Nimeamua niache kazi nikajiajiri

Kuna matapeli humu
Humu wapo watu wa aina zote unazozijua na usizozijua duniani....

wako mapadre wachungaji mashehe maaskofu masista wateja mashoga mabasha vibamia mandingo bwawa visima

wamo pia maduu matozi usalama wa taifa usalama wa raia marais wananchi wapiga kura wabunge madiwani madalali wezi majambazi

wako vibonge wembamba wasomi

wamo timu simba timu yanga timu kiba timu WCB wako timu muziki mzuri na timu ujanjaujanja

wapo pia bingo fleva na wapo bongo movie mazombii mazumbukuku wa insta wa fb wa viber wa Twitter wa badoo na takataka zozote unazozijua na usizotarajia kuzijua leo wala kesho
 
Acha kujitafutia shida. Huki sio kipindi kizuri cha kujiajiri. Utakuja kupata magonjwa ya moyo bure. Sasa kama elimu yako mbuzi kwa nini usitumwe tumwe? Kama hupendi kutumwa kaongeze elimu...
Acha kumtia woga dogo....hakuna kipindi kizuri kama hiki kujiajiri....fursa za kumwaga. ...tangu nimezaliwa unga wa ugali haujawahi kuuzwa kilo buku miatatu...Leo unauzwa buku mia nane....
MUNGU akupe macho ya kuona wengine wanachokiona....
 
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
HONGERA mkuu....nani nitoe ushuhuda wangu...2008 August 08 naacha kazi rasmi...mke hanielewi wazazi hawanielewi na hata washkaji hawanisomi kabisa wanaamini kuna mchango unaolipa zaidi ndio nimeufuata....nikamwambia no naacha kazi naingia mtaani kupamban mwenyewe...

ila wife nilimjenga kisaikolojia kuwa asishangae tupo nyumba ya kupanga maisha yanaweza kukataa tukatimuliwa na pia asishangae katikati ya jiji tukapikia kuni na maisha yakasonga...so alinielewa kuwa tunakoenda sio kuzuri tujipange.

sekeseke likaanza. ..ndani ya mwezi wa kwanza tangu niache kazi nimeanza kugongea buku la vocha kwa wife....plan zangu kumkichwa...baadae nikapita nssf yangu kama 5mil nikajipanga nikalianzisha....napiga kazi ya kwanza nikakopwa kama 18mil ndani ya mwaka mzima....nilivyokuja kulipwa the rest ni story na huwa nasikitika mtu anavyoogopa kuacha kazi kama vile ana ubia na mungu kuwa ajira yake ndio maisha yake....

kulala njaa kutembea kwa miguu kukesha unafanya kazi na kutolipwa kwa wakati ni changamoto za kila anayejiajiri.
ubunifu katika kazi zako unyenyekevu heshima ya matumizi ya pesa na kufanya kazi kwa bidii huku ukimwomba sana MUNGU ndio siri ya mafanikio katika kila story ya aliyejiajiri
 
Mkuu kuogopa ni sawa na kuwa umekufa changamoto zinavyo kuwa nyingi ndo akili inaongeza namna ya kufikiri mpaka kuyafikia mafanikio
 
Ushauri wa kuoga huu. ...hakuna kitu inanikera kama msomi anaposema unatake calculated risks...upuuzi daraja la kwanza. ...risks are just risks no more no less.
umwamua kuacha kazi acha ingia mtaani mengine muachie mungu....finito.
Sawa kila mtu na maoni yake, naheshimu mawazo yako mkuu ila kumbuka kuna watu walishaacha kazi baada ya muda mfupi wakarudi kulilia Kazi, kuacha Kazi ni jambo zuri ila unahitaji maandalizi ndo maana watu wengi utasikia alifanya Kazi kisha akaacha akafungua biashara it means alijipanga kabla ya kuacha
 
Acha kujitafutia shida. Huki sio kipindi kizuri cha kujiajiri. Utakuja kupata magonjwa ya moyo bure. Sasa kama elimu yako mbuzi kwa nini usitumwe tumwe? Kama hupendi kutumwa kaongeze elimu...
ha ha ha et nichum nibebike.. kweli majina haishi

but pole kwa kuogopa maisha nyie ndio mnajaribu siku mkistaafu aalafu mnasingizia kulogwa
 
Acha kujitafutia shida. Huki sio kipindi kizuri cha kujiajiri. Utakuja kupata magonjwa ya moyo bure. Sasa kama elimu yako mbuzi kwa nini usitumwe tumwe? Kama hupendi kutumwa kaongeze elimu...
Mkuu me nawachora2 hao wanaomsaport, hali kwasasa sio shwar kitaa nivizur kabla ajaacha kazi angeshaanza hiyo biashara ili aje akiwa nauhakika waatachokifanya, mliobahatika kupata ajira nivizur mkaanzisha miradi mingine mkiwa bado mpo kwenye ajira ila usiache kazi hali yakuwa bado ujajua utafanya nini
 
Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi... Hongera kwa kujikomboa ktk fikira za utumwa wa mkoloni mwajiri... Mi niko njiani nakamilisha tu taratibu za kutoka ktk utumwa.Bora nami nikawe mkoloni.
 
Daah! kuajiriwa ni utumwa wa kudumaza akili...lakini mm nakushauri kitu kimoja piga kazi.
 
ningekuwa sina mkopo kazi ningeacha ila huu mkopo unaniongezea miaka ya kuwa utumwani na maujuzi yangu ya kujiajiri yanazidi kupungua makali shiiiitt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…