Nimeagiziwa sumu ya panya

Flamegood

Senior Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
129
Reaction score
293
Mahali ninapofanyia shuguli zangu kuna mkaka kapita na baiskeli ni hawa wanaouza sumu za panya "habari, kuna dada nimepishana nae hapo nyuma kaniambia nikuletee sumu ya panya" me nikashangaa sana He!

Nikamuuliza kwani huyo dada yupo wapi akajibu nimepishana nae alikuwa anaelekea upande uleee" (alinionesha uelekeo), me nikamjibu "Hapana, labda umekosea mahali na si hapa maana mimi cjaagiza sumu" kijana akaondoka zake kwenda kuuliza pengine.....

Je, ni kweli kijana aliagizwa kwangu au ni mbinu yake ya kibiashara? Na kama aliagizwa kwangu kweli huyo dada ana maana gani? Au alikosea mahali alipoagiziwa aipeleke?
 
Mambo mrembo..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…