Hongera sana,
Mimi nataka nitoe ushuhuda juu ya utajiri uliopo kwenye Kilimo. Nilkinunua hekari nne Bagamoyo nikalima kama pilot study. Hekari tano unaweza panda miche ya minanasi kati 80,000 na 90,000. Kwa mwaka huu wa kwanza nimevuna mananasi zaidi ya 50,000 kwa bei kati ya Tshs 700 na Tshs 1000 kwa kila nanasi. Kwa kugundua utajiri unaopatikana katika kilimo, nimenunua hekari 70 hukohuko bagamoyo na hadi sasa nimeshapanda miche 400,000 na lengo kwa mwaka huu ni kupanda miche 550,000 ili baada ya miezi 18 nianze kuuza. Kati ya mananai 550,000 natarajia kuuza mananasi 400,000 kwakuwa huwezu kuvuna kama ulivopanda. Kwa wastani wa bei ya 800 natarajia nipate si chini ya Thss. 300,000,000. Ni kama ndoto lakini nimefanya pilot study ya kwenye shamba langu dogo nimeona inalipa, kwakuwa kwasasa wanunuzi wanagombania mananasi na kutokana na udogo wa mashamba ya wakulima, gari moja haiwezi kujaa kutoka kwenye shamba moja.
Note: Ngugu zangu, mimi naishi na kufanyakazi nje ya nchi lakini nimeona umuhimu wa kuwekeza kwenye kilimo, kwahiyo wale mliokaribu hapo nyumbani fanyeni hima kweli kilimo kwakuwa biashara za ubabaishaji umekwisha. Nilipofika shambani kwangu na kuona watu zaidi ya 50 wanafanyakazi nikajisikia faraja sana kutoa ajira kwa Watanzania wenzangu, shime tuelekee kwenye kilimo.
Naomba kamahakuna special group inayojihusisha na kushauriana na masuala ya kilimo naomba tuianzishe ili tuweze kujadiliana mambo muhimu ya kilimo na tufahamishane tujaribu kuangalia jinsi gani tunaweza kusaidiana. Masoko yapo mengi sana nje ya nchi, changamoto ni kwamba order zinazotakiwa ni kubwa sana, inabidi kujipanga ili kuzitimiza. Nomba tuwasiliane.