Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Hongera kwa kutambua umuhimu wa mke!Ila mkuu ungeacha uzi upumue,acha na wengine waandike tusome uzoefu wao au maoni yao!Sasa ukijibu kila comment wengine inatuchosha kupitia!Ungeweza kujibu comment chache zenye uhitaji wa kufanya hivyo!
 
Huyo mdau hapo juu amejiandikia kujifurahisha tu mkuu,purukushani za kulea watoto hata kama mkeo akikuudhi vipi huwezi kumuombea kifo maana siyo mchezo mfano me siku nikisema nishinde home mpaka saa5 asubuhi nipo hoi maana vurugu za watoto usichukulie poa.

Hata hivyo nikupongeze umeweza hata kujaribu kukaanga chapati,ndo nimesikia kwako leo kumbe chapati na chumvi huwa zinawekwa?nilikuwa sijui aisee!!!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk

Kuna watu unaona waandika kujifurahisha ila wanaamini sana wanachokisema. Kwa kweli nasikitika kukutana na watu wenye mawazo hasi kwa sababu hujui mwenzako analipokea vipi. Unakuta ile hasi inakuwa kama Corona watu wanaambukizana tu unajikuta hata wewe umekuwa na mawazo hayo. Kwa kweli napinga sana

Nashukuru sana ila nimejifunza kitu, siku nikiwa home mke wangu akiwa anapika naweza hata kupika nae ili na mimi nijifunze. Akiumwa inakuwa kazi kubwa sana na watoto hata kuogesha unakuwa hujui

Watoto wanaumiza kichwa wakiwa home hata kushika PC nisema nachati swez mara huyu kashika TV
Huwezi kufanya jambo ukawaacha wenyewe
 
Hakuna league ya kuoa au kuolewa kila kitu kinafana pale kinapofanywa kwa mda wake maalumu
Bora ukosee kunyoa kuliko kukosea kuoa au kuolewa
Be blessed mpendwa. .

Kwa hapa Dar tena mitaa ya Sinza siku hizi biriani lina soko sana. Wanauza watu wengi biriani kuku sijui kuna kitu gani cha ziada. Hivi biriani linahitaji ufundi mwing sana?


Sina Hakika kama linahitaji ufundi mwingi kulipika au laah. Kiufupi sijalifatilia sababu sina interest nalo kuanzia kulila mpaka kulipika.
 
Sina Hakika kama linahitaji ufundi mwingi kulipika au laah. Kiufupi sijalifatilia sababu sina interest nalo kuanzia kulila mpaka kulipika.

Kuna vyakula unaweza jua jinsi wanavyopika ila ukawa hauna interest nalo it is true
 
Kwa kweli Mungu ni mwema sana na Namshukuru kwa siku hii ya leo. Imekuwa na changamoto nyingi sana hii siku ya leo ila najua nimezishinda na usiku umeingia hapa ni kwenda kulala tu hakuna purukushani za ziada.

Kwanza kabisa wife kasafiri kaenda kwa wazazi wake, leo nimejikuta niko kwenye mitihani kidogo. Mke wangu amejaliwa kweli kwenye mapishi, huwa akiwepo nyumbani amepika lazima niwahi nyumani nikapate maakuli. Napenda sana kula mimi na nafurahi sana kumpata mtu mwenye kujua kupika mapishi mengi sana.

Asubuhi imeanza nimeamka na njaa kali sana, imenibidi nikatafute sehemu nipate kifungua kinywa. Kwa kweli kila napoenda ukiangalia mazingira ya upishi na hata sehemu zenyewe kuna mainzi nimeshindwa ikabidi ninunue mkate nipike chai ninywe

Ile nimebandika chai nimeweka majani na sukari nikasubri ikachemka ili ninywe. Nilivyokunywa tu chai ilikuwa chungu sana kama mwarobaini. Ikanibidi nipige simu nimulize wife vipi mbona chai chungu majani leo mbona yaekuwa machungu. Akanijibu nitakuwa nimezidisha majani na yeye huwa anaweka vitu vingi zikiwemo mdalasini, iriki na vingine kanitajia sivijui. Kwa njaa ile nilimeza na ile mikate kama nyoka anavyomeza kuku

