Nimeamua kuachana na aina zote za kamari

CARDLESS

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
7,840
Reaction score
15,918
Wakuu za asubuhi..

Nikiwa na uchovu wa kulala na mawazo makuu hasa ya kupoteza kiasi kikubwa cha fedha zangu na hata muda kupitia hii michezo ya kamari.. Nimeona niweke wazi kuwa hii michezo sio mizuri na inapelekea madeni yasiyo na kichwa wala miguu, ugomvi, kutoaminiwa na hata kushawishi wizi au unyang'anyi..

Nasema haya baada ya kuwa muhanga mkubwa kabisa wa hizi kamari yaana.. betting za soka, madudu ya wachina yale nk.. Jana tu nimepigwa pesa ndefu kiasi kwamba hata job sioni mzuka kukaa yaan kichwa kiko vuluvululu....

NAOMBA MUNGU ANISIMAMIE KATIKA HILI NA ANIPE NGUVU ZAIDI YA HAPA NILIPOFIA JUU YA KUACHANA KABISA NA KAMARI..
Ushauri wangu kwa vijana wenzangu kamari si mchezo mzuri tuachane nao kabisa...

NIMEAMUA KUACHANA NA KILA AINA YA KAMARI
 
hahahah subiri baada ya wiki ikifika jumamosi mechi ziendelee utarudi mwenyewe.....kamari ni addiction mbaya sana
 
fanya hivi ili uweze kuacha .....usitimie simu smartphone,,,,usitumie computer wala laptop hivi vitu vitakushawishi ukitoka kazini nenda kanisani au bar mpaka muda wa kulala
Sasa akienda bar hapo unampoteza cha msingi aangalie mwenyew kitu gani anaweza fanya kuwa busy pale anapokuwa free naamin akuzaliwa kucheza kamali amezaliwa amekuw si kwa sababu ya kamali..
Amefika mahali alipo kwa sababu mbali mbali so ukiamua kitu unaweza cha msingi kaa mbali na marafiki zako wacheza kamali au wape msimamo wako pia wasiongelee kabisa mada za Kamal mkiwa nao...
Kila lakher mkuu mimi huyu pepo alijaribu sana kuniingia lkn nilimshinda na kujiamini kuwa mimi ni mwanaume...pambana
 
Pole sana kwanza kamari ni haramu ukicheza kamari unamkosea mungu na nimchezo wa shetani
 
Pole mkuu hata mimi natafuta dawa, jana kanichania liverpool nilimpa double chance, iliniuma sana
 
Ukiona umeliwa wewe, ujue mwingine kala. Hii michezo haitakiwi uweke kiasi kikubwa cha pesa hadi kikuathiri. Pia usiwe na tamaa kuweka pesa yako kwenye zile outcomes zenye odds nyingi. Mara nyingi matokeo sahihi huwa kwenye zile odds za chini ya 1.15. Sasa wewe ukiona zile zenye 3, 5, 10 nk hizo sio za kuweka pesa maana kushinda ni ngumu sana.
 
Mkuu mara ya mwisho kutumia football betting ni mwaka jana tena kwenye ligi za msimu uliopita.. nilikuwa natumia mkeka bet, m-bet, premier na meridian.. baadae nikajiingiza kwenye kamari za mchina maarufu kama BONANZA/DUBU/HAMORAPA/KIDOLE JUU N.K.. hapa ndipo nilipoathirika zaidi.. Najiona mjinga sana maana degree yangu haijanisaidia kutatua tatizo hili sugu.. huwa napoteza muda sana kwanye haya madudu.. Mtu kushinda haina maana kwamba nami sijawahi shinda nimewahi sema unajikuta mambo mengi hufanyi hata kumtembelea let say mzazi ni ngumu..
 
Ukiweza kujua namna bora ya kuishinda tamaa hapo utakua umeshinda kiukweli ..
 
Daah pole sana,baada ya kupinga pesa za maana ktk makampuni ya kibongo, mwenzako sasa hivi nime upgrade nimeachana na makampuni ya kibongo nimehamia BWIN BET,BETFAIR NA BET365 na bet kwa kutumia usd kupitia master card,jana basketball nimeweka stake usd15 nimepiga usd 110.
 
Mkuu nipe tips za basketball
 
Na FOREX pia umeachaa...?
 

Leta screen shot ya mkeka huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…