Kama vile tozo walizoweka hazitoshi, wameamua kuchukua tozo zingine kwa kupunguza ukubwa wa vifurushi vya intanet. Hivi huko serikalini wanafikiri kwa kutumia kiungo kipi cha mwili. Walivyo mazuzu nasikia wamepiga pin mitandao ya ngono!! Sijui wanamkomoa nani wakati ni wao wenyewe ndo wanakosa mapato. Na ufinyu wao wa kufikiri unaonekana dhahiri jinsi wanapodhani kila anayetumia intanet basi ni kwa mambo yasio na faida. Kama wangekuwa na akili wasingejali watu wananunua vifurushi vya intanet kwa matumizi yapi ili mradi wao wanaingiza pesa, na hatimae serikali kupata kodi kwa njia halali pasipo na manung'uniko.
Kwa miaka nenda rudi nimekuwa nikitumia kifurushi cha TTCL cha 10GB kwa wiki, kwa Sh 10,000. Leo nakuta eti wanatoa 7.5GB. Yaani kwa akili yao wanataka niendelee kuwapa Sh 10K kwa 7.5GB. Kujibu mapigo, nimeamua kuanzia leo najiwekea internet cap ya 500MB kwa siku. Yaani nanunua kifurushi cha 3.5GB kwa wiki, kwa Sh. 5000. Nahakikisha kwa siku natumia 500MB tu, na kwahiyo nitakuwa nimewapora mapato kwa 50%. Kwavile ku-set data usage kwa njia ya modem haiwezekani, kuanzia leo natumia hotspot ya simu, na nimesha-set data limit.
Nime-turn ON hadi Smart Data Saver! Ofcourse, hii imenikamua haja kubwa manake nilii-test kwa kujitumia email lakini nikaipata baada ya karibu dakika 15 lakini potelea mbali. Mtu niliyepata akili zama za kutumiana barua unafikiri nitatishika na dakika 15 za kupokea email?! Hapa ni mwendo wa "Akuanzie Mmalize". Full Hujuma.
Kwanza kutumia 10K kwa wiki kwa intaneti peke yake ni anasa za kijinga. Kuanzia sasa nitaingia Youtube endapo tu ile data cap/limit ya 500MB haijakamilika kwa siku husika. na Instagram naingia kwa machale. NI mwendo wa kukomoana tu! Nilikuwa naangalia Game of Throne, nitaishia Season 4; kwani kuna tatizo? Nina zaidi ya 100GB ya tutorials ya mambo ninayosoma, kwahiyo wala sihitaji za ziada, manake hata hapo kale unaweza kukuta topic moja nina video zaidi ya 5 za watu tofauti tofauti. Ni ujinga tu kwa sababu x + y =5 haina tofauti yoyote na m + n = 9 -4.
Anayekuhujumu, nawe mhujumu! Hapa angalau 50% tu ya watumiaji wa intanet wakipunguza matumizi kwa 50% huku wengine wakitumia kama zamani, amini usiamini, lazima waombe poo hawa wanyonya damu, na kwa Jina la Bwana Aliye Hai, hii vita nitashinda!