Nimeamua kujifunza Python programming

Nimeamua kujifunza Python programming

Za jioni wakuu,
Napenda kujifunza vitu vipya na kuanzia jumatatu ya wiki hii nimeanza kujifunza programming language ya python. IT sio fani yangu niliyosomea ila nataka nianze kutengeneza applications kama hobby na kujifunza kitu kipya.

Background ya IT : nilishawahi kujifunza HTML kama miaka 4 iliyopita kwa kutumia online tutorials nadhani nimeshasahu mengi.

Resources : Nimeamua kutumia Codecademy kama chanzo changu cha taarifa kwa sababu ni free na kozi zao ziko simple na well structured na kila hatua kuna mazoezi ya kufanya yanayosaidia kuelewa zaidi.

Nilipofikia: mpaka sasa nimemaliza asilimia 28 ya kozi nzima(nimetumia siku tatu - angalau saa moja kila siku) nimejifunza Syntax, Strings and Console, Conditionals and Control Flow sasa najiandaa kuanza Functions.

Malengo: Nategemea kumaliza kozi yangu ndani ya wiki mbili au tatu na kutengeneza application itakayosaidia kuorganize taarifa za wagonjwa wanapofika hospitali nia iwe kupunguza muda anaotumia mgonjwa hospitalini au application yoyote itakayofanana na hiyo.

Changamoto : Kutokana na niiyojifunza, nimetengeneza application inayoitwa JF Saccos ambayo mteja anaandika jina na umri. Nimeweka condition kuwa kwenye kuandika jina liandikwe bila kuweka namba yoyote na ikiwekwa namba basi apewe taarifa kuwa 'amekosea na aanze upya' jambo ambalo nimefanikiwa ila kwenye umri nimejaribu kuweka condition iwe zaidi ya miaka 18 na akikidhi vigezo akaribishwe na sentesi "Hongera ndugu %s, mwenye miaka %s,umefanikiwa kufungua akaunti" na akiwa chini ya miaka 18 apewe taarifa kuwa "Hairuhusiwi Wenye Umri Chini Ya Miaka 18". Ila tatizo hata nikiweka chini ya miaka 18 bado inakubali. Sijaelewa nini shida kwenye code. Walimu mnaweza kunisaidia. Mnaweza kuicheki hapa na nimeweka screenshot chini.

View attachment 546863 View attachment 546864

CODE:
print "KARIBU JF SACCOS"
from datetime import datetime
date = datetime.now()
print "Leo ni tarehe %s" %date

print "Jina lako"
name=raw_input()

print "Andika umri wako"
age = input()

if age > 18:
print "Hongera ndugu %s, mwenye miaka %s,umefanikiwa kufungua akaunti" %(name,age)
else:
print "Hairuhusiwi Wenye Umri Chini Ya Miaka 18"
 
Embu jaribu izo code.....
 
Python ina learning curve ndogo sana kulinganisha na programming language nyingine kama java na c++ kama hujawahi kujifunza hizi. Lakini kwa namna Python ilivyokuwa simplified kwa navyoona mimi siyo language bora kujifunzia programming kwa ule usimpo wake kwa kuwa haifuati sana principle za programming language zile maarufu kama c++ na java.

kwa mfano katika Python huna haja ya kuspecify variable type, unaipa jina tu basi. lakini hizi nyingine huwezi. control loops zake na vitu vingine ni vyakivyake. Ukitoka kusoma hii afu huje kwa mama zake inakuwa mtihani kidogo.

All in All all the best.
 
Thanks kiongozi kwa mchango wako, ila sidhani kama nina mpango wa kusoma hizo languages nyingine ndio maana nilitafuta language ambayo sio ngumu kujifunza ila yenye uwezo wa kufanya mengi.

Hata hivyo resources nyingi online wanashauri kuanza na Python kama unataka kushuka kwenye huo mtiririko wa akina C++ etc wakati nachagua nijifunze lugha ipi nilifanya uchunguzi kabla.

"
Python was designed to be easy to understand and fun to use (its name came from Monty Python so a lot of its beginner tutorials reference it). Fun is a great motivator, and since you'll be able to build prototypes and tools quickly with Python, many find coding in Python a satisfying experience. Thus, Python has gained popularity for being a beginner-friendly language, and it has replaced Java as the most popular introductory language at Top U.S. Universities. "

Asante sana kwa mchango wako
 
Updates :

Nimesoma topic ya function ila bado kuna subtopic bado sijaimaliza...nilitaka nije na code inayojumuisha function ila nitasubiri nimalize kwanza function.

Nimefanya zoezi lingine kwa kuandika codes ya Project inayoitwa "JF Health Centre" inayomtaka user kuandika jina na umri na kumkaribisha kwenye huduma kwa kumtaja jina na umri na pia kumtaka kuchagua aina ya daktari aidha daktari bingwa au daktari wa kawaida(GP) na kumpatia gharama ya consultation kulingana na uchaguzi wa aina ya daktari.
shot 1.png

Pia nimegundua kutokuwa na elimu ya loops inanifanya nisiweze kuiamuru code isimame pale user anapokosea aina ya entry. So nitasubiri nimalize loops nijue nitasolve vipi tatizo hilo though mdau @Arduino Sentinel alinidokezea.

Stefano Mtangoo
 
badala ya screenshot ungeweka simba zako kama text. Au tumia Pastebin kama hapa panakutatiza. Muda nilio nao ni mchache kuanza kuandika upya kili kilicho ktk picha!
 
Nakufuatilia kiongozi naona nami najifunza Ila download rodeo ide pia uwe unapiga hapo code zako pia hii ni Python ya nyuma I think siyo 3.6 sababu kwenye 3 hiyo raw input haipo na lazima kuwe na brackest kwenye print. All in all unaenda vizuri
 
Kwa kujifunza IDE haifai. Atumie tu Editor (Geany, Sublime, TextMate, et al) na Terminal, zinamtosha kwa sasa!

Atakuwa anatumi Py2.x na kama ameshaanza hivi ni bora akamaliza halafu aende kwenye changelog kujua nini kimebadilika. BTW Software nyingi sana zimegoma kuhamia 3.x na zingine zipo kwenye movement (zikiwemo maktaba muhimu kama wxPython). So hajapotea njia 😉
 
Nakufuatilia kiongozi naona nami najifunza Ila download rodeo ide pia uwe unapiga hapo code zako pia hii ni Python ya nyuma I think siyo 3.6 sababu kwenye 3 hiyo raw input haipo na lazima kuwe na brackest kwenye print. All in all unaenda vizuri

Sijasahau mkuu....leo nitaicheki. Wewe ni IT expert au unajifunza kama mimi ? Kama unajifunza kama mimi umeanza na lugha gani na umefikia wapi ?
 
Back
Top Bottom