Nimeamua rasmi kuacha kuishabikia Simba

Nimeamua rasmi kuacha kuishabikia Simba

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
habarini wakuu?
kiujumla mimi nilikuwa mshabiki mkubwa wa timu hii ya msimbazi,lakini kwa kutazama future ya timu hii nimegundua haipo vizuri,hali hiyo ikapelekea kutojihusisha nayo kwa muda ikiwa ni pamoja na kupumzika kufuatilia soka la kibongo !
kuna rafiki yangu akanipigia simu na kuniuliza kuwa amesikia nimehama timu mimi nikamwambia kuwa sijahama timu,yeye akanishauri niende nikaondoe dought ktk tawi letu la klabu la hapa mpira pesa magomeni mikumi,mimi nikamwambia waambie kwa niaba yangu!
basi rafiki yangu huyu akawaambia jamaa yupo simba na hatoacha kushabikia simba,
mimi nilivyorudi nikasikia maneno hayo!na juzi katika ile mechi na mwadui ilivyoisha ninasema hivi"HUWEZI KUWEKA NADHIRI NA KLABU YA SOKA,MIMI NIMEACHA KUSHABIKIA SIMBA RASMI NA NAENDA KUTAFUTA CHANGAMOTO NYINGINE SEHEMU NYINGINE"
haiwezekani simba ininyime raha na arsenal ininyime raha...
hivyo nafikiria yanga au azam kuwa kimbilio langu wakati arsenal fc nitaitolea tamko tarehe 2 sept baada ya dirisha la usajiri kufungwa...
siku njema
 
manchester city,chelsea,barcelona,juventus,psg,tp mazembe,azam,yanga,
ni timu nzuri kuzishabikia
 
Mmmh!!!! Kama ulikua na msaada kwenye club sawa, kama ni shabiki tu kwaheri wasalimie uendako
 
Mmmh!!!! Kama ulikua na msaada kwenye club sawa, kama ni shabiki tu kwaheri wasalimie uendako

unajuaje kama sikuwa na msaada?au wewe unajua mtu lazma awe friends of simba ndo awe na msaada na simba?au unajua wenye msaada ni kina zakaria hanspope na mzee kinesi ?

think out the box
 
Tanzania shabikia Yanga, Majuu shabikia Manchester United hapo utakuwa na amani moyoni mwako.

ahsante kwa ushauri ila man u hawa niliowaona juzi na newcastle hawanishawishi
 
Ni shabiki usiyejitambua, na sidhani kama unajua kwa nini unashabikia timu hii unayoishabikia.

Wewe hukupaswa kuondoka mwenyewe kushabikia simba ila ulipaswa kufukuzwa kabisa
 
We sio mnazi wa mpira hata hizo timu nyingine pia zitatetereka utahama pia bora uache kushabikia mpira kashabikie Netball au Tennis tena mshabikie Serena huwa hashindwi
 
Ni haki ya mashabiki kuhama club kama kuna sababu za kutosha mimi nilikuwa mshabiki mkubwa wa Arsenal baada ya kunizingua muda mrefu ikabidi niamie Man United.Kama mchezaji ruksa kuhama,meneje ruksa kuhama kwanini iwe taabu mshabiki,mpenzi kuhama ebo.

nimependa maneno yako!ahsante
 
We sio mnazi wa mpira hata hizo timu nyingine pia zitatetereka utahama pia bora uache kushabikia mpira kashabikie Netball au Tennis tena mshabikie Serena huwa hashindwi

mimi ni shabiki na mpenzi wa soka
 
Simba timu mbovu sana kuanzia uongozi mpaka wachezaji, kazi yao kuchagua viongozi wenye gubu , pia inasajili wachezaji waliongoza kufunga magoli kwenye ligi za nje bila kufanya utafiti wa kutosha kwamba walibahatisha au juhudi zao binafsi. Pia Simba imeathirika kisaikolojia kwa kushindwa kufanya vizuri miaka kadhaa mfululizo na wasipokaa vizuri mwaka huu wanaweza kushuka daraja.
 
timu hii haina mipango,usajiri umeshafungwa lakini hadi leo bado inakomaa na usajiri!

mara papaa niang amekuja na mabegi mwalimu anayehama kituo cha kazi,kumbe mtalii!amecheza mechi 1 anasepa,sasa wamemleta nd'aw naye itakuwa hivyohivyo!

hivi hizi gharama za kulisha na kuhudumia watu wasio na faida si bora ukasaidie watoto yatima kule fire!ah hawa ