Nimeamini ukitaka Marekani ikuheshimu, tengeneza silaha za nyuklia (silaha za maangamizi)

Nimeamini ukitaka Marekani ikuheshimu, tengeneza silaha za nyuklia (silaha za maangamizi)

Yohana469

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2021
Posts
302
Reaction score
450
Hakika nimeamini silaha za maangamizi (nyuklia)ni silaha zinazoogopwa dunia nzima matokeo yake endapo mataifa makubwa yakitumia nadhani ndio mwisho wa sayari hii ya dunia ,kwa kitisho alichokitoa urusi kwa silaha za nyuklia na mataifa ya magharibi ku-surrender ni hakika silaha za kuogofya,na ndio mana mataifa kama Iran na Korea yanang'ang'ania kutengeneza ni hakika utaheshimika kwa kila taifa.
 
Ndio maana haifai silaha kama hizi kumilikiwa kwa namna yeyote ile sababu zina hatarisha usalama wa dunia imagine silaha kama hizi zimilikiwe na watu wenye itakadi flani ambao wanaamini ukimwangamiza mtu flani wa
imani flani unapata thawabu itakuaje?
 
Sio anaogopa, maslahi ya dunia na vizazi vyake ndicho kitu anachozingatia.. kwa akili yako kabisa unahisi US hamwezi RUSSIA? Unadhani US nae akitoa nuclear zake utaandika hapa hata hii mada?
 
mimi si shabikii yeyete yule awe anamiliki weapon of mass destruction awe US au mwingine kivyovyote vile kwa vile sababu zake hazina future kwa kwa sayari yetu , just imagine juzi rushia katishia kwamba kikosi cha nyuklia kiwe tayari mda wowote kutumika zina maana gani kama conventional war ameona itamshinda akubali haya ni mambo ya kisiasa yatapita watakuja wengine lakini dunia na vizazi viendelee kuwepo
 
Ngoja na sisi tutafute wawekezaji waje kututengenezea...
 
Nchi yoyote duniani yenye maslahi makubwa ya kuyalinda, lazima ipate hofu kuhusu silaha za maangamizi hasa zile zinazotokana na mataifa inayohasimiana nayo.

Ndio maana nchi zote kubwa duniani zinazotambulika kama nuclear weapon states na mkataba wa NPT, hazikubaliani kabisa na hatua za mataifa mengine [madogo] kumiliki silaha hizo. Lolote la hatari linaweza kutokea muda wowote na kuathiri maslahi yao!
 
Back
Top Bottom