana.

Tukiacha sababu za kidini na tamaduni, ni muhimu kumfahamu mwenzio vizuri kabla ya kuchukua uamuzi mzito. mfano nchi za magharibi wanaishi miaka mingi na kuzaa watoto wakiwa tu boyfriend/girlfriend kuoana inakuja baadae wameshatambua kwamba kweli wanaweza kuwa pamoja.

Mtu anaweza kuwa ni mpenzi lakini usiyaone makucha yake mpaka ukae nae kidogo kupata hali halisi ya jinsi alivyo.
 
Anijaribu kidogo nimekuwa gari? Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka mitatu! Single mothers wengi wametokana na zao la kujaribiwa afu wanaachwa na watoto wenyewe. Hakuna kitu kinachoitwa majaribio kwenye maisha Mkuu! By the way nilishapoa sijui huu uzi umefufukaje tena
 
Una miaka mingap?!
 
Haidhuru utapata mwingine
 
Ungekazia utambulisho kwanza ambalo ndo jambo muhimu zaid,siyo kukazia ndoa,hata mimi ningekutema.
Utambulisho ulikuwa ni kwa masharti kuwa niache kazi niishi kwake ndipo utambulisho ufuate! By the way nilishasahau naendelea na life langu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…