Nimeambiwa nina damu nyingi je ugonjwa huu unaweza kuisha? Madhara yake yapoje mbeleni?

Nimeambiwa nina damu nyingi je ugonjwa huu unaweza kuisha? Madhara yake yapoje mbeleni?

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
3,996
Reaction score
5,156
Habari zenu wakuu,

Nilikuwa nasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa na mwili kuuma, ikabidi niende hospital kupata vipimo, majibu yakaja yanaonesha Nina damu nyingi ambapo ni 18 gm/dm (kama sijakosea vipimo)

Daktari alinambia kiwango cha kawaida ni 16 kwa me, na ke ni 14, hivyo alinishauri niwe natoa/kuchangia damu na pia akanisihi nisile sana mboga za majani na matunda kwa wingi, kwa sababu tayari nina damu ya kutosha, ni kwel nilikuwa natumia mboga za majan na matunda kwa wingi hivyo kanambia nipunguze badala yake ninywe maji ya kutosha.

Amenipa dawa nazitumia,je huu ugonjwa una weza Kwisha kwa kufanyaje na je madhara yke yapoje mbelen?
 
Endelea kula mboga za majani kwa wingi halafu kila baada ya miezi mitatu unaenda kuchangia damu
 
Ndugu kuchangia damu NI Jambo jema kabisa Ila kwahali uliyonayo kutoa damu itamlaximisha mwili wako kuzalisha damu Zaid ya hapo 18 ulipo NI vema ufate taratibu zingine za kupunguza damu Kama inshu ya kula Yan unaeza kula asubuh na mchana au mlo mmoja Kama utaweza, mie pia nimepima juz wakakuta 17.4 kwenye kutoa walinisii Sana naweza zalisha tatizo lingine kubwa hvyo hapa najaribu kupunguza kula tuu Mana hamna jinsi Ile Hali inajitokeza wakati fulan na kupotea Yan unahis ndo unaenda Kule tulikiambiwa lazima tutaenda hata iweje.

Pole jamaa hope tunapambana site kila Hali kushusha hii damu
 
Sawa hata hivyo alinisihi nipunguze kula kula ovyo especially mbiga za majan
 
Experiencing the same thing right now. Ee Mungu nisaidie
 
Habari zenu wakuu,

Nilikuwa nasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa na mwili kuuma, ikabidi niende hospital kupata vipimo, majibu yakaja yanaonesha Nina damu nyingi ambapo ni 18 gm/dm (kama sijakosea vipimo)

Daktari alinambia kiwango cha kawaida ni 16 kwa me, na ke ni 14, hivyo alinishauri niwe natoa/kuchangia damu na pia akanisihi nisile sana mboga za majani na matunda kwa wingi, kwa sababu tayari nina damu ya kutosha, ni kwel nilikuwa natumia mboga za majan na matunda kwa wingi hivyo kanambia nipunguze badala yake ninywe maji ya kutosha.

Amenipa dawa nazitumia,je huu ugonjwa una weza Kwisha kwa kufanyaje na je madhara yke yapoje mbelen?
Kuwa na damu nyingi, au hali inayojulikana kama polycythemia, ni tatizo la kiafya ambapo mwili wako unatengeneza seli nyekundu za damu nyingi kupita kiasi. Hii inaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwemo:

  1. Polycythemia vera: Hii ni ugonjwa wa nadra wa saratani ambapo mfupa wa ndani (bone marrow) unatengeneza seli nyingi za damu.
  2. Hypoxia: Ukosefu wa oksijeni ya kutosha kwenye tishu inaweza kupelekea mwili kutengeneza seli nyingi za damu ili kuboresha usafirishaji wa oksijeni.
  3. Matumizi ya dawa au virutubisho: Baadhi ya dawa au virutubisho vinaweza kusababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu.
  4. Hali zingine za kiafya: Kama vile matatizo ya figo au ini.

Madhara ya kuwa na damu nyingi​

  1. Kuongezeka kwa mnato wa damu: Hii inaweza kupelekea kuganda kwa damu, hali inayoweza kusababisha matatizo kama vile kiharusi (stroke) au mshtuko wa moyo (heart attack).
  2. Madhara kwa viungo: Kuongezeka kwa mnato wa damu kunamaanisha kuwa damu inapita polepole kupitia mishipa midogo, jambo linaloweza kusababisha matatizo kwa viungo kama vile figo.
  3. Dalili nyingine: Uchovu, kizunguzungu, maumivu ya kichwa, na matatizo ya kuona.

Matibabu na Matarajio ya Baadaye​

  1. Matibabu ya Polycythemia vera: Hii inahitaji uangalizi wa daktari na mara nyingi matibabu yanajumuisha kutoa damu (phlebotomy) ili kupunguza kiasi cha seli nyekundu za damu, na matumizi ya dawa za kupunguza uzalishaji wa seli hizi.
  2. Matibabu ya Hypoxia: Inategemea sababu ya msingi. Kama ni kutokana na hali ya juu (altitude), kuhamia kwenye eneo lenye oksijeni zaidi inaweza kusaidia. Ikiwa ni kutokana na ugonjwa wa mapafu, tiba za oksijeni na matibabu ya msingi wa ugonjwa inaweza kuhitajika.
  3. Uangalizi wa kiasili na maisha bora: Ikiwa tatizo linaweza kudhibitiwa kupitia mabadiliko ya mtindo wa maisha, unapaswa kufuata lishe bora, kufanya mazoezi, na kuepuka uvutaji sigara na unywaji pombe kupita kiasi.
Muhimu: Ni vyema kufuata ushauri wa daktari wako na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili kudhibiti hali hii.
 
Back
Top Bottom