Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

Nimeambukizwa virusi vya UKIMWI (H.I.V)

DR. Msigwa niliangalia mahojiano yake kwenye Tv alisema NIMR wamemzungusha.

Labda nenda katibiwe ukirudi umepona tuitumie kesi yako kama ripoti ya mtu mmojammoja anecdotal evidence

Na nipo interested kama kuna mtu ametibiwa na Dr Msigwa akapona hebu ailete ripoti yake hapa!

Na kama ndo wewe mwenyewe Msigwa uloandika au chawa wake, naomba jazeni hii uzi kwa shuhuda halisi. Asanteni
 
Tumia dawa za hospitali mkuu, Hawa kina msigwa sijui kama wangekua wanaweza kutibu ukimwi kabisa tusingekua tunahangaika nao na haya mafuriko, wangekua kwenye Forbes list huko!!!
 
Mdogo Angu soma hapa ni muhimu USIACHE Nitaandika maelezo marefu kwa sababu inahitaji kuongea zaidi ili uweze kuelewa plz nitajaribu kufupisha kadri navyoweza !

Polee Sana!

Matatizo tumeumbiwa binadamu,Kikubwa ni kuamini kwamba kila linalotukuta lina sababu Japo si Rahisi kuijua sababu kwa mara moja!

Kwanza kabisa Unaonekana bado upo kwenye denial na bado huamini kama Kweli unaweza kuwa na maambukizi, tuliza akili Mdogo wangu huu wakati ulionao ni wakati ambao akili yako bado haiamini kila kitu na inaamini sana kuwa bado muda unao na unaweza kupona na kuondoa Virusi hivyo mwilini..

Huu ni wakati ambao akili yako inaamini kuwa HIV ni kifo na kumbe swala hilo si la kweli!

Kwenye wakati huu wengi sana hupotea na tunapoteza Wengi kwa kukosa washauri wenye uelewa mzuri wa maswala ya maambukizi na wengi huamini kila kitu wanachoambiwa na kuona mitandaoni, Na huku wengine wakitapeliwa Pesa nyingi sana huku tatizo lao likibaki pale pale..

Huu ni wakati ambao unapaswa kutulia na kufata ushauri wa Daktari na washauri wengine mahali ambapo umeanza huduma ya Tiba na matunzo nafikiri kuliko wakati wowote ule....

Mpaka Sasa Si WHO, CDC,CRO, Medspace wala NIMR waliotangaza Dawa ambayo huenda ni mbadala wa ART..
Japo bado baadhi ya reseaech na procedure zinaendelea....

Kwahiyo ukitoa pesa ili kupata suluhisho la hilo tatizo lako utakuwa unaibiwa....

Na mdogo wangu naomba nikushauri katu asije mtu yoyote kukudanganya kuhusu Kuacha kutumia Dawa za ART kwa kigezo utumie Dawa zake...

Kwa sasa katika mwili wako kuna High production ya Virus wanamultiply sana na ndo maana ni wakati mbaya sana kuacha kunywa dawa!
HIV virus Si kirusi kinacho attack nutrients za mwili kwamba utakunywa dawa yenye protein ili kuzidisha protein na kufanya Waondoke mwilini...

NGOJA NIKUPE SOMO KUHUSU HIV NA DAWA ZA ART ZINAVYOFANYA KAZI ILI UPATE UELEWA KUWA ART NI BORA KULIKO HIZO MITISHAMBA

HIV Ni ina kirusi cha RNA na kinafahamika kama Retrovirus kwa kuwa kina tabia ya kujibadili na kuwa DNA kwa Kujichanganya Na vinasaba vya Mwili wa binadamu na hapo ndo huweza kubadili baadhi ya commands kwenye mwili na ku alter information za kawaida za mwili na kuamrisha mwili kutengeneza Wadudu ama virusi wengi kadri iwezavyo...

Utengenezwaji huu na upangwaji wa Virusi (Virion)
Hufanyika kwa haraka sana ndani na nucleas na nje ya nucleas ya Cells za binadamu katika hali hiyo cells nyingi hushindwa kuhimili Hali hiyo na nyingi huwa weak na kuharibika...sana sana hizi Tcells aina ya CD4 Kwakuwa ndiyo attachment yake na receptor au kufuli l funguo yake ndipo lilipo...

