Nimeamini Kuna wazee wengine wana ukoloni na roho mbaya sana

Nimeamini Kuna wazee wengine wana ukoloni na roho mbaya sana

Senior Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
3,405
Reaction score
3,689
Salaam wakuu,

Nina hadithi ya kweli ningependa ku share nanyi. Ni kitu nimekishuhudia kwa macho yangu na kimetokea kuniumiza sana roho !!! Sumtyms huwa nikiwaza nakosaga na majibu kabsa. Ule usemi " Sio kila king'aacho ni dhahabu " ni ukweli kabisa na nime prove kwamba wakat mwngne kwenye maisha unaweza ona kitu flan kwa uzuri kumbe deep inside ni totally vice-versa (Ni shidaa na manyanyaso completely).

Well kuna familia moja iliyo karibu sana na familia yetu sisi kiasi tunaweza sema ni kama ndugu wa damu. Familia hiyo imetokea kubarikiwa na utajiri na mali nyingi hapa mjini. They are well off. Huyo mzee na mkewe nimetokea kufahamiana nao tokea miaka hyo ya nyuma pindi hawajawa na mafanikio makubwa kama ilivyo leo. Cha kushangaza huyo mzee ana ukoloni wa ajabu si kwa watoto hata kwa mkewe mwenyewe. Mzee ana magari ya kifahari amepark garage cha ajabu hakuna mtu anae tumia magari hayo ila ni yeye mwenyewe, hakuna cha mtoto wala mke yote anatumia mwenyewe, ana businesses nyingiza mamilioni ya hela lakn cha ajabu mke wake hasomeki hata ana shughuli gan ya maana anafanya. Mke wake ni mtu wa kupanda daladala daily na magari yapo nyumbani na kufanya petty businesses as if wao ni watu flan maskini sanaa. Mke kipindi cha ujana wake alikua na kichwa cha biashara sanaa kiasi kwamba alikua amewajengea na wazazi wake nyumba huko kijijini kwao miaka hyo ya 80's. Everything in her life started to fall apart alivyo olewa na huyo mzee.

Ukicheck huyo mwanamke ni mke wake ndoa na wamebarikiwa kupata watoto wazuri wenye maadili na akili darasani (Ni watu wazima sasa na wakubwa). Wametoka mbali yeye na mkewe tokea wakiwa hawana hata Tsh 100 wakiishi uswahilini nyumba za kupanga miaka hiyo..mke amepambana na kuvumilia yote na mumewe till wamekua watu matajiri sana lakn jinsi anavyo mtreat mkewe na watoto inasikitisha sanaaa !! Hii hali inasababisha watu wa raise questions. Mke kila anapo jitahidi kufungua a business of her own, mme wake ni kumpiga vita daily mpaka hyo biashara inakufa (ni biashara nyingi tu imekua hvi), mke havai vizuri kama wanawake wengine wa kitajiri. Huyo mzee anamletea dharau na matusi mkewe hata mbele ya ndugu wengine. Ni kitu flan kinawaumiza sana watu roho. Kuna wamama wanajua kuvumilia sana jamani. Nyie acheni tu.

Watoto wamemaliza vyuo with good grades lakn hamna hata mmoja unae weza sema ana kazi nzuri sehem au ana biashara flan ya maana anafanya. Mzee wao ana connections nyingi za maana na nzito lakn amezikalia tu hzitumii kusaidia jamii yake. They all live like peasants. The kids are very humble people. Ukionyeshwa na kuambiwa mzee wao ni mtu mwenye mali na businesses nyingi za maana mjini hapa huwez amini, utabisha mpaka panakucha. Ni mambo mengi sana nimekua nikiyaona kwenye hii familia mengne siwez andika humu.

Sasa wanajamvi najiuliza kitu kimoja, haya mafanikio yana maana gan kama jamii yako haina raha au ku enjoy mafanikio yako wewe baba ukiwa kama kichwa cha familia ??? Inakua kua vp mzee unakua na ukoloni kihivyo hata kwa mkeo ambae amekesha akikuombea kwa Mungu mfanikiwe na kuishi maisha mazuri ?? Hayo mahela yote umekua ukimtafutia nani miaka yote hiyo ??? Ni mchezo flan wa kukomoana au inakua vipi ??

Ushauri kwa wanawake: Hakikisha kwa namna yeyote ile ndoto zako hazipotei na kufa wakat unapo ingia kwenye maisha ya ndoa !! Sisi wanaume wakat mwingne tuna roho mbayaaa sanaaa. Its like mtu anapata mke mchapa kazi lakini still unakuta hataki ashike hela. Akifanikiwa kidogo ni matatzo. Ina raise maswali mengi sanaa wakat mwingne.
 
"Ndo ulivyo utajiri wetu wakinga mtuache tunajijua wenyewe"
 
Dah..! Nimependa sana huo ushauri uliuotoa kwa sisi wanawake hapo mwisho wa thread yako! Asante

We acha tu, kweli tembea uone. Ndio hvyo we kazana asije mwanamme yeyote akakukalia kichwani. Watu wana build dreams together asa unakuta mwenzio ndio kwanza anataka aizime ndoto yako. Ni ajabu sanaaa !!!
 
Duh aya mambo yapo sanaa kuna mama mmoja n jiran yet mmewe ana gar bt yy ukanyaga ya mguu na nmeshuhudia akimpita mkewe mara kibao kama amuoni vile......halii hii inatupelekea wanawake wa skiz tushindwe mvumilia mtu kivyangu ctokuja mvumilia mwanaume inauma sanaa
 
Wanasema ukitaka kujua tabia ya mtu subiri pesa imtembelee...
 
Duh aya mambo yapo sanaa kuna mama mmoja n jiran yet mmewe ana gar bt yy ukanyaga ya mguu na nmeshuhudia akimpita mkewe mara kibao kama amuoni vile......halii hii inatupelekea wanawake wa skiz tushindwe mvumilia mtu kivyangu ctokuja mvumilia mwanaume inauma sanaa

Alaf unakuta mmetoka mbali na mwenzio...mshakula sana viporo na matembele. Leo mtu anakufanyia hvyo. Kukupa hela ya matumizi we mkewe ni shida. Hivi mara zingne mtu hujishtukii au ni kitu gan ??? Na watoto wanaona kila kitu ni vile hawaongei tu. Daaaah !!!!
 
Mambo ya ndani ya mtu ndugu huwezi kuyaingilia kule kwetu kuna usemi usemao "numba tsa wandu tsiorye shiriha" nauzingatiaga sana kujaj mambo ya ndani ya watu.
 
Namna hiyo mi ndio maana huwa nasema bora uolewe na mume tajiri hata akikunyanyasa na vitu vyake haiumi sana..... Mtu amezima ndoto zako mmekula matembele,mkajinyima kwaajili ya kuwekeza mwisho wa siku anakufanyia ushenzi kama huu...kwa kweli mi atanisamehe tu. Nitapita njia za panya nimuibie tu. nyooo...
 
Unqtaka mama apande gari ili pesa ziyayuke enhe?
Ukitaka kujua watu wanavyoish mbona utajichosha tu
 
Namna hiyo mi ndio maana huwa nasema bora uolewe na mume tajiri hata akikunyanyasa na vitu vyake haiumi sana..... Mtu amezima ndoto zako mmekula matembele,mkajinyima kwaajili ya kuwekeza mwisho wa siku anakufanyia ushenzi kama huu...kwa kweli mi atanisamehe tu. Nitapita njia za panya nimuibie tu. nyooo...

Inauma, Inakera, Inaboa, Insikitisha !!! Mungu anaona yote.
 
Back
Top Bottom