Nimeamua kusitisha matumizi kwa aliyekuwa mke wangu, kisheria nina makosa?

Nimeamua kusitisha matumizi kwa aliyekuwa mke wangu, kisheria nina makosa?

Anaomba msaada wa kisheria mnamletea ukatoliki eti watoto ni baraka! Acheni hizooooo
 
Habar zenu wakuu.

Miaka7 iliyopita nlikua na mwanamke tuliishi nae na tukapata watoto wawilii lakini ndani ya uhusiano huu pia tulienda kwa shehe tukafunga ndoa ili tupate cheti kwasababu hyu bibie ni mwalimu na alikua anataka apate uhamisho ahamie mjini kwani alikua akifundisha nje ya mjini.

Hapo ndani maisha yetu mwanamke alikua mkorofi mnoooo mlevi na pia usaliti ndani yake. Sasa kwasababu kule anapoishi ndo kulikua na biashara zangu nikawa naishi kwake nayeye akija mjini anafikia kwangu alizidisha ukorofi hdi akanifukuza kwake nikaondoka nikaendelea na biashara zangu nikanunua gari mbili huku nahudumia watoto.

Hatimae namimi nikaoa kwani mimi ni muislamu na nmepata mtoto mwingine hpo ndo mwalimu akaanza kunisumbua nimuandikie talaka. Wakati huo huo siruhusiwi tena kuwaona wanangu naninalipa ada na pia hela ya matumizi kila wiki. Baada ya kunizuia nimekata huduma zote.

Jee kisheria hapo nina makosa asanteni wakuu naomba ushauri wenu. Natanguliza shukrani
Mkuu, pole sana kwa mikasa. Usiache kutuma pesa ya matumizi kwa watato wako kwa kuwa huyo mlevi hatopata shida ila watoto ndio watapata shida... Vumilia kwa kuwa watoto wakiwa wadogo ni wa mwanamke ila wakifika miaka saba utakuwa na uwezo wa kuwachukua.
Kama fedha unazomtumia anazifuja mtumie kidogo kidogo. Labda wiki hii unatuma laki, wiki ijayo tena unatuma laki ivo hivyo kulingana na mahitaji ya watoto. Wewe usiwe na story naye. Just mtumie kwenye tigo pesa/ Mpesa huku ukimblock asikupigie wala kuwa na mawasiliano naye ya aina yeyote...
 
Asante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom