Nimeamua Kufanya Uamuzi Huu Ili Nijisomeshe...Msaada Tafadhali!!

sikutarajia kama nitacheka kwa alivyojieleza mdau ila imenibid nicheke. Umemuuliza ukweli kabisa.

Me pia nimecheka ila nimeogopa kufumbua mdomo hapa jukwaani. Maana waswahili wanadai ukikuta wenzako wanalia na wewe lia nao.

Angefikiria njia nyingine. Unaweza ukauza hiyo figo halafu hata kabla hukumaliza masomo yako hiyo ilyobaki ikashindwa kufanya kazi. Hapo kutakua na faida gani!!??!

Mwili sio sawa na gari kijana. Spea za mwili ni adhimu sio adimu.

Unaweza kumuona mwenyekiti wako wa mtaa anaweza kukuunganisha kwa wafadhili.
 
Acha ndoto za kuuza viungo, tafuta vibarua vya kufanya kama mwanaume bila kubagua kazi ili mladi ni halali, kwani una malengo ila njia unayotaka kutumia sio.
 
heshima kwenu wanandugu...

Nayapenda sana maisha yangu na ninapenda sana nifanikiwe maishani hivyo sina budi kufanya hivi ili kusonga mbele. mimi ni mwanachuo katika chuo mojawapo hapa tz na kwasasa nina hali ngumu sana ya kifedha licha ya kujaribu njia tofauti ili kujikwamua na kusonga mbele.
Ninataka kuuza baadhi ya VIUNGO vya mwili wangu ili nipate walau ada ya kuendelea na masomo yangu niwe na maisha mazuri niweze kuwasaidia wadogo zangu na familia kwa ujumla.

Afya yangu kwa ujumla ni nzuri (99% uhakika) na ninataka niuze;
~FIGO ~KONGOSHO ~MBEGU ZA KIUME au DAMU ikiwezekana. hapa nachoomba kutoka kwenu ni kama kuna mtu yeyote anaejua ni hospitali gani au taasisi gani inanunua bidhaa hizo?. i am very serious and i will apreciate you contribution

Pole Kamanda. Hata hivyo, mambo haya mawili zingatia yatakusaidia. Mosi, usidhani kutopata elimu ya chuo kikuu ni tiketi ya kutofanikiwa kimaisha au hata kinyume chake. Pili, usidhani kuna kanuni katika elimu kwamba lazima uanze masomo ya chuo kikuu baada tu ya kumaliza elimu ya sekondari, maana lengwa hapa ni kwamba waweza pia ukafanya shughuli Zako na baadaye ukasoma na utakuwa na uelewa mpana wa uhalisia wa maisha. Sir Ken Robinson, mtafute kwenye u tube na google. Ni mdau nambari moja duniani katika kupinga fikra mfu za elimu na uelimishaji. Hapo nimekumegea tu mabaki katika mwiko ama upauo/pakulio. Pata picha ningekuwa nimekupakulia hata nusu kisosi. Najuta kuchelewa kujifunza kutoka kwakwe ila tazama, hakuna kuchelewa katika kujifunza.
 
Kusoma sana nikuogopa maisha, unaweza kutoa viungo vyako kwa ajili ya elimu lkn hata mwaka wa masomo usimalize ukapata tatizo la kifya na viungo ulivyotoa vinahitajika tena, unafkiri utakua na pesa ya kuvirudisha tena?? na nani atakua tayari kukuuzia??

Afya njema ni utajiri kuliko kitu kingine ndugu..
 
Nashindwa hata cha kukusaidia ila hizo fikra zako ni za kinyama don do it please. Kuna njia nyingi za kufanikiwa ila hiyo uliyochagua ni mbaya sana.
 
pole sana ndugu yangu lakini sikubaliani na wazo la kuuza baadhi ya viungo. kama ulivosema umejaribu kutafuta pesa but imekuwa ngumu, nakushauri u-keep trying hard kwani siku zote sio rahisi. waweza ahirisha hata mwaka ili upate muda wa kutosha kutafuta pesa
 
Kusoma sana nikuogopa maisha, unaweza kutoa viungo vyako kwa ajili ya elimu lkn hata mwaka wa masomo usimalize ukapata tatizo la kifya na viungo ulivyotoa vinahitajika tena, unafkiri utakua na pesa ya kuvirudisha tena?? na nani atakua tayari kukuuzia??

