Nimeamini uchawi ni story za kusadikika tu.

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Niko mapumzikoni kijijini kwetu huku kwenye moja ya mikoa ya kanda ya ziwa.
Sasa kuna sehemu hapa kijijini kwetu pana mti mkubwa watu wanapaogopa sana,wenyeji wanasema ikifika saa 1 jioni ndio mwisho wa kupita hapo vinginevyo tegemea kukutana na mambo ya ajabu.
Sasa mimi hivi ninavyoandika saa 8 usiku huu ndio nimerudi nyumbani kutoka matembezi yangu na nimekatisha hapo hapo wanapopaogopa wao na sijaona wala kukutana na kitu chochote cha ajabu.
Hivyo basi nimeconclude kwamba uchawi haupo,ni story tu za watu.
 
MBONA MUDA HUU SIO SAA 8 USIKU?
TUTAAMINIJE UMEANDIKA UKWELI IKIWA UONGO UMESHAONEKANA?
 
Wahenga husema "hujafa hujaumbika" ila mi nasema "ukubwa ni jalala" sikutishi haitatokea Mtu yeyote akavunja rekodi ya ubishi wangu kuhusu uwepo wa uchawi ulimwenguni kote hadi yaliponikuta ila Mungu alinisaidia nikavuka hizo changamoto za kiroho.

Amini usiamini kila kitu kina pande mbili duniani; Bonde na mlima, mwanzo na mwisho, upend6na chuki, utajiri na umasikini, uchoyo na ukarimu, juu na chini, wingi na uchache, mchana na usiku, ukweli na uongo, faida na hasara, nene na nyembamba, mwanga na giza, kubwa na ndogo, ndefu na fupi, nene, iliyopinda, upole na ukali, tamu na chungu, nzito na nyepesi, dhoofu na imara, ndiyo na siyo, rahisi na ngumu n.k, hakikadhalika ishu za kiroho zina pande mbili "Mungu na Shetani" hulazimishwi kuamini ila habari ndiyo hiyo.

Ubinadamu ni kazi, The humanity is work.
 
Existance of reality in binary oppositions. Yani kuna dunia inayoonekana na dunia isiyoonekana
 
Sasa unaandika hapa ukiwa tayari Usha vuka hapo.
Unaonaje ungeandika wakati ukiwa umeketi chini ya mti mkubwa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…