Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Lazima washangae, ngoja niweke ndani ya malengo yangu mwaka huu by december lazima ni post nimefikia wapi

Ila wanadai wanaume wanajua kupika zaidi ya wanawake, wako makini sana, sijajua kama kuna ukweli ndani yake
Ukweli kabisa, wakati wa kupika vile mnavopika kiaina mtu anaweza hisi unaboronga msosi

Ila baada ya kuiva na kutenga mezani huo utamu wake sasa unaishia kujiramba na kutamani upikiwe tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na hongera.Ila ulichagua pishi gumu Sijui Kwanini.Umenikumbusha kuna siku nlikua naumwa mr.akaingia jikoni alinipikia mchemsho mzuri wa samaki.Ugali ndo alichemka alipika mkubwa Sana alishindwa kukadiria maji.Mwenyewe akasema tutakula mchana na usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Its so funny eti mke kasafiri halafu eti mwanaume unaingia jikoni kupika mpaka unachukua na picha na ku-upload JF!

Whats this?

Niingie jikoni tuseme sina vitu vya kufanya?

Tuseme hoteli zote na baa zote,Chinese restaurants,KFC,Merry Brown and some shit like that vyoote hivyo nisiende agiza au hata kitimoto eti niingie jikoni napika mataputapu?

Aisee kuna watu wana muda wa kuchezea beyond measure!

Aisee wanadamu tunatofautiana sana!
 
Bora yako wewe unaweza kutengeneza irregular chapati, mimi najua kuzichoma tu zikiwa duara tayari. Ia ndizi, wali, ugali wetu wasukuma, samaki kukaanga, nyama, napika hatari.
 
Mwanaume lazima ujue kufanya vyote kama usafi, kupika na kadhalika. Ina maana mkeo akiumwa au kusafiri we utaishije? Au kabla hujaoa ulikuwa unaishije? Huwezi kula take away kila siku. Hakuna kitu kizuri kama siku moja moja kutenga kamuda na kuipikia familia hii ina raha yake sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah aise mazee asikuambie mtu hawa watu wanne Mama, Mke, Dada na Dada wa kazi ni wakuheshimu sana
Kuna siku nilibaki mwenyewe home nikasema wacha leo nipike ugali c naonaga jikoni ukipikwa fasta fasta 15min mzigo tayari, sitakaa nirudie kuingia jikoni kwa yalionikuta.
Nilieka maji fresh kwenye jiko pamoja na sufuria shida ilianza kwanza sijui unatakiwa ujue kukadiria maji ujue ni ugali wa watu wangapi, mi nilijiekea maji.
Yalivochemka nikaanza kueka unga na kukoroga, kila nikikoroga mzigo hauwi mgumu yani unakua mwepesi zaidi uji.
Nikaendelea kueka unga yakaja mabonge mabonge makubwa, kimoyo moyo nikajisemea haya yanaishaga ukiwa mgumu wakati wa kusonga. Mzigo nikaendelea kutia unga , weka unga na mimi.
Dah aise nakuja kusonga na mwiko umekua mgumu mwiko hausogei nikajaribu na nguvu zangu zote kusonga, huku nasema mbona yeye anasongaga tu hivi chap chap. Nikalazimisha ule mwiko ukavunjika huku unga umejaa karibia jikoni kote kila mahali ni unga.
Nikachukua lile sufuria na unga wake pamoja na ule mwiko uliovunjika nikatupa vyote. Dah aise wanawake wana nafasi yao kubwa sana.
 

Hahah uliweza kula lakini???
 
Hata kama mwanaume huruhusiwi kuingia jikoni lakin mpaka huo umri hujui kupika chai!!??... Its so shameful!!! japo umesema hutaki dharau na maneno ila hapo umefeli sana..
 
Hata kama mwanaume huruhusiwi kuingia jikoni lakin mpaka huo umri hujui kupika chai!!??... Its so shameful!!! japo umesema hutaki dharau na maneno ila hapo umefeli sana..

Wengine wenye kebehi siwajibu ila wewe ngoja nipoteze mda kukujib

Umepata sh ngapi kunikebehi? Umepata faida gani? Usichukulie maisha yako ukafananisha na mie nilivyoishi. Usilazimishe 1 iwe mbili, hujui chochote kuhusu mimi alafu unakataka kuniponda.

Angalia maisha yako huna kasoro au wewe umekamilika
 
Kasoro gan ww? Kupika chai kunaitaji elimu gan kuanzia unakuwa mpaka ulipofika sasa....!![emoji19][emoji19]
 
Halafu kuna watu wanasema "mwanamke ni chombo cha starehe".
Btw, hiyo chapati iliyotoka ya mwisho ni zuri sana hongera.
Huyu jamaa ni mtaalamu huwekuwa hujui kupika chapati itoke bomba vile alafu ametoa na idadi ya kilo moja.

God save us
 
Hongera kwa kutambua umuhimu wa mke!Ila mkuu ungeacha uzi upumue,acha na wengine waandike tusome uzoefu wao au maoni yao!Sasa ukijibu kila comment wengine inatuchosha kupitia!Ungeweza kujibu comment chache zenye uhitaji wa kufanya hivyo!
Yaani mimi comments zake sisomi na si kwa urefu ule. Comment ndefu utafikiri uzi

God save us
 
Nimecheka sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…