Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Nimefunga lakini kuna vijana wengu wamepoteza ajira.
Mpaka kuna mmoja nasema huyu isijetokea sababu ya stress akarudia mambo yake ya ajabu.
Alikuwa drug addict baada ya kutoka sober akapata ajira hapa anajikimu na kazi yake anaipenda.
Haya sasa hivi hana kazi ile sh 2 aliyokuwa anaipata tena hana.
Sijui itakuwaje only God knows.
Hatari sana hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili balaa ni suala la how long will the crisis exist

BUT

Every body will experience the pain

Walianza mashirika ya ndege

Wakaja makampuni ya bahati nasibu

Wakaja sekta ya utalii na chain yote

Sasa ni ma hotel ya ndani na waendesha shughuli za masherehe

Wasanii, Wanasoka (hasa hasa Ulaya) wameanza kuumia (japo wao wana saving)

Wakati huo huo wajasiriamali wadogo wadogo kama wale wa minadani n.k.

Sekta binafsi kama shule binafsi na staffs wote, vyuo binafsi, daladala n.k.

Tutaenda na mwisho watumishi wa Serikali wanaweza kuambiwa wapunguziwe % flani ya mshahara

Wenye nyumba za kupanga nao wameanza kuambiwa wawe wavumilivu kwenye kukusanya kodi

Hata hao wa hardware na wengine ambao kwa sasa wapo stable wataumia maana uwezo wa watu kununua utapungua, na vipaumbele itakuwa mahitaji ya msingi kama msosi ambapo watu watakuwa hawana hela za kununua

Najaribu kuwaza, mwakani tunaweza tusiwe na wanafunzi wa kidato cha kwanza, cha tano na wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni


Well hii thread ni kwa ajili ya wote tuliaoathiriwa kiuchumi directly na corona.
Najua kila mmoja atakuwa ameathirika kwa level yake lakini nawaongelea wale waliopigwa pigo takatifu. Mfano anayefuga kuku wa kizungu atapeleka wapi na alikuwa anategemea watu wa catering kwenye mashughuli, watu wa catering na mapambo jamani eeee ndo hivo tena tupige goti tu naimani Jehovah adinai atatusikia.
Kuna wale wanaofanya biashara za importation na exportation jamani poleni sana wenzangu hiki kilio chetu sote.

Wauza uji mihogo n. K mashuleni poleni sana.

Sasa usiombe corona ikuathiri kwa kiasi kikubwa na huku una mkopo sijui bank sijui microfinance haloo hao watu wanajifanya kama vile hakuna kinachoendelea wao wanataka rejesho tu ilihali mikopo wamesitisha na pengine hata wao mishahara wamepunguziwa kwa kiasi fulani ila sasa kwa kupiga simu na kudai hao balaaa.

Kama mimi mkurugenzi na muanzilishi wa kampuni ninalia lia njaa fikiria wale wa chini yangu hali ikoje?
Shughuli za uzalishaji hakuna lakini fixed costs kama hela ya pango na ulinzi lazima nilipie natoa wapi mimi hizo ilhali sizalishi?

Binafsi nimefunga ofisi nimefunga na nyumba nimerudi kwa bi mkubwa vijana wa sasa wanasema kurudisha jezi eee ndo nisharudisha jezi hivo.
Na hii ni biashara yangu changa sana niliyoipambania usiku na mchana isimame. Ninmeipambania haswa wanaojua nini nachofanya humu na tuna mawasiliano ya karibu wanaelewa.

Lakini corona imeipenda zaidi.

Ooo kuna watu watakuja na sera zao hapa huna saving sijui akiba uncertainties bla bla nyie ndugu kama ninavyosema kujiajiri ni kugumu sana hasa kukuza biashara jamani ukisema utoe laki uweke akiba unawaza hii laki si nikinunua kitendea kazi fulani kitasaidia mauzo yaongezeke? Basi unachukua ile hela unaongeza vitendeo kazi.

Wajasiriamali na wafanyabiashara mliokuwa kwenye game mda mrefu hongereni sana na SHIKAMOOOOONI maana najua mmevuka vizingiti vingi.

Wale jirani zangu jamani nishatoka kijijini nimerudi mjini kwenye ugali wa bure mnaweza kuja tu kunisalimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basically, hakuna ambaye hakuathiliwa na Corona kwanjia moja au nyengine ukiufatisha mnyororo wa thamani katika sector/Industry tofauti tofauti ila kuna walioathirika zaidi pia.

Corona imeathiri kwa aina mbili, wale walikuwa Field tiali ndio kama amu na wale walikuwa na mpango wa kuingia Field kwamaana imeathiri PLAN nyingi sana walizopanga watu.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 Kaka hiyo neema ukiipata usinisahau mdogo wako
Nitakuita Dada wa Mimi! Wala hakuna matata
 

Attachments

  • IMG-20200412-WA0128.jpg
    IMG-20200412-WA0128.jpg
    48 KB · Views: 1
  • Thanks
Reactions: amu
Mimi nimekimbia ofisi juz kat wamepiga mnada furniture za ofis yangu wateja wangu wengi ni mashule na makampuni ya utalii
Pia niliagiza mizigo china imekwama uko tangu february ndugu mteja anataka refund alaf mkulungwa niko juu ya mawe balaa
Yaan kua CEO wa vikampuni uchwara ni stress balaa kuitwa tapeli nje nje yaan
 
Back
Top Bottom