Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Nimeamini kweli mke ni ubavu wa pili

Dah....hapo atakuwa anatengeneza ugali wa ngano sasa [emoji1787][emoji1787]

Sent using Beretta ARX 160

Hahaha ungemshauri asonge kabisa apike na mboga za majani
Kumbe tambi ukizikoroga zinakuwa ugali wa ngano
 
Hahahahaha dah aisee
Ulivyokula zinalika kweli?
Usikute umekaanga kama nilivyokaanga chapati jana, ikawa kaukau

Fanya mpango uoe kaka kwa namna hii utakula chips kila siku
Haziliki mkuu. Nimekula chips. Wali, ndizi na ugali naviweza japo mara chache huwa nasahau kuweka chumvi. Sasa tambi nimekumbuka kuweka ila ikawa too much. Nadhani mwakani nitaoa ila sio sababu ya kupika. Kuna kitu inaitwa kufua hahaa!
 
Ujawai ishi mwenyewe yani ujui kupika dah pole sana man.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimekaa gheto kitambo sana. Ila kwenye ile nyumba kulikuwa na single maza sie tulikuwa tunachanga jioni tukija tunakuta keshafanya yake. Wapangaji single tulikuwa watatu na wote tulikuwa tunachanga
Aisee tulikuwa tunaishi kama home vile
Kuna watu wakarimu sana Mungu awazidishie
 
Uko vizuri
Ngoja nikazitafute huko Youtubute au ungetuwekea link kabisa kuna wengi wetu humu tuna hamasa ya kutaka kujua
Uki search tu youtube JINSI YA KUPIKA CHAPATI, utapata madini mengi sana. Bundle yako tu.
 
Zimenipiga knock out asee. Nitajaribu kurudia usiku kuzipika nikiwa kwenye mood!
Uweke chumvi kidogo na sukari kama unapenda.
Pia unaweza ukaweka sukari tuu.
Pia chumvi tuu inapendeza ila hakikisha unaonja maji kabla haujatilia tambi. Ukiona yamezidi chumvi mwaga maji uweke mengine.
Pia usipike nyingi maana zina tabia ya kukinaisha badala ya kushibisha.
 
Sikuangalia picha baada ya kusoma comment yako imenibidi nirudi kuiangalia..[emoji1787][emoji1787][emoji1787] amoeba huyu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app

Aisee huyo sio amoeba, ni chapati iligoma kabisa kuwa duara nikaona inanichelewesha
Amoeba has that shape?????
 
Pita hapo marikiti, kuna majani ya CHAI BORA ya MASALA. Tea bag unadumbukiza kwenye maji mchezo umekwisha. Ukitaka mbinu nyingine nishtue.

Yapo hayo mbona tena nayatazama hapa yana boksi la njano sasa sikuweka hayo
Haya naona yana vipakti ndani unadumbukiza kwenye maji ya moto
Niliweka majani ananunua yana mchanganyiko wa viyu vingi ikiwemo mchaichai, mdalasini nk
 
Uweke chumvi kidogo na sukari kama unapenda.
Pia unaweza ukaweka sukari tuu.
Pia chumvi tuu inapendeza ila hakikisha unaonja maji kabla haujatilia tambi. Ukiona yamezidi chumvi mwaga maji uweke mengine.
Pia usipike nyingi maana zina tabia ya kukinaisha badala ya kushibisha.

Wewe daa una maujuzi ya kupika
Umemshauri vizuri asiende kuzimwaga
Atakuwa amepoteza hela
Au zitakuwa na chumvi nyingi sana hawezi kuzila tena
 
Upishi nadhani upo ndani ya mtu...unakiwa ufeel ile hali ya kupenda kupika sio unapika kisa una njaa.

Wewe unaweza kupika vizuri kabisa?
Ulifundishwa na bi mkubwa toka utotoni au umejifunza ukubwn?
 
Uweke chumvi kidogo na sukari kama unapenda.
Pia unaweza ukaweka sukari tuu.
Pia chumvi tuu inapendeza ila hakikisha unaonja maji kabla haujatilia tambi. Ukiona yamezidi chumvi mwaga maji uweke mengine.
Pia usipike nyingi maana zina tabia ya kukinaisha badala ya kushibisha.
Thanks. Nadhani nilikosea kuweka chumvi, maana napenda tamu tamu. Nitaanzia youtube kabisa, ila nitakua nimeweka oda ya chips, ust in case hahaa!
 
Mie nilikuwa naona kazi nyepesi. Mungu awabariki wapishi, ila wewe unajua kupika?

Inawezekana wanakimbia kwa sababu hawajui kupika. Watu wengi wanajinadi wanajua kupika hususani wanawake ila mapishi yao mabovu. Ukikutana na mtu lazima ajipe ujiko au sio?

Yeah najua kupika.
 
Haziliki mkuu. Nimekula chips. Wali, ndizi na ugali naviweza japo mara chache huwa nasahau kuweka chumvi. Sasa tambi nimekumbuka kuweka ila ikawa too much. Nadhani mwakani nitaoa ila sio sababu ya kupika. Kuna kitu inaitwa kufua hahaa!

Hahaha unataka uoe afue. Akikudai house girl utafanya nini? Wanawake wengi wa sasa hawataki kazi za nyumbani kabisa. Utaletewe house girl afanya huku yeye kanyoosha miguu juu
Omba Mungu akupe mke mwema ndugu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimewapenda bure

Sent using Jamii Forums mobile app

Dunia ya sasa ukisikia mambo mabaya unaona kawaidaa. Zamani kidgo ukisikia hata neno jambazi au mbakaji ulikuwa unashangazwa sana. Kwa sasa yanaonekana ya kawaida sana

Upendo umepungua, nafurahi mno kujua kwako kuna wingi wa upendo
Thank you very much, please do not change. .
 
Chakula gani ambacho kiko complicated ambacho unajua kupika?
Mr anawahi rudi nyumbani kwa mapishi yako????

Sijaolewa

Ni biriani tuu ndo ambayo sijajaribu kupika, mengine yote napika.
 
Back
Top Bottom