Nimeachwa

Kwanini uwe abmormal kwa sababu ya mwanamke?
Wapo wengi sana..
 
huyo si mpentekoste, bali ni mpendakote!

pole sana mpendwa!

mpenzi wangu katika BWANA WA MAJESHI ulipotelea wapi tumekukosa sana humu jamvini..................hivi kwa nini wasema ni mpenda kote na huku kamtupia mkatoliki mwenzangu virago vyake.................

nionavyo kwani hakujua awali ya kuwa anaswagana na mkatoliki?
 
Huyo kapata mtu mwingine, anasingizia dini. Alikuwa wapi siku zote asijue kama wewe ni RC? Pole, mwombe mungu atakupa wa kufanana nae!
 

mpendwa, Ruta,

mi nipo tu humuhumu jamvini, naona labda tunapishana tu majukwaa mpendwa.

nimesema huyo ni mpendakote kwa kuwa nimeassume kuwa mr. creative alikuwa na uhusiano ya kijinsia na huyo mpenzi wake na sasa mwenzie kamuacha na ameanza kuchanganyikiwa kisaikolojia. kama ndivyo basi inaonekana hawana ndoa na hivyo hayo mahusiano yao yalikuwa premarital au extramarital affair.

huyo binti nimemuita mpendakote kwa kuwa anaonekana anapenda uzinzi na pia anapenda mambo ya Yesu (kwa kuwa ametambulikana na mr. creative kama mpentekoste), kama asingekuwa hivyo, basi asingejihangaoisha na uzinzi kabla ya ndoa na kama wangekuwa na ndoa na mr creative, basi wasingeachana kwani Bwana anakuchukia kuachana kwani ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alivyotufundisha na ametuamuru kuachanishwa na kifo tu. hii ni kwa wapentekoste na wakatoliki sawia

ubarikiwe sana mpendwa Ruta

tumsifu Yesu Kristu!
 
Mmekuwa wote mda gani?
Je, mliwahi kugusia swala la utofauti ktk dini zenu? na kama mligusia mlifikia muafaka gani?
Isijekuwa ulimwambia mambo ya dini hayana shida unaweza kubadilisha na baadae ukakataa, make nayo nimewahi kuona kwa vijana wengi na mwisho wao unakuja kuwa kama wa kwako.
Ila usikate tamaa kama kakuacha utampata mwingine ambae mungu amepanga muwe wote
 
ni muda kama wa miezi miwili,suala la imani alilingumzia yeye alitaka niende kwenye imani yake ambacho ni ki2 kisichowezekana au wewe unaonaje?
 
Kwani umejuaje kuwa kisaikolojia uko - abnormal? Ungekuwa abnormal ungeshafanya mambo ya ajabu hata kwenda kwa sangoma..

Sasa ndugu yangu kumbuka..mahusiano hayana dini..ila mahusiano yana mwisho tupende au tusipende. Na mwisho wa mahusiano siyo mwisho wa maisha ni sehemu tu ya maisha..

Kuna sababu nyingi za mwisho wa mahusiano hiyo ya dini ni moja kati ya elfu... mkichokana unaweza tumia dini, hela, ulevi, umalaya ..sababu ziko nyingi..

Cha maana kumbuka dalili za mvua ni mawingu...Labda tu kama mtamaliza tofauti zenu..lakini ni vizuri ukaanza kufuatilia haki zako za msingi na kujua mwisho wa mahusiano siyo mwisho wa maisha kwani ulizaliwa peke yako!
 
mpendwa mr. creative,

ulishawahi kusikia majaribu yaliyompata Ayubu? hebu yachukue maisha ya Ayubu kama "template" kisha uchukue maisha yako na uyafit ndani yake kisha utuambie kama kwa hayo yaliyokupata bado una sababu ya kuchanganyikiwa. kama unampenda sana huyo mwenzio, mwambie Yesu na kama ni mapenzi yake atamrudisha kwa wakati wake, la si mapenzi yake, mshukuru Mungu kwa kukupa nafasi nyingine ya kujipanga upya na kukuepusha na lile ambalo wewe kwa akili zako hukuweza kuliona likikujia!

zaidi sana umshukuru Mungu kwa maisha ya mwenzio na angalu kwa siku alizowajalia kuishi pamoja kwa furaha, kumbuka wako wengi wanaompenda lakini huishia kumtazama tu akipita na hawakuwahi kupata hata fursa ya kuongea naye, sembuse wewe ulipata kibali cha kumuita "mpenzi wangu" naye akaitika?

siku zote ulibariki jina la Bwana mchana na usiku

ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…