Mchana nikaona nipike chapatti, mbona siku zile wife alipika na niliona ni kazi rahisi. Yesu wahu ile jimechanganya unga na mafuta na maji ya chumvi, naona unadana mikononi tu. Kumbe nimezidisha maji ikabidi niende kwa mangi nikaongeze unga wa ngano. Ila kwa kweli nilikanda lile liunga mpaka mikono ikauma. Niliacha kwa mda nikaangalia taarifa za Corona Al Jazeera nisubiri kijasho kikauke kidogo

Nilipomaliza nikaenda washa moto jiko la mkaa (Jiko Koa). Ule mkaa ulikuwa umelowa na maji. Niliuwasha sana kama saa nzima hivi ndo mkaa ukawaka. Niliwasha na karatasi wapi nikajikuta nimechana daftari la mtoto la shule lote kesho nina kazi ya kwenda kununua jingine. Nikaenda store kwenye makorokoro nitafute tu hata kimfuko cha plastiki, nilipokipata ndio kikawashia moto

Kazi ikaja bhana kuzisukuma, nilisukuma sukuma sukuma kila nikisukuma duara haliji naona linakuja ovyo ovyo. Huwezi amini nilisukuma ile chapati moja nusu saa. Nikasukuma sana mwisho nikaona nipike hivyo hivyo. Ile kuiweka jikoni tu na mafuta wacha niungue lile frampeni lilikuwa la moto sana. Mkono wangu nimeungua karibia vidole vyote, cha kusikitisha ile chapatti ya kwanza ikatoka kama ina macho vile inanishangaa. Nimeshindwa kuila hii chapatti hebu angalieni inavyonitizama kwa dharau kama hivi:

View attachment 1378190

Nikapika chapati ya pili nayo imeunguwa imekuwa kaukau. Kwa kweli nimemkumbuka sana mke wangu na vyakula anavyonipikia. Nimejua hata kama mwanamke ni mama wa nyumbani hapaswi kudharauliwa kazi ya moto si kazi nyepesi ina shughuli pevu. Ukila chakula cha mkeo ujue ni damu yake, jasho lake, nguvu zake, upendo wake, maumivu yake ya kuungua nk. Kubeza chakula kilichopikwa na mwenzio ni dhambi kubwa Mungu atusamehe tu.

Ila nashukuru chapatti moja tu kati ya kumi na tano ndio iliyotoka vizuri nyingine nimeunguza sana. Sijui kama kesho zitafaa kula kiporo, ila kwa kweli kuna haja ya kujua kupika hata kama una mke. Nimekulia katika familia za kibepari mwanaume hakai jikoni, siwezi kujilaumu mwenyewe kwa kutojua kupika. Kwa kweli leo nimejua umuhimu wa mke wangu katika maisha yangu, Nakupenda sana Mke wangu, Mungu akujalie maisha magumu ukiniacha mwenyewe nitakonda. .
View attachment 1378191

At least this one came out better compared to others: (Sadly, It is the only one)
View attachment 1378193

Kwa jinsi nilivyoungua Yesu tu ndio anajua, Nawasisitizia tu tuwaheshimu sana wake zetu. Hata kutofanikiwa ni kwa sababu tu ya kutoheshimu nafasi za wenza wetu katika maisha yetu. .
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nachekaaaa nakufaaa...mpaka nmetimuliwa sebuleni na kupondwa na brush la Viatu kwenye matter call[emoji23][emoji23] chapati ina macho ya dharau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nachekaaaa nakufaaa...mpaka nmetimuliwa sebuleni na kupondwa na brush la Viatu kwenye matter call[emoji23][emoji23] chapati ina macho ya dharau

Sent using Jamii Forums mobile app

Nashangaa watu wote walio comment hawajaona

Aisee wewe macho yangu yako kama yangu. Haki ya nani yacheki yalivyokuwa yananitizama

Hahaha nani kakutimua sebuleni huyo?? Aisee pole sana
 
Yan nmejikuta tu out if control kicheko...nalipua balaa...alaf mama kantizama usoni km sekunde 6 bila kuongea..nikaona anaangaza kitu cha kunipondea nikaanza mbio...ila kimenipata duuuuh chapatii
Nashangaa watu wote walio comment hawajaona

Aisee wewe macho yangu yako kama yangu. Haki ya nani yacheki yalivyokuwa yananitizama

Hahaha nani kakutimua sebuleni huyo?? Aisee pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom