Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Mke ni ubavu wa pili kwasababu tu ya mapishi?

Inaonekana Tangazo la rombo hotel hujawahi kuliona

It's Scars

Hahah am from Rombo I know about Rombo more than you do
Usichokijua mke wangu huwa anaamka asubuhi sana anapika kama ni chapati, au maandazi au mihogo
Sijawahi kula kitafunio kilicholala
Nikiwa nyumbani nakula vyakula fresh na vya kuburudisha nafsi
Leo hii nimejua umuhimu wake kwa upande wa mapishi

Ila nimemzungumia mke wangu kaka sikumanisha wake za watu wote; nimemmis sana wakati napika jikoni
 
Hongera Sana kwa kupata mke anaejua Mapishi
Nimemkumbuka Mzee mmoja aliwahi kuniambia
Raha ya mke ni mke anaejua kucheza na mwiko jikoni

Namuomba Mungu na Mimi nipate Mke kama wakwako
Maana kila siku nakula vyakula vya hovyohovyo
 
Hongera Sana kwa kupata mke anaejua Mapishi
Nimemkumbuka Mzee mmoja aliwahi kuniambia
Raha ya mke ni mke anaejua kucheza na mwiko jikoni

Namuomba Mungu na Mimi nipate Mke kama wakwako
Maana kila siku nakula vyakula vya hovyohovyo

Nashukuru sana ndugu
Ushauri wa mzazi usiupuuze hata kidogo shika kama unavyoshika sala
Kwa kweli kitu ambacho sikipendi kabisa ni kwamba vile vijiko kwa mama ntilie vimeingia midomo mingi sana

Mke mwema anatoka kwa Mungu tu hakuna njia ya mkato. Ukiomba utapata tu pasi na shaka. .
 
Umejua kunichekesha looh, asante.

Kati ya wanaume nnaofahamiana nao, wengi wao wanajua au wanapenda kupika.... Kila nikiwaambia naomba nije kuonja mapishi yako wananipotezea...

cc: Asprin
 
Umejua kunichekesha looh, asante.

Kati ya wanaume nnaofahamiana nao, wengi wao wanajua au wanapenda kupika.... Kila nikiwaambia naomba nije kuonja mapishi yako wananipotezea...

Mie nilikuwa naona kazi nyepesi. Mungu awabariki wapishi, ila wewe unajua kupika?


Inawezekana wanakimbia kwa sababu hawajui kupika. Watu wengi wanajinadi wanajua kupika hususani wanawake ila mapishi yao mabovu. Ukikutana na mtu lazima ajipe ujiko au sio?
 
Tatizo sio mkeo kuondoka,,Tatizo hujui kupika.

Mke wangu ni my other half
Kuna watu wanapika kila siku na hawajui kupika (wanakaanga tu)

Mke wangu anatimiza mahitaji yangu ya mie kula chakula bora na mie namtimizia mahitaji ya maisha bira
Sio dhambi kutojua kitu
 
Wakati bimkubwa na dadazangu walipokuwa wananifundisha kupika nilikuwa nachukia sana lakini sasa naiona faidayake
 
Wakati bimkubwa na dadazangu walipokuwa wananifundisha kupika nilikuwa nachukia sana lakini sasa naiona faidayake

Kongole kwa bi mkubwa na dada.
Unaweza kupika vyaula aina tofauti?

Unajua ukijua kupika huwezi kosa hata kazi ni kipaji
 
Najua kupika vyakula tofauti tofauti adi nipoishi wanishangaa

Lazima washangae, ngoja niweke ndani ya malengo yangu mwaka huu by december lazima ni post nimefikia wapi

Ila wanadai wanaume wanajua kupika zaidi ya wanawake, wako makini sana, sijajua kama kuna ukweli ndani yake
 
mwanaume mzima unapata wapi ujasiri wa kukaa jikoni na kupika chapati?
 
ujifunze pia siku mkeo akiumwa na wewe umpikie

Sent using Jamii Forums mobile app

Kabisa natakiwa nifanye hivyo
Nishwaweka kwenye malengo yangu

Siku hizi na hawa dada wa kazi basi unakuta huoni umuhimu wake. Siku ukiwa alone lazima ujue umuhimu wa kujua kupika
Nataka nijifunze kupika vitu simple sana
Vyakula vyenye urahisi zaidi kulingana na mda wangu
 
We nae acha uzembe bana. Mbona kupika kazi rahisi tu. Anyway, niko napika hapa. Eti ukizidisha chumvi kwenye tambi unafanyaje waungwana? Au nitafute chips?
Dah.... Chumvi gani unatumia mkuu? Sodium Chloride au Potassium chloride? [emoji2960]

Sent using Beretta ARX 160
 
mwanaume mzima unapata wapi ujasiri wa kukaa jikoni na kupika chapati?


Wanaopoka hotelini ni wanawake

Umeamua kunitusi tu
Unahisi kutakufanya ujisikie mwanaume jasiri kunifedhehesha
Hongera
 
Back
Top Bottom