Kuna hatua kadhaa hufanyika ili kirusi kiweze kutengenezwa na kuharibu cells hatua hizo ni...
  • Kufungamana au kujishikiza kwenye cells ambayo ni cells ya CD4 (CD4 receptors- CCR5) kwa lugha nyingine huitwa Binding au Attachements
  • Kuungana au Fusion kirusi huingia ndani ya cells na kutoa vitu vyake vilivyo ndani..
  • Kujibadilisha kwa lugha nyingine huitwa Reverse transcription--kwakuwa RNA ni vigumu kuweza kufanya transcription (Kutoa order katika miili yetu kumbuka order hutoka kwa DNA na hutumwa kwa mfumo wa mRNA) virusi hufanya reverse transcriPtion yaani hujibadili kutoka HIV-RNA na kuwa HIV DNA na hapa ndo shida huanza..
  • Hatua inayofuata ni kujizalisha kwa wingi inavyowezekana ili kupata virusi wengi hatua hii huitwa Replication..
  • Kwa kuwa Ndani ya cells katika replication ni utengezaji wa material tu hatua hii hufanyika Kupanga material zote zilizotengenezwa huitwa assembly
  • Hatua ya mwisho ni budding ni kutoka kwa ile ile virus zilizotengenzwa ili zikomae na kwenda kufanya hatua hizo kwenye cells nyingine....
Nafikir umeelewa kuhusu hizo hatua zote...
Hakuna dawa yoyote ya mitishamba itakayozuia hatua yoyote kufNyika....
Sasa ART ina kazi moja wapo ya kuzuia hatua hizo kufanyika ili kuzuia uharibifu wa cells zaid na kuongeza kinga kwa kufanya hivyo...

Kuna dawa za ART Zinazuia kufanyika kwa...
binding/attachments tunaziita CCR5 antagonist pia zipo Post attachment inhibitors
Pia zipo zinazuia hatua ya Fusion (Fusion inhibitors)
Hatua hizi za mwanzoni huwa ni ART za sindano na kwa Tanzania bado hatujawahi kuwa nazo kwa sababu ni ghali...
Na hatua zinazofuata zote huwa na inhibitors zake..
Lengo la kuzuia HIV kufanya hivyo vyote ni ili ishindwe kuzaliana na Mwili utashughulika na HIV zilizokuwa weak na hazieleweki through engalf system ya macrophages..

Sasa kwanini nimekuambia yote haya kwa sababu ya kukujengea Kujiamni mwenyewe kuwa bado Una nguvu na wala Usiwaze kuhusu hicho unachowaza uko sawa na kutumia dawa kutakuweka katika afya nzuri sana..

Ukiacha kutumia dawa kwa hali yoyote ile utasababisha usugu wa Dawa (Drugs Resistance) ambayo inaweza kupeleka kufail kwa matibabu ya ART (ART drugs Failure) na ukifika huku inakuwa ni hatari sana...kwa sababu ART tena haitaweza kufanya chochote kwwnye mwili wako..

Kwahiyo jitahidi unywe dawa kwa wakati na baada ya miezi sita Angalia hali ya virusi kama unatumia dawa na lishe bora unaweza kujikuta upo kundi la watu walio na kiasi kidogo sana cha HIV (TND for HIV in HVL- Target Not Detected for HIV in HIV VIRAL LOAD)..

Najua ni Safari ndefu lakini ni fupi kama utajiamini na kuondoa hofu yoyote..
Asante kwa muda wako..
Na kama una swali unaweza kuuliza

NB: hakuna mtu aliyepima HIV positive baada ya muda akawa negative unless kafanya Bone Marrow transplant na yenyewe huwa ina 5% ya curetage...
 
Ok Nitakujibu,

kwanza kuna PrEP na kuna PEP...

PrEP ni Pre Exposure Prophylaxis
PEP ni Post Exposure prophylaxis

PrEP hutumika kabla ya mtu kuwa exposed yaani kwa mfano unaenda kufanya Huduma ambayo unahisi huduma hiyo itakuweka karibu zaidi ya kupata maambukizi huwa unashauriwa kutumia PrEp masaa 2 mpaka 24 kabla ya huduma hiyo...(wanaotumia sana wanajiuza na watumishi wa afya kwa huduma ambazo ni delicate na lazma zifanyike)

Hii huzuia maambukizi yasitokee simply kama nilivyosema awali kuna process ambazo Kirusi hupitia kabla ya kusambaa na kushambulia cells...PrEP ni hizo hizo ART unapewa kwenda kublock hizo process Zisifanyike..
Nikuibie siri tu kati ya Virus wote HIV ni kirusi kilicho weak sana kwahyo unapozuia baadhi kwenye hatua ya mwanzoni unawafanya washindwe kuendelea na kujibadilisha hivyo wanakuwa weak n a mwili unafanya engafing kutumia macrophages na kuwaondoa kwakuwa wanakuwa hawana nguvu wakiwa RNA ...

Kwahiyo ili asifike kwenye Advance stages ndo maana kuna masaa ya hiyo dawa kufanya kazi kwa PrEP nafikiri unjua kuwa ni masaa mawili mpaka 24 kabla ya kazi na inashauriwa tena baada ya kazi apate PEP..

SASA PEP inatolewa baada ya Mtu kuwa exposed na matukio au huduma ambazo anahisi zimemuweka kwenye hatari ya kuambukizwa...
Na hii ina muda ni mpaka masaa 72 baada ya kuwa exposed..
Jinsi inavyofanya kazi ni sawa na Prep..na ni sawa na ART..
una swali..?
 
Back
Top Bottom