Nimeamua nifanye biashara ambayo mahesabu yananionyesha nitapata hasara

Nimeamua nifanye biashara ambayo mahesabu yananionyesha nitapata hasara

Mkuu
Wakuu baada ya mwaka jana mwezi wa tano kuamua kufanya biashara ya mchele na namshukuru Mungu inanilipa vizuri mpaka sasa.

Kipindi naanza biashara nilikuwa nipo mwaka wa pili chuo flani,na sasa nipo mwaka watatu nategemea kumaliza mwakani nihitimishe masomo yangu.

Lakini baada ya mwaka kumalizika nimefanya tathmini nikaona heli nifungue kibiashara kingine,ingawa katika hali yakawaida nikipiga mahesabu kwenye karatasi inanionyesha nitapata hasara lakini dhamira iliyopo moyoni inaniambia nitapata faida nisiogope kufanya.

Biashara yenyewe nikuwa nimefungua "Kibanda umiza,cha kuangalia mpira."

Baada yakuona watu wanaenda mbali kuangalia mpira halafu huduma wanayoipata wanalalamika mbovu na kila mechi wanalipia 1000.Ila mimi nimeamua kuliweka center flani hivi na nitaonyeshea kwa sh 700.

Je kwa wale wenye ufahamu na biashara hii wanaona ntatoboa kweli japo kupata ela ya kula na kulipa kodi ya chumba tu?.[/Mkuu hongera kwa kuthubutu, binafsi ningekushauri kwanza ustick kwenye biashara 1(mchele) ujiimarishe na kuitanua vzr ndipo ufikirie kudivesify. Pongezi sn mkuu. By the way nikuombe unipe abc za biashara ya mchele maana najiandaa kuingia huko ila bado cjapata mtu wa kunidadavulia zaidi. Ubarikiwe.
 
Kweli mkuu nakuunga mkono ufumuliwe kabisa hausaidii chochote, maana hata ww umeandika maneno mengi kweli ila hakuna mchango wowote kuhusu tatizo la jamaa uliotoa
Uko sahihi mkuu maana hata wewe umejikita kwenye mapungufu ya mchangiaji huyu sio kumshauri mleta mada.

Mkuu mleta mleta mada yafuatayo ni mambo ya msingi kuzingatia katika hilo unalotaka kufanya
1/mahali unapotaka kuweka biashara yako
2/aina ya wateja watarajiwao ,hali zao kiuchumi na makadirio yao kiidadi
3/Aina ya kisimbuzi/visimbuzi unavyotarajia kutumia na gharama za vigurushi
4/gharama ya umeme na nyinginezo
Hapo ukiweza kufanya mahesabu vizuri unaweza kupata jibu ila usitegemee matokeo ya mda mfupi. By the way biadhara yoyote inahitaji ubunifu ni jambo la msingi
 
Wasomi raha sana risk cost analysis nyingi pia kuja na altenative solution ndio maana hadi kuna watu wanashuka ubungo kila Leo baada ya mwaka uchumi wake unakua mkubwa kuliko vijana wa mjini . Nakushauri mkuu tumia kisumbuzi cha dstv na azam tu maana vinginevyo matangazo yatakatika katikati ya game . Visumbuzi vya ujanja ujanza sio gurantee maana kila mda mfulani vinakatiwa channel. Utarudisha hela za watu
 
Back
Top Bottom