Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Ndugu wanajamii,
nimekutana na jamaa mmoja mwenyeji wa huko Bukoba- katika kupiga story kaeleza jinsi anavyolima huko BUKOBA na ambavyo hapati mazao ya kutosha kutokana na kilimo cha maharage na mahindi.. alibainisha kwamba katika ekari kumi alizonazo anavuma magunia 3 mpaka 4 ya maharage. na kama ni mahindi basi anapata magunia saba..

katika soma soma zangu hapa JF niliwahi sikia kwamba kwenye ekari moja unaweza kupata hata gunia 5-10 za maharage na zaidi ya 10 za mahindi. sasa hapo utaona kwamba mazao anayopata kwenye ekari 10 mtu mwingine anayapata katika ekari moja.

kwa kuwa mimi sina utaalamu sana wa kilimo cha maharage na mahindi, naomba kuuliza na kupatiwa majibu katika yafuatayo:

  1. Je Mbegu gani nzuri za mahindi na Maharage .. Na je zinapatikana wapi -- naomba kupata jibu specific ya aina pamoja na zinapopatikana
  2. Ninajua Maharage yapo ya aina nyingi... Je aina ipi inatoa mazao mengi? upatikanaji wake upoje?
  3. Je unapolima maharage na mahindi , Je unatakiwa upande umbali gani kati ya shimo moja na jingine (i.e je kuna kipimo maalum?)
  4. Je ukubwa wa shimo unatakiwa uweje
  5. Je ni lazima kuweka mbolea katika kila shimo kabla kupanda-- kama ni ndiyo je uweke samadi kiasi gani.
  6. Je ni wakati gani wa kupanda yaani Je ni kabla ya mvua kuanza, katikati ya msimu wa mvua au mwisho wa msimu wa mvua? nauliza hivyo nikiwa na mawazo ya kuhakikisha mvua haiharibu maua ya harage/hindi yatakayotoa mazao.
inawezekana mtu asiwe na majibu ya maswali yote ila nitashukuru hata ukijibu angalau moja unalolijua.

thanks
 
Naamini hili litakuwa darasa kwa wengi wetu; wenye data tafadhali.
 
jamani wanandugu nakumbushia tena, mwenye some information katika issues za hapo juu naomba msaada tutani!!
 
Hebu jaribu....

*
Tanzania Seed Company Ltd. / Tanseed International Ltd.
Tanzania Seed Company Ltd.
Tanseed International Ltd.
PO Box 140
Njombe
Tanzania
E-mail:*tanseed@yahoo.com *
Tel: +255 26 278 2354
Fax: +*

Sina details zao zaidi lakini nimewapata kwenye internet website.
 

Nina dogo langu moja pale SKU yaani shirika la kilimo Uyole Mbeya, nitawasiliana nalo litupe midata yote kuhusu maharage. data zangu ziko chini sana, si vizuri kushusha upupu wakati ukweli upo.
 
Safi sana Kiongozi ila majina sometime yanazingua sababu umejiita Elnino basi hata mie Washawasha naogopa ikija hiyo Elnino si hata mie itanikomba?(im kidding right)Mkuu mie nilikuwa nataka kujua hizo mbegu za muda mfupi zinapatikana wapi na kwa gharama zipi na muda gani zinakuwa kwa kupanda mpaka kuvuna?

Mchanganuo pliz
 
amoeba ni vijiji gani hivyo mkuu?
 
Great Thought great Action,wasiwasi wangu ni hiyo bei tu ya gunia la mahindi mbona mimi najua bei ni kati ya 20,000 to 30,000? Hiyo ya 60,000 kaka unaitolea wapi tena?
 
Nina dogo langu moja pale SKU yaani shirika la kilimo Uyole Mbeya, nitawasiliana nalo litupe midata yote kuhusu maharage. data zangu ziko chini sana, si vizuri kushusha upupu wakati ukweli upo.

Malila, dogo wa Uyole ulimpata?
 
Nina dogo langu moja pale SKU yaani shirika la kilimo Uyole Mbeya, nitawasiliana nalo litupe midata yote kuhusu maharage. data zangu ziko chini sana, si vizuri kushusha upupu wakati ukweli upo.

Msimu wa kupanda mahindi umewadia; vipi kuna anayefahamu mbegu bora za mahindi zinapatikana wapi.
 
Wadau, naamini ili upate mazao bora na mengi uchaguzi wa mbegu bora ni kigezo kimojawapo. Kuna anayefahamu mbegu bora za mahindi; anifahamishe?
 
Wadau, naamini ili upate mazao bora na mengi uchaguzi wa mbegu bora ni kigezo kimojawapo. Kuna anayefahamu mbegu bora za mahindi; anifahamishe?

Mbegu za mahindi hutofautiana kutokana na altitude ya eneo husika, na ndio maana unaweza ona mbegu hiyo inafaa Njombe na isifae Dodoma, hebu twanga simu hii 0765504765, hapa utampata jamaa wa SKU, naamini atakupa msaada kidogo juu ya mbegu za kilimo au atakupa pa kuanzia mkuu.
 
Jaribu kuangalia website ya wizara ya kilimo wanatoaga publications za mazao mbalimbali
 
Hongera. Nadhani kila mtu inabidi atafute kitu mbadala cha kufanya na ulichofanya wewe ni kitu kizuri.
Ila hujasema unalima zao gani. Mahindi au maharagwe? Au maua (labda ya mbegu, ndio unazalisha kwa magunia)?

Vipi uhakika wa soko?
 
Mimi niko chuo. Sina kitu mfukoni, lakini naanza taratibu nikiamini nitafika huko siku moja.

Najifunza mambo mengi sana, natafakari sana, naongea na watu na marafiki wenye akili wanaojielewa ninapozidiwa kimawazo, napanga mipango midogo midogo na watu wangu wa karibu, nitajifunza mengi madhali ningali hai, sitapoteza muda wangu, nitafikiria na kupanga hata kama sina nikiamini nitapata siku moja kwa juhudi ninazoweka.

asante Elnino.
 

Karibu sana ktk Ulimwengu wa wakulima.
 
Elnino, hapa ndiyo umenikuna haswa! Haya ndiyo mapinduzi yanayohitajika kwa Watanzania! Tukamate maeneo yote ya kilimo tulime kwa wingi kwa sababu tunakoenda kwa sasa chakula kitakuwa kama ilivyo kwa mafuta kwa sasa. Ntafuata nyayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…