Nimeamua niache kazi nikajiajiri

Hongera kwa kuacha kazi ila uwe tayari kuzikabili changamoto za kujiajiri...Acha kazi uipate kazi ya kuitafuta kazi ya kujiajiri

Sikiliza wimbo wa Nikki Wa pili ft Ben Pol and G nako - Sitaki kazi upate Kujifariji kidogo
 
Mkuu umesema vyema ila punguza uoga kujiajiri sio ngumu kama tunavyo fikiria ila kuchukua maamuzi ndo kazi ukisha Fanya maamzi huwezi kujuta hata kidogo
 
Hapa tunadanganyana.kama umepata pa kujishikiza.komaa hapo hapo.usiache kazi uende kujiajiri eti una laki 5.hyo unaona hela?ni afadhali uendelee kuajiriwa.alafu ufungue vijibiashara.uweke watu.lakini si kuacha kazi.
Mkuu asante kwa kusema kitu ambacho wengi hatujui
 
hongera sana kwanza unuthubutu ilo lina stahiki pongezi

kutokana na kuwa na mtaji wa laki tano nadhan ungejaribu kutizam fursa z kilimo km utvutiw nazo zinlipa

au kama hauko interested na kilimo nadhan wakuu wako watakupa fursa
 
Duh you people hii mnasema kufurahisha genge amaa...hehe ujue inategemea na unafanya shughuli gani, Kuna kazi zinawalipa watu jmn acheeeniii mjasiriamali hatii mguu
Ss waweza mshaur mtu kweli aache ukurugenz akauze karanga kisa ni Ujasiriamali?..
Mkuu kuna wakati akili za wachangiaji zinawatosha wenyewe ujasiliamali hauhitaji mbwembwe inahitaji umakini kuacha kazi sio tatizo tatizo umejipangeje? na tatizo sio kujipanga tatizo unacho enda kukifanya unakijua?
 
Mkuu umesema vyema ila punguza uoga kujiajiri sio ngumu kama tunavyo fikiria ila kuchukua maamuzi ndo kazi ukisha Fanya maamzi huwezi kujuta hata kidogo
Nimekuelewa mkuu lakini si kweli kuwa ukishafanya maamuzi huwezi kujuta.Hujawahi kuona biashara zikifa na mtu akajuta, wengine mtaji waliupata kwa mkopo. Tatizo stori za kwenye vitabu hazituelezi hali halisi na changamoto za kujiajiri.

Nilishawahi kujiajiri lakini kwa sasa nimeajiriwa. Hata hivyo niliwahi kuongea na baadhi ya wadau walioajiajiri na kuangalia miradi mbalimbali. Sizungumzii hizi biashara ndondogo za kutafuta hela ya kula na kulipa kodi ya pango kama ya kuuza karanga barabarani.

Sipingani na swala la kujiajiri, lakini kuacha kazi ili ukajiajiri inabidi uwe makini sana. Kujiajiri sio rahisi kama wengi wanavyotaka kuaminisha wenzao.
 
Mkuu nashukuru kwa ushuda wako kujiajiri kuna changamoto zake ila pamoja na changamoto kuwa nyingi ukiwa mvumilivu utayaona matunda yake shida inakuja je unapo jiajiri umejipanga kupambana hizo changamoto?
 
Ujasiriamali huu si mchezoo... Ujasiriamali sio kila kitu mkuu,inategemea na Ujasiriamali, Fate ya muuza karanga vs fate ya mkurugenzi ,SMH...
I admire Ujasiriamali if it pays more than a job not otherwise...
Mkurugenzi wa kampuni ya nani?
Maana mimi nauza karanga leo..lakini kesho nitafungua kampuni ya kusambaza na kulima karanga,na nitahitaji mkurugenzi,je hauoni Ladyred kua utaleta tena cv yako kwangu kuomba kazi ya ukurugenzi wa kampuni ya karanga ambayo imetokana na kuuza karanga barabarani.

Waafrica tunapenda sana readymade,hatutaki shida.
 
Daah...!! Ongera sana imejivua utumwa ila heshimu maamuzi yko wala usije kujilaumu kwa maamuzi yako.

Biashara zina changamoto nyingi inawezekana ukaanza vizuri au vibaya katika biashara utakayoanza ila usife moyo biashara ni uvumilivu kuna PANGO,TRA,MANISPAA ,ULINZI SHIRIKISHI ,USAFI etc .. wote hao ni wageni wako unapaanza biashara.

