Nimeamua kusitisha matumizi kwa aliyekuwa mke wangu, kisheria nina makosa?

Anaomba msaada wa kisheria mnamletea ukatoliki eti watoto ni baraka! Acheni hizooooo
 
Ina maana hajui shule anayosoma wanae?
Shule zote si wana akaunti????

Labda atoe ufafanuzi zaidi, nilichokielewa ni kama anatuma hela kwa mama halafu mama ndo anafanya hayo malipo.
 
Mkuu, pole sana kwa mikasa. Usiache kutuma pesa ya matumizi kwa watato wako kwa kuwa huyo mlevi hatopata shida ila watoto ndio watapata shida... Vumilia kwa kuwa watoto wakiwa wadogo ni wa mwanamke ila wakifika miaka saba utakuwa na uwezo wa kuwachukua.
Kama fedha unazomtumia anazifuja mtumie kidogo kidogo. Labda wiki hii unatuma laki, wiki ijayo tena unatuma laki ivo hivyo kulingana na mahitaji ya watoto. Wewe usiwe na story naye. Just mtumie kwenye tigo pesa/ Mpesa huku ukimblock asikupigie wala kuwa na mawasiliano naye ya aina yeyote...
 
Asante sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…