Nimeamua kujifunza Python programming

Noted mkuu.... nadhani Codecademy wanatumia version ya zamani baada ya muda wata-update nadhani. Nikimalliza kozi yote ndio nitaangalia version mpya zina nini cha ziada.
 
Mkuu nilijisahau kidogo inapatikana HAPA
Kuna trick nyingi ila naona rahisi ni kutumia While loop

badala ya
Code:
name=raw_input('Andika Jina Lako:')
if name.isalpha():
  print name
else:
  print "Umekosea Rudia Tena"

Andika
Code:
while True:
    name=raw_input('Andika Jina Lako:')
    if name.isalpha():
      print name
      break
    else:
      print "Umekosea Rudia Tena"
 
Umenikumbusha mbali sana! Wabongo sio watu wazuri....Miaka fulani tulikuwa tunafanya brainstorming maeneo flan huku tukipata "The cold ones" jinsi ya kupunguza cue kwenye mabenki yetu kwa kuweka utaratibu maalumu numbers kwa wateja...Haikupita Mwezi mmoja watu waka-introduce new app CRDB....
 

Polee walikiwahi.... watu pesa mbelee
 
Mbona unatapika ma idea, nikikuibia utanishtaki



Small minded people will never understand
 
Mbona unatapika ma idea, nikikuibia utanishtaki



Small minded people will never understand

hehehehe hiyo idea ruhusa kwa watu kuiba maana ninazo nyingi...hiyo ni idea ya kujifunzia tu.. Thanks for your concern though😀
 
Ukimaliza Basics za Python unaweza anza kufanya vitu interesting kwa wxPython (GUI), au DJango (Web)
Kwa sasa endelea kujifunza basics mpaka umalize!
Keep pressing on...!
 
Hongera sana! Python ni programming language nzuri. kwa kujifunza, code academy ni sehemu nzuri kuanzia, lakini nakushauri tafuta kitabu "Learn Python the Hard Way", mwandishi ni software engineer nguli Zed Shaw. Hutojutia kukisoma, kina mazoezi 54 hivi, ukikimaliza kwa kufanya kila zoezi ipasavyo, utakuwa na msingi mzuri wa Python. Kila la kheri!
 
Ushauri: Endelea kujifunza kwa kutumia Python 2.7.x, Python 3, haijakamilika kwasababu applications nyingi zilizoandikwa kwa Python 2.7.x hazijaweza kufanya kazi kwenye Python 3, Python 2.7.x nitaendelea kuwepo, ondoa wasiwasi kuhusu hilo na asikushawishi mtu kukimbilia Python 3!
 
Ukimaliza Basics za Python unaweza anza kufanya vitu interesting kwa wxPython (GUI), au DJango (Web)
Kwa sasa endelea kujifunza basics mpaka umalize!
Keep pressing on...!
Namshauri akimaliza basics, asome alot of python code. Wakati huo huo aanze kudevelop web applications kwa kutumia microframeworks kwa mfano flask, webpy, bottle, wheezyweb etc, zote hizo ni za Python. Write and Read alot of code!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…