Tetesi: Nimeamini Mhe. Mbowe sasa amekwama

Utajiri pekee anaomiliki kijana wa kitanzania ni simu ya smartphone
 
Kwa sasa ungeimarisha idara ya maafa na uokoaji ndani ya mkoa wako ingekua vyema zaidi kuliko kuhangaika na siasa.
 
Badala ya kupangua huo uongo unajikita kwenye chama tena hahahahahahaa Tanzania bana yani unawaza chama tu kupukutika thibitisha uongo wake
 
Sema umemuelewa.
Binafsi nilichoelewa kwa mbowe ni porojo alizopiga ili kuikera serekali akikamatwa ajifanye Bob wine
 
Tumekusikia,,,amekusikia,,subiri uteuzi
 
Unawaaibisha watu wa kwenu huko uyole, anyway swala la msingi ni pole kwa wahanga lakini mengine ni mambo ya kina Elton john tu....
 
Badala ya kupangua huo uongo unajikita kwenye chama tena hahahahahahaa Tanzania bana yani unawaza chama tu kupukutika thibitisha uongo wake
Suala sio uongo wake wala ukweli wake ,bali ni wakati wa kuanza malumbano ya kisiasa kwa wakati huu wa janga kubwa lililopoteza maisha ya watanzania wenzetu.

Ndio maana kuna somo la Sayansi ya siasa.
Lazima ujue kucheza na akili za watu kwa wakati sahihi.
Wafiwa kwa sasa hawahitaji siasa wala lawama mana hilo ni tukio la ajali sio tukio la kupangwa. Wahanga na familia zao wanahitaji kutiwa moyo na kusaidiwa kwa hali na Mali sio kusikiliza lawama ambazo hazitawasaidia kwa sasa.

Mbowe angeweza kuwahi eneo la tukio au angemtumia mbunge wake kuhamasisha uokoaji na kuopoa miili ya marehemu akiwa bega kwa bega na mkuu wa mkoa. Hakika angeheshimika zaidi na hata kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kuonyesha kuwa ana guswa na matatizo ya jamii zaidi.

Angefika kwenye eneo la tukio na kutoa hata sh. Mil. 5 kama motisha kwa vijana na askari waliokua wanaokoa na kuopoa miili ya wahanga angejijengea sifa yenye utu zaidi na angesifiwa hata na viongozi wa serikali. Angeweka pembeni kabisa masuala ya siasa.
 
Mbowe hadi atoe hizo hela kitengo cha majanga ambacho serikali inatenga bajet yake zinafanya nini? Ujue unaandika vitu virefu halafu hamna point jitahidi kujenga hoja kivuko mwisho watu kubeba 100 hao 200+ walikuwa wanakwenda wapi? Msimamiz wa kivuko cha serikali kawajibika?
 
akili ndogo hii, kila Mtanzania ana uhuru wa kuzungumzia chenye maslahi au kinachogusa Watanzania
 
Ugonile Mpoki,
Mpoki zimamoto haijawahi na haitawahi kufanya uokoaji baharini, ziwani hata mtoni. Mferejini inaweza, lakini magari yao hayawezi kutembea ndani ya maji na pia sidhani kama uogeleaji ni sehemu yao ya kazi licha ya magari yao kubeba maji. Kuweka injini mpya ni moja ya hatua ya usalama wa abiria kwenye chombo lakini cha muhimu zaidi ni kuwemo maboya au fulana za kuelea, bahati mbaya sijaziona kwenye picha za eneo la tukio. Hivyo nilivyovitaja ni lazima viwemo na Sumatra wanalazimika kutueleza kama vilikuwemo na vililingana na idadi ya abiria; Pia Sumatra wanalazimika kutueleza idadi ya abiria waliopanda kama inalingana na uwezo wa chombo, vyote hivi vinasimamiwa na serikali.
Vipi, mwenzetu ulipatapo kachimpumu kidogo kabla ya kuandika.
Msalimu Tulia.
 
[emoji26][emoji26]hatutoi rambirambi mkuu...Kama mnategemea rambirambi za mv Nyerere mkamnunue Kubenea mwaka huu mmekwama hapa Ni RIP tu....
 
Tuache siasa kwenye jambo hili.
Watu wamefiwa watu wanaomboleza.
Inauma sana.
Acheni masihara.
Naamini kabisa ndugu yako wa karibu angekuwa kafa kwenye hii ajali usiangendika hizi mambo humu.
Tuacheni tuomboleze. Siasa za kipuuzi tupa kule.
Jiwe hata Nusu mlingoti kagoma kushusha...
 
kwani kuna nafasi zilizo wazi huko????? mana naona kijana kajikamua kuandika upuuzi tupu...ka uchaguzi flan US embassy walitoa walio yaona mkabishana nao ,mbowe nae kasema yaliyo tokea bado mnabisha...halafu mnakaa kufurahia polisi kushangilia ushindi wa ccm...vijana kama ww ni tatizo
 

Siasa za Afrika msipojua kucheza nazo ikulu mtaisikia kwenye vyombo vya habari.

Mfuko wa Maafa ni wa serikali ya CCM wapinzani kwa sasa wanaonekana hawana umuhimu wowote mana hakuna mahali wanapojitokeza kusaidiana na jamii kutatua tatizo .
Nchi yetu ni tegemeze bado.
Tunategemea wahisani bado kwa hiyo kiongozi mkubwa wa Chama chenye wapiga kura mil. 6 kutoa mil. 5 kuhamasisha vijana ili wafanye ngumu ya kuopoa miili ya wahanga tena watanzania wenzetu hakika ingekua ni kiki nzuri sana ya kisiasa kuliko kuanza matamko ya kisiasa na lawama ambazo serikali itakapozijibu wananchi watazidi kujiuliza ingekua kuna ndugu zake Mbowe angeanzisha malumbano ?
 
Mkuu mmiliki wa kivuko ni serikali, hivi watanzania wapoteze maisha na pasiwepo na yeyote wa kunyooshewa kidole? Jifunze kuheshimu mawazo ya wengine hata kama ni machungu. Kubadirisha injini pekee siyo ufumbuzi wa kuzuia ajali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…