Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Kumbe tupo wengi, japo mimi ni tofauti kidogo.
Nina maumivu nimezaa na binti mmoja, mtoto bado ana umri wa miezi 5 juzi ananiambia nikamchukue anataka kuolewa. Kumbuka nina mke ndani hajui chochote na akijua ndoa inayumba. Maumivu x2, kwanza nampenda binti mpaka nikamzalisha. Pili hilo la mtoto sielewi cha kufanya, na anadai nisipoenda kumchukua atamleta mwenyewe kwangu
Huyu hataki kuolewa anataka kua mke mdogo
 
huu uzi ulikuja kimasihara cha ajabu umegonga 500+ comments

Kwa sababu ni mambo yanayo mgusa kila mtu. Wachache sana walioko kwenye mapenzi yaliyo nyooooka. Wengi wetu tunapitia haya yaliyo msibu jamaa alafu kabla ya kujua tatizo na kupona tunajikuta tumesha ingia kwenye uhusiano mwingi ili kupoza machungu matokeo yake ni kuumiza wengine.
 
Piga moyo konde na u-move on. Nilipitia changamoto kama yako miaka kadhaa ilopita. Inawezekana huyo alikuwa na mtu wake, na wewe ukawa second choice. Mwenzio aliposikia umeahirisha kupeleka posa, akakuwahi.

Niliwahi kupoteza miaka 3+ kwa mwanamke ambaye kumbe hakuwa na plan na mie huku nilikuwa namuandaa kuwa mke. Alikataa ndoa mara 3. Nika move on na kupata mwingine na kuoa. Mapenzi inayopewa ninajuta kwa nini nilipoteza miaka 3+ kwa 'umbwa' yule.
 
Piga moyo konde na u-move on. Nilipitia changamoto kama yako miaka kadhaa ilopita. Inawezekana huyo alikuwa na mtu wake, na wewe ukawa second choice. Mwenzio aliposikia umeahirisha kupeleka posa, akakuwahi.

Niliwahi kupoteza miaka 3+ kwa mwanamke ambaye kumbe hakuwa na plan na mie huku nilikuwa namuandaa kuwa mke. Alikataa ndoa mara 3. Nika move on na kupata mwingine na kuoa. Mapenzi inayopewa ninajuta kwa nini nilipoteza miaka 3+ kwa 'umbwa' yule.

Umbwa tena [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Pole sana mkuu. Jogoo hafi kwa utitiri. Jipe muda kwanza utulize akili. Najua atakutafuta ila usithubutu kujaribu kumfikiria tena. Funga huo ukurasa
Wanawake huwa ni mafala sana, yani anaweza akakuacha muda ambao hautarajii halafu ukiwa na msimamo na ujasiri usibabaike na maamuzi yake baada ya muda anakutafuta,, na ukisema umrudie tena hamkai muda mrefu mnakosana tena vibaya vibaya
 
Na pia nadhani ulijitoa sana kwake kwa kila kitu. Going forward be careful unapodeal na mwanadamu; na angalau uwe tayari kwa lo lote maana mwanadamu anaweza kubadilika wakati wo wote. Jitoe kwa upendo huku ukijua kuwa ni sadaka tu unatoa lakini siyo kwa kutegemea cho chote maana kusema kweli loyalty ya mtu huwezi kuinunua ama kwa material things wala upendo wako wa kweli. Mwanadamu anaweza kuwa kiumbe katili sana akiamua!

Lakini pia kama malengo yako yalikuwa safi kwa huyu binti (if your intentions were pure) basi ondoka na dhamira safi huku ukijua kuwa hukumpotezea muda wake...and the Universe will reward you handsomely. Mwache aende na mtakie mema ila usije ukashangaa huko mbele ya safari kama atataka kurudi tena.

Kwa sasa hakuna njia ya mkato. Kuumia ni lazima utaumia lakini utavuka. Kwa kadri muda unavyokwenda maumivu nayo polepole yatapungua; na nati hizo zinazokaza kwenye moyo zitaanza kuachia na furaha yako itarudi.

Na ni lazima uchukue tahadhari. Usije ukaishia kuchukia wanawake wote. Huyu hakuwa wako na imeonyesha hivyo. Hata kama ungelazimisha basi huko mbele ya safari ungeumia zaidi ya unavyoumia sasa. Angalia tu usije ukaenda huko ukilalama na kuita kila mwanamke ni laghai, mbwa na malaya. Hutakuwa sahihi. Na siku moja utakuja kumpata aliye wako ambaye atakuonyesha mwanamke mwema na waifu matirio yukoje. Endelea kumtafuta mwanamke huyo kwa roho njema, moyo safi na dhamira isiyo na mawaa na siku moja utampata tu.

Sasa umekua! 👏🏼👏🏼👏🏼💪💪
Kuna madini mengi sana hapa 👍
 
Back
Top Bottom