Nimeambiwa mishipa midogo katika moyo wangu haipati damu ya kutosha hivyo imenisababishia maumivu upande wa kushoto

Nimeambiwa mishipa midogo katika moyo wangu haipati damu ya kutosha hivyo imenisababishia maumivu upande wa kushoto

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habari wakuu,

Nimekua nikisumbuliwa na maumivu ya upande wakushoto ktk bega na nyuma ya bega usawa wa moyo nimefanya ecg na echo nimebiwa echo Iko sawa. Ila ecg inaonyesha shida kidgo nkaambiwa haya maumivu yanasabishwa na mishipa midogo midogo iliyoko katika moyo haipati damu yakutosha. Nikauliza inatokana na nin akasema inatokea tu. So Ina nkapewa aspirin.

Wakuu nakuja kwenu kuuliza vip huwa kunautatuzi wamoja kwa moja kuifanya mishipa midogo midogo ipate damu yakutosha nakumaliza kabisa tatizo la maumivu
 
Pole,

Daktari aliyefanya ECG ndo ana uwezo wa kusema lolote juu ya hili ua mabadiliko ya mwenendo wa umeme yaliyoonekana na kama yana hatari yoyote au la. Au yanahitaji tiba zaidi.

Jibu lingine unaweza kulipata kwa Invasive Cardiologist ambaye huweza kufanya vipimo zaidi vya kuangalia kiasi cha tatizo kwenye mishipa ya damu ya moyo na kama kwa kiasi husika unahitaji kufanyiwa chochote au la. Hii utaipata kwenye vituo mahsusi kwa magonjwa ya moyo kama Jakaya Kikwete/MNH VS Aga Khan nk.
 
Tatizo hili huwa linatokana na nin
Kuna sababu 21 na zaidi zilitajwa kwenye uzi uliouliza kama siku 2-3 zilizopita(Tatizo la umeme kwenye moyo).

Ili kupata sababu halisi hutegemea historia halisi ya mgonjwa husika, dalili, wakati gani, nini huongeza shida au kupunguza, aina ya mabadiliko ya umeme kwenye ECG nk.
 
Kaka nimepitia baadhi ya juzi zako unasumbuliwa na matatizo mengi kiasi lakn naomba nikushauri kama utafata ushauri wangu utapona kabisa tatizo lako

Tumia kitunguu saumu chukua punje za kitunguu saumu asubuhi meza punje 5 au 4 kwa Kutafuna then unatumia na maji kusukumizia
Mchana tumia mchana kiwango hiko hiko baada ya kula na tumia usiku baada ya kula

Kitunguu hutanua mishipa ya Damu na kitunguu pia hutibu matatizo ya Figo na ukawa sawa kabisa, kitunguu hutibu pia vidonda vya tumbo,husaidia pia kuondoa msongo wa mawazo, kitunguu huondoa cholesterol,mafuta yaliyopo kwenye mishipa ya Damu huondoka yote,hutibu pia UTI, hutibu pia Malaria sugu , matatizo ya moyo,bawasili

Kingine jitahidi Ufanye Mazoezi ya Mwili utoe jasho lakutosha mwilini,punguza Uzito , jitahidi Sana uwe unakuwa karibu na mungu wako usihambuliwe na mapepo mabaya,uchawi,majini na magonjwa nenda msikitini au kanisani hata kwa watumishi

Yote hayo bila kusahau kuacha kutumia mafuta ya korie, achana kabisa kula chips,acha kula vyakula vya wanga, asubuhi usile ukashiba kula kidogo tu,acha Matumizi ya sukari ni hatari ,acha Matumizi ya vyakula vya Ngano ni hatari si salama , Usitumie vinywaji vya viwandani kama soda na pombe nk.

Badili mfumo wako wa Maisha, maradhi hayatokwisha ukikaidi

Ukiuthamini ukale,Usasa hautokumaliza[emoji1621]
View attachment 2739880View attachment 2739881
 
Samahani eti magonjwa kama aya. Pia uchawi si unakuepo
 
Habari wakuu,

Nimekua nikisumbuliwa na maumivu ya upande wakushoto ktk bega na nyuma ya bega usawa wa moyo nimefanya ecg na echo nimebiwa echo Iko sawa. Ila ecg inaonyesha shida kidgo nkaambiwa haya maumivu yanasabishwa na mishipa midogo midogo iliyoko katika moyo haipati damu yakutosha. Nikauliza inatokana na nin akasema inatokea tu. So Ina nkapewa aspirin.

Wakuu nakuja kwenu kuuliza vip huwa kunautatuzi wamoja kwa moja kuifanya mishipa midogo midogo ipate damu yakutosha nakumaliza kabisa tatizo la maumivu
Pole kwa maumivu unayopitia. Kulingana na maelezo yako, inaonekana una hali inayohusisha mishipa midogo ya moyo (microvascular angina), ambayo inaweza kusababisha maumivu ya kifua au maumivu ya karibu na moyo, hata kama mishipa mikubwa ya moyo inaonekana kuwa sawa kwenye vipimo kama echocardiogram.

Hii hali husababishwa na kutokuwa na mtiririko mzuri wa damu katika mishipa midogo ya moyo. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo kama:
  • Mishipa midogo ya moyo kubana zaidi ya kawaida.
  • Magonjwa ya mishipa kama vile ugonjwa wa ateri za moyo, kisukari, au shinikizo la damu.
  • Inflamesheni (uvimbe) kwenye mishipa ya moyo.

Kuhusu utatuzi wa moja kwa moja wa tatizo hili, hapa kuna baadhi ya njia zinazotumika kusaidia kuboresha hali hii:

1. Dawa za kutanua mishipa ya damu: Dawa kama vile nitrates au calcium channel blockers hutumiwa kusaidia mishipa ya damu iweze kupanuka na kuongeza mtiririko wa damu.

2. Dawa za kuzuia kuganda kwa damu: Ulivyopewa aspirin ni sahihi, kwa sababu husaidia kuzuia kuganda kwa damu kwenye mishipa midogo. Matumizi ya dawa nyingine kama anticoagulants pia yanaweza kuzingatiwa.

3. Dawa za kudhibiti shinikizo la damu na cholesterol: Kama kuna tatizo la shinikizo la damu au cholesterol ya juu, dawa hizi zinaweza kusaidia kudhibiti hali hiyo na kuboresha mtiririko wa damu.

4. Mazoezi na mabadiliko ya mtindo wa maisha: Mazoezi ya mara kwa mara yanaweza kusaidia kuboresha mtiririko wa damu na kuimarisha afya ya moyo. Mabadiliko ya lishe, kama kupunguza mafuta yasiyo na afya na kula vyakula vyenye virutubisho kama matunda na mboga, pia yanaweza kusaidia.

5. Matibabu mengine: Katika baadhi ya visa, madaktari wanaweza kuzingatia matumizi ya tiba ya mwanga wa chini wa kiwango cha nishati (low-level laser therapy) au matibabu mengine ya kisasa kusaidia kuboresha mtiririko wa damu kwenye mishipa midogo.

Ni muhimu kuwasiliana na daktari wako mara kwa mara na kufuata ushauri wao kuhusu dawa na mtindo wa maisha. Kila mgonjwa ni wa kipekee, hivyo matibabu yanaweza kutofautiana kulingana na hali yako binafsi.

NB: Mimi sio daktari... Copy and paste.
 
Back
Top Bottom