Mimi nlikuwepo huko lkn nilijivua mapema sahvi nikifika kwenye biashara zangu vijana wanasema boss kaja.

Nlikuwa naosha gari za watu sahvi naoshewa, Nlikuwa naomba gari za watu sahv naombwa mimi

Yote maisha kujipanga tu Mkuu
 
Uko na situation na mawazo kama yangu, tangulia mkuu nami nakuja huko.

Changamoto:
~Kuna kupanda na kushuka katika kila biashara(usikimbilie nguvu za giza);
~Kuna wateja wengi watukutu-wenye lugha chafu, dharau, dhuluma, etc..(nenda nao taratibu, usivunje sheria);
~Government policy- utapambana na kodi na makato mbalimbali kuendana na biashara yako (tii sheria, jitume ili upate faida ya kutosha, faida yako isiishie TRA);
~Kuna watu wabaya, eg. majambazi, huwa wanaharibu biashara za watu wengi especially maduka (muombe Mungu ulinzi, pia mtaji wako ukikua wekeza sehemu nyingi tofauti kadri utakavyoweza, hapo ukiibiwa n kama unatekenywa tu);
Etc...etc...

Faida:
~You will be your own boss (hakuna kupelekeshwa);
~Kipato chako kitaongezeka kulingana na juhudi na ujanja wako (be creative);
~Hakuna pressure za kukaguliwa vyeti wala kutumbuliwa (wewe ndiye mtumbuaji);
Etc...etc...

NB:Tunza vyeti vyako vizuri, biashara si fani ya kila mmoja.
 
Hahaha ujue mnachukulia easy sana Ujasiriamali, em niambie na hio laki tano unalimaje na kusambaza karanga,unafunguaje kampuni?? Unadhani ni ishu ya leo na kesho Hio??huu mchezo kaufanya bakhresa for 30 plus years... Bakhresa tunao wangapi, tuwe realistic...
Nakubali yawezekana ila sio easy kama unavoiweka hapa eti leo kesho subutuuu,watu tuko makazini sio kuwa Ujasiriamali hatuujui ohoo..u need a plan,Ujasiriamali mwingine u need work experience kwanza nk, hizi za kubahatisha hizi utaachieve vipi vision kwa kubahatisha tu??
I know some people wenye kampuni zao it's a life time process sio leo na kesho msifarijiane
 
Ieleweke wazi pia wewe ndo kampuni kampuni ndo wewe, so it is work work work work work and work muda woote,hizi show za kuwa na kampuni sio za sa 11 unaachia desk, ts ur company u work all the damn time...u should live with these people wenye makampuni jmn,sijui km kuna watu wanafanya kazi kama hawa...habari za ur own boss ni badaaee sanaa, huku from scratch ni msoto mwanzo mwisho
 
Ni kweli dada inahitaji kujituma sana, pia pressure na kisukari huwa havikawii endapo mtu hana ujasiri na uwezo wa kuhimili mikiki!
 
Kwa uzoefu wangu lazima uwe mvumilivu Sana, usiwe mwepesi kukata Tamaa. Umeingia safari yenye mihangaiko mingi kufika unapotaka kwenda. Lazima udefine lengo unataka kufika wapi. Kazania hadi ufike. Wengi watakukatisha Tamaa, marafiki zako watakuwa watu wasio enda Shule, watakudharau, maneno Ya kuudhi lakini we vumilia... USIJE KATA TAMAA KABISA.. lazima upate watu wa kukutia nguvu, soma vitabu. Kunjua moyo hata ukifail Mara kadhaa nyanyuka songa mbele.. Ukipata hasara vumilia.. Never give up
 
Hongera, laki 5 ni hela nyingi sana Kwa mtaji. Ila pia ni hela ndogo kama, hutakua serious. Ili ushauri uwepo lazima mshauri ajue uko wapi mazingira gani na ikoje. Ni whatsup 0762208190 Kwa ushauri zaidi
 
i) Hali ya uchumi mitaa ya Africa si nzuri imagine majirani zetu Kongo wameshindwa ku raise $ kwa uchaguzi...

ii) Pamoja na hayoooo yaeza kuwa matakwaaa.. yao hao DRC
Fanya utafiti kuhusu soko lako..
wanaeza nunua nini?
kwa kiasi gani cha pesa....
wana pesa kiasi gani????uwezo wao mfukoni???

iii) Maisha ni kuishi kwa kupenda ufanyalooo..

penda kazi yako....develop passion it is not about monie boss..


Sincerely,

The Beast!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…