Nimeamua nifanye biashara ambayo mahesabu yananionyesha nitapata hasara

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2016
Posts
4,707
Reaction score
11,365
Wakuu,

Baada ya mwaka jana mwezi wa tano kuamua kufanya biashara ya mchele na namshukuru Mungu inanilipa vizuri mpaka sasa.

Kipindi naanza biashara nilikuwa nipo mwaka wa pili chuo flani, na sasa nipo mwaka watatu nategemea kumaliza mwakani nihitimishe masomo yangu.

Lakini baada ya mwaka kumalizika nimefanya tathmini nikaona heli nifungue kibiashara kingine, ingawa katika hali yakawaida nikipiga mahesabu kwenye karatasi inanionyesha nitapata hasara lakini dhamira iliyopo moyoni inaniambia nitapata faida nisiogope kufanya.

Biashara yenyewe nikuwa nimefungua "Kibanda umiza, cha kuangalia mpira."
Baada yakuona watu wanaenda mbali kuangalia mpira halafu huduma wanayoipata wanalalamika mbovu na kila mechi wanalipia 1000. Ila mimi nimeamua kuliweka center flani hivi na nitaonyeshea kwa sh 700.

Je kwa wale wenye ufahamu na biashara hii wanaona nitatoboa kweli japo kupata hela ya kula na kulipa kodi ya chumba tu?
 
Labda alisoma lakini hakusoma vizuri.Asante kwa kumuelewesha ndugu yangu.
Ndg jifunzeni kujibu baada ya kusoma siyo ujibu kwanza ndipo usome. Wapi kasema ameacha biashara ya mchele? Mfumo wetu wa elimu ufumuliwe tu maana inatuaibisha
 
Tuanzie hapa
1. Unataka kutumia king'amuzi gani?
2. Bundle gani/na gharama yake ni kiasi gani?
3. Umeme utatumia kiasi gani?
Sasa tuje kwenye targeted population niyakutosha na itaendana na bei ambyo umepanga
 
I have same idea
Nimeshapata eneo la kukodi ambalo lipo centre kwa eneo nilipo
Nataka kujenga banda ambalo litakuwa na capacity ya watu 200
Kwa wenye uzoefu zaidi naomba mnijuze
 
Ndg jifunzeni kujibu baada ya kusoma siyo ujibu kwanza ndipo usome. Wapi kasema ameacha biashara ya mchele? Mfumo wetu wa elimu ufumuliwe tu maana inatuaibisha
Kweli mkuu nakuunga mkono ufumuliwe kabisa hausaidii chochote, maana hata ww umeandika maneno mengi kweli ila hakuna mchango wowote kuhusu tatizo la jamaa uliotoa
 
Tuanzie hapa
1. Unataka kutumia king'amuzi gani?
2. Bundle gani/na gharama yake ni kiasi gani?
3. Umeme utatumia kiasi gani?
Sasa tuje kwenye targeted population niyakutosha na itaendana na bei ambyo umepanga
1.Azam na DSTV.

2.Azam 15000,DSTV 184000 kwa mwezi.

3.Umeme ni wa luku kwa siku naweza tumia wa elfu tano(Maximum).Population nimeyotagert ni watu 200 mpaka 300 kwa mechi hasa ligi kuu wingereza.Hapo bado uefa.
 
I have same idea
Nimeshapata eneo la kukodi ambalo lipo centre kwa eneo nilipo
Nataka kujenga banda ambalo litakuwa na capacity ya watu 200
Kwa wenye uzoefu zaidi naomba mnijuze
Unwjengea matofali or mabanzi or mabati mimi binafsi langu nilamabanzi limechukua kama million 2 hivi banda tu hapo bado TV na King'amuzi.
 
Unwjengea matofali or mabanzi or mabati mimi binafsi langu nilamabanzi limechukua kama million 2 hivi banda tu hapo bado TV na King'amuzi.
nipe mchanganuo wa cost ulizotumia
 
Aisee mkuu uko vizuri nikupongeze, Kila la heri katika biashara yako cha msingi usikate tamaa...Umiza kichwa juu ya kujua mbinu za kuboresha biashara yako
 
Kuwaita Accacia Wanyonyaji ni upotoshaji.Mkataba wao ni wa kisheria na una pande 2, wao kama wawekezaji na Tz kama mmliki. How comes wawe wanyonyaji? Tusil aumu tulipo anguka bali tulipo jikwaa.Nimtazamo tu!
 
Dhaa!! Hii biashara ya mchele naitaman kichiz,
Mkuu nafkir una uelewa kidogo hebu tiririka hapa
Na mm nijitoe
 
Kaka biashara ya mchele unafanyeje? Tushirikishane. Unatoa wapi mchele na unapeleka wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…