Scenario yako inafanana na yangu kidogo, mi nilimuacha mwanamke ninae mpenda nikiwa bado nampenda kwakua alifanya kosa moja tu ambalo nimejiwekea misingi sitamsamehe yoyote akifanya kosa hilo
Nikamwambia aniweke kwenye list ya watu wake waliokufa na hataniona tena,
kadri alivyokua anazidi kuniomba msamaha ndo jinsi nilivyokua nazidi kumchukia kila neno lake alilosema na yale aliyowahi kuyasema yote nilikua naona ni uongo sikumuamini tena na hata ningeishi nae nisingemuamini maisha yake yote
Alifikiri labda nilikua natania tu au ilikua ni hasira ila huo ndo msimamo wangu licha ya kuwa kweli nilimpenda lakin nimemuacha for my peace, dignity and survival
Mwanzo niliumia sana lakin nimejilazimisha hadi imefikia hatua sina hisia za upendo wowote kwake wala simchukii ila sitamani hata kumuona,
Kwa sasa sina hisia za kumpenda mwanamke yoyote nmekua kama chuma inayotembea.