Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
NIMEAMUA KUMPELEKA SHEMEJI YANGU MAHAKAMANI
Anaandika, Robert Heriel.
Haki lazima ikatendeke!
Mbwembwe zangu zote lakini naishi Kwa Shemeji. Kuna wakati nakaa nawaza Kama nisingekuwa na Dada ingekuwaje, maana ndugu zangu wote wa kiume Hali zetu dhoofu ilhali Kama Yukreini. maisha yametupiga makombora, tumepigika tukachakaa!
Ukinikuta nyumbani utafikiri ndio Mimi ninayeandika huku mitandaoni Kwa kujiamini mwenye misimamo na kujitia Great Thinker, Thubutu! Ooh! Huku nimepoa Kama Uji wa Mgonjwa wa malaria Kali. Hasa Shemeji yangu akirudi kutoka kazini,
Taikon taabani maji kidevuni, Sister angu yeye alishanichoka miaka nenda Rudi licha ya kuniwekea Sanctions za kutosha ili niondoke lakini niliapa nitakomaa na vikwazo vyao mpaka kieleweke. " Mimi nirudi kijijini Mimi" mpaka najicheka kwenye kioo nijitazamapo.
"Ooh! Taikon kanenepea Kwa Shemeji"
Mara "Ooh! Unachezea Rimoti ya TV Kwa Mume WA Dadaako" Hayo maneno hata Kama yanakera lakini mvumilivu hula mbivu hata kama za uvivu. Endeleeni tuu na kelele zenu za chura, Mimi tembo hazinitishi.
Ninakaba penati Kama nipo ligi ya mpira za arabuni, Chenchi nikutumwa sirudishi nipo Radhi nikane kwa ubishi; nilikupa! nilikupa!
Nitawezaje kujiunga bando nifurahie maisha ya Mtandaoni. Nina washikaji kibao Mtandaoni, wapo wanaoniheshimu na kuniona mtu wa maana, ndio niwashikaji zangu hata kama hatujawahi kuonana. Sitishwi na maneno ya wanaonikera Mtandaoni kwani maneno Yao wala hayafui dafu mbele ya maneno ya Shemeji yangu huyu na Sister angu.
Shemeji yangu anamaneno ya kejeli na Dharau katu sitosahau.
Lakini sikumtuma aniite nyumbani kwake, nilikuwa zangu kijijini Makanya huko na maisha yangu yasiyo na mbele wala nyuma baada ya kumaliza University lakini niliridhishwa nayo. Yeye ndio aliyeniita Mjini ati atanitafutia kazi.
Nafika mjini siku zaidi ya tisini hakuna kwenda kazini labda kunipa vijikazi vya pale nyumbani. Hiyo ni baada ya Housegirl kufukuzwa pale nyumbani kisa nilileta uroho wa kutaka Kula kimasikhara Kama Rikiboy. Ugomvi ukazuka na uhasama ukaibuka. Japo sio vizuri kusema mambo binafsi hata Mimi Nafsi inanisuta lakini maji yameshavuka ukingo wa shingo na sasa yanaelekea puani, Acha niseme kabla ya pumzi yangu kuzima.
Kama ninakula, ninakunywa, ninaafya iweje nisichakate mchakato wa Katiba iliyopendekezwa. Lakini Shemeji yangu akazuia Katiba mpya na kumfukuza Housegirl. Analeta Siasa za UCCM na UCHADEMA kwenye maisha, looh!
Nilimshamsomea kila risala naye bila Sala akaniona Kula kulala, ati sina fikra wala maarifa, elimu yangu ati msalaba nilioubeba kwenda kunisulubisha. Mimi nikamuuliza kwani ulivyonitoa huko kijijini Kwetu Makanya hukujua hayo yote. Nikamuona anarapu rapu na kunitolea shit motherfanta.
Nikasema huyu hanijui, ndimi Taikon Master mwenye Mkanda mwekundu wa kuganda Kama ruba.
Juzi nimetimiza miaka mitano tangu nifike Kwa Shemeji, nimepata mchumba nikiwa hapohapo Kwa Shemeji yangu. Usishangae Kwa nini natafuta mchumba wakati naishi Kwa shemeji na sina kipato cha uhakika, umri unaruhusu kufanya hivyo. Ninamiaka 31 ningefanyaje, kuniona sina akili ni kuonyesha wewe ni mbumbumbu!
Mchumba wangu naye anaishi Kwa Shemeji yake. Wote twaishi Kwa mashemeji.
Kila nikutana na Mchumba wangu tunahadithiana changamoto zinazotusibu kwenye nyumba za mashemeji.
Zangu zinavumilika lakini zake sio kitoto, huyo Shemeji yake mshenzi sana, anataka Kumla Mchumba wangu. Hii kidogo inanipasua kichwa.
Jana Shemeji yangu ananijia na habari ambayo nilidhani ni taarifa ya habari ya uchumi aliyoisikiliza ITV. Akaniambia; Taikon hivi unajua kilo moja ya Unga ni Tsh 1,800 wakati kilo ya mchele ni Tsh 2,300/=,
Nikamjibu Mimi sikusomea uchumi.
Tumekwazana, ati anasema majibu yangu ni yadhihaka, anafikiria namna ya kunifukuza hapa nyumbani.
Mimi nimemuambia siondoki mpaka atimize ahadi yake ya kunitafutia kazi.
Nimemuambia Mchumba wangu ni mwanasheria, nitaenda Mahakamani kumfungulia Shauri Kwa kosa la kunidanganya na kunipotezea miaka mitano nyumbani kwake. Huku nikifanya kazi bila malipo yoyote.
Mchumba wangu kaniambia atanisapoti na tayari tumeanza kusoma makarabrasha ya uendeshaji wa kesi.
Ushahidi wa Meseji alizonitumia nikiwa kijijini Makanya kutaka nije mjini kuna kazi ninao, ushahidi wa kumfukuza Housegirl ninao, na Mimi kuchukua nafasi ya housegirl pasipo malipo yoyote.
Mwanasheria wangu(mchumba wangu) ameniambia hata akisema Kwa mwezi alikuwa anamlipa mfanyakazi Tsh 50,000/= Kwa mwezi.
Basi hizo pesa Kwa miaka mitano ni 3,000,000/= na usumbufu basi tutapata milioni Saba hivi.
Milioni Saba hiyo tumeiwekea bajeti ya matumizi Yafuatayo;
1. Milioni 1. Mahari
2. Milioni 1.5. Vitu vya ndani.
3. Milioni 1. Kodi ya Miezi sita Kwa chumba cha laki na nusu.
4. Milioni 3. Mtaji wa Biashara ya Dagaa.
5. Laki tano. Matumizi.
Tuombeane uzima Taikon ndio natoka hivyo.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Arusha.