Afya njema ni utajiri kuliko kitu kingine ndugu..

Kuna mlevi aliniambia kuwa wanaokimbilia masomo ya uzamili baada tu ya shahada za kwanza ni waoga wa changamoto za maisha. wanataka kujificha chini ya mwamvuli wa elimu.
 
Your right mkuu!
 
heshima kwenu wanandugu...

Nayapenda sana maisha yangu na ninapenda sana nifanikiwe maishani hivyo sina budi kufanya hivi ili kusonga mbele. mimi ni mwanachuo katika chuo mojawapo hapa tz na kwasasa nina hali ngumu sana ya kifedha licha ya kujaribu njia tofauti ili kujikwamua na kusonga mbele.
Ninataka kuuza baadhi ya VIUNGO vya mwili wangu ili nipate walau ada ya kuendelea na masomo yangu niwe na maisha mazuri niweze kuwasaidia wadogo zangu na familia kwa ujumla.

Afya yangu kwa ujumla ni nzuri (99% uhakika) na ninataka niuze;
~FIGO ~KONGOSHO ~MBEGU ZA KIUME au DAMU ikiwezekana. hapa nachoomba kutoka kwenu ni kama kuna mtu yeyote anaejua ni hospitali gani au taasisi gani inanunua bidhaa hizo?. i am very serious and i will apreciate you contribution

sasa mdau angalia usije uza na hle ya kutole' haja ile aiseeee.........
hautakiwi uwe na expectatn kubwa na elimu ya bonga.....mbulula we we..........
postpone kafanye deal ndogo ndogo uanaume kazi..........usije kuongeza idadi ya kina scofield,madam elton jonh bure
 
pole sana ndugu yangu lakini sikubaliani na wazo la kuuza baadhi ya viungo. kama ulivosema umejaribu kutafuta pesa but imekuwa ngumu, nakushauri u-keep trying hard kwani siku zote sio rahisi. waweza ahirisha hata mwaka ili upate muda wa kutosha kutafuta pesa

uamuz wa busara na kibinadamu
 
heshima kwenu wanandugu...

Nayapenda sana maisha yangu na ninapenda sana nifanikiwe maishani hivyo sina budi kufanya hivi ili kusonga mbele. mimi ni mwanachuo katika chuo mojawapo hapa tz na kwasasa nina hali ngumu sana ya kifedha licha ya kujaribu njia tofauti ili kujikwamua na kusonga mbele.
Ninataka kuuza baadhi ya VIUNGO vya mwili wangu ili nipate walau ada ya kuendelea na masomo yangu niwe na maisha mazuri niweze kuwasaidia wadogo zangu na familia kwa ujumla.

Afya yangu kwa ujumla ni nzuri (99% uhakika) na ninataka niuze;
~FIGO ~KONGOSHO ~MBEGU ZA KIUME au DAMU ikiwezekana. hapa nachoomba kutoka kwenu ni kama kuna mtu yeyote anaejua ni hospitali gani au taasisi gani inanunua bidhaa hizo?. i am very serious and i will apreciate you contribution

ni kitu kizuri kutaka kufanikiwa maishani na nakupongeza sana kwa kuwa na njaa ya kuelimika na kuwa msomi ila nasikitika kukwambia kwamba njia unayotaka kuichukua ili upate fedha za kujikimu si nzuri
 
Tatizo la tanzania inahitaji kuwa na wasomi au wataalamu wengi, ila tatizo linakuja katika hizo gharama za kuipata hiyo elimu yenyewe, nadhani pia na serikali pia imeshindwa kujua jinsi gani ya kuwasaidia raia wake ili kila mmoja aweze pata elimu kwa urahisi, wapo wengi sana wanaoshindwa kujiunga na mashule au vyuo kwa kushindwa mudu gharama, pole sana ndugu, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA RAIA WAKE.
 
wakati mwengine utakuja na uzi unataka uuze o655 huu umasikini huu!!!!!!!!!!
 
pole Sana mkuu lkn nakushauri utafute njia nyingine sio hiyo.
 
Back
Top Bottom