Nimeamua kumuacha mke wangu……………..!

Nimeamua kumuacha mke wangu……………..!

Wakati naumwa nilipewa likizo ya naniliu ya miezi mitatu ili nipone, sasa likizo imeisha na yeye anataka kusafiri, hivi kweli katika mazingira kama hayo, unaweza kweli kufurahi...............! Kusema kweli nilikuwa nahitaji uangalizi wake wa karibu sana tena sana maana miezi mitatu sio mchezo.

miezi mitatu dah kwa kweli unahitaji uwepo wake sana sana sana,

Mama Ngina plizi hebu usisafiri kwanza kaa kwanza na Baba Ngina hata kwa wiki tatu ndo usafiri loh.....
 
yaani hii post nilikuwa naipitapita maana nilikuwa nashangaa ni mpuuzi anamuacha mke wake ila nilivyoifungua ilibidi nicheke. Vipi utampa bodyguard wakumsindikiza maana asije akawa anapitia kwa akina Bishanga
 
mie roho haijadunda sana mana nilivyoona heading nikaanza na paragraph ya mwisho kwenda juu. mama ngano safiri salama ila rudi kabla wa wiki uliyopewa afu usitoe taarifa ya ujio wako. fanya suprise mtambuzi atafurahi sana na hyo suprise
 
Unabeep fire wewe eeh? Maneno yako taamu sana ngoja moto ukuwakie! Safari njema mama ngina.
 
Eheee, umenikumbusha halafu Bishanga aliahidi kutembea na mke wa mtu mwaka huu, hayo yalikuw ani miongoni mwa yale aliyoyakusudia mwaka huu...............Ngoja nifanye utafiti, maana mama Ngina aliisoma ile posti akacheka sana.................LOL
hapa itabidi nimulike mwizi
Halafu kuna wale aliokuwa akicheza nao ule mchezo wa kibaba na mama, na Kidali Po, sio kwamba watakumbushana...........Aaaaaagh! Kumbeeee, Hii safari inanifanya machale yanicheze, Jamani yaani naibiwa hivi hivi, ngoja niongee na yule dada yangu wa Chabo kama anaweza kunipa likizo ya wiki moja tuambatane. Nimeshtuka
 
Unabeep fire wewe eeh? Maneno yako taamu sana ngoja moto ukuwakie! Safari njema mama ngina.
jamani si nimesema namuacha mke wangu asafiri kwenda kuwaona wazazi wake, kuna ubaya gani hapo?
 
mie roho haijadunda sana mana nilivyoona heading nikaanza na paragraph ya mwisho kwenda juu. mama ngano safiri salama ila rudi kabla wa wiki uliyopewa afu usitoe taarifa ya ujio wako. fanya suprise mtambuzi atafurahi sana na hyo suprise
Hana haja ya kuweka ulinzi shirikishi, mwanangu Ngina anatosha, wala hahitaji usaidizi wa Cantalisa na King'asti. Huyu Ngina ni balaa ni mkuda hafai.....................
 
La! mwanawane umenishitua sana heading yako kumwacha mama Ngina?,nilianza kujiuliza Ngina ataishije? mimi sina habari na wengine hata kama ingekula kwao lakini Ngina! loh! kumbe nimegundua socrates at work.
 
imeaandikwa mwanamume atawaacha wazazi wake naye ataambatana na mkewe watakuwa mwili mmoja.....
sasa hapa kuna vitu vya kuvikubali kwanza (hii kwa uelewa wangu) inamaana mwanamke yeye haachi wazazi wake hivyo lazima aende maandiko hayajamfunga lakini la pili ni kwamba sielewe vizuri mkiwaacha wazazi ukiambatana na mkeo inamaana unaenda kwao hivyo nenda naye ka vipi kwa sababu maandiko hayakutoa mnaaenda wapi
lakin katka hali ya kawaida ni vizuri akaenda likizo ni siku nyingi akirudi atakuwa na akili mpya na mawazo mapya kuliko ukin'gangania akae hapo (japo kwa shida na raha) vumilia m2 wangu

WAPI imeandikwa hivyo?
 
Eheee, umenikumbusha halafu Bishanga aliahidi kutembea na mke wa mtu mwaka huu, hayo yalikuw ani miongoni mwa yale aliyoyakusudia mwaka huu...............Ngoja nifanye utafiti, maana mama Ngina aliisoma ile posti akacheka sana.................LOL
hapa itabidi nimulike mwizi
Halafu kuna wale aliokuwa akicheza nao ule mchezo wa kibaba na mama, na Kidali Po, sio kwamba watakumbushana...........Aaaaaagh! Kumbeeee, Hii safari inanifanya machale yanicheze, Jamani yaani naibiwa hivi hivi, ngoja niongee na yule dada yangu wa Chabo kama anaweza kunipa likizo ya wiki moja tuambatane. Nimeshtuka

Mkuu ukiona anakazania kwenda jua kuna kitu, anaenda anakumbushia fasta halafu anarudi
 
Mbona kang'ang'ania hivyo kwenda kusalimia wazazi, au kwenda kukumbushia miaka ile ya ujana. Tafakari, Chukua hatua.
 
Khaaa..............yaani we Babu umesababisha mshale wa kumoyo ugande ghafla ndo nini kuanza na heading ya ukanjanja. Nilishaanza kulia nani atanipikia uji. Namtakia Mama Ngano safari njema.

Najitolea huo n'chale uliokuchoma nije niutoe bureee ! Staki hata senc 5 ! Nifanye kazi ya msalaba wa msimbazi.
 
Hana haja ya kuweka ulinzi shirikishi, mwanangu Ngina anatosha, wala hahitaji usaidizi wa Cantalisa na King'asti. Huyu Ngina ni balaa ni mkuda hafai.....................

Si ndiyo mitoto ya Jakaya ilivyo? Dawa yao ni kuwang'olea fuse ya nyama ! Unawapachikia ya dagaa, binzi, miezitatu!
 
Mtambuzi katika siku uliyoniudhi ni leo.......................................

Kichwa cha habari kama gazeti la Uwazi??? Umeanza lini kuandika "UDAKU"

Hovyo kabisa wewe yaani nimekuja mbio kujiandaa kutoa ushauri kumbe ndani ni hivi

Muone kwanza sura mbayaaa kaa nani hii...........................
 
Problem child part 2 inaanza! Takeaway daily!.
Heshima yako baba,
Dah hiyo heading imenistua nikampigia mama kabla sijasoma akawa hapokei na uzi ukawa umeshafunguka lol!
Sijui ingekuwaje kwa nilichokuwa nimepanga kumuuliza,
Poa tunamtakia mama safari njema,na mungu ampeleke salama na amrudishe salama.
 
Kichwa cha habari kama gazeti la udaku vile. . . Lolz

Nwy mtakie safari njema, awarudie na zawadi toka kijijini.

Duuh mie mwenyewe nilidhani babu kamuacha bibi, nilitaka kuhoji wajukuu 2tajifunza nini kutoka kwake...., Anwy 2namtakia safari njema na akumbuke Maboga wakat wa kurudi.
 
Mtambuzi katika siku uliyoniudhi ni leo.......................................

Kichwa cha habari kama gazeti la Uwazi??? Umeanza lini kuandika "UDAKU"

Hovyo kabisa wewe yaani nimekuja mbio kujiandaa kutoa ushauri kumbe ndani ni hivi

Muone kwanza sura mbayaaa kaa nani hii...........................

Dena Amsi, sublakheri kwanza.
Mimi nimesema nataka kumuacha mke wangu mama Ngina asafiri kwenda kuwaona wazazi wake, kuna ubaya gani hapo?
Samahani kama nimekuudhi kumruhusu mke wangu kipenzi kwenda kuwaona wazazi wake..................LOL
 
Back
Top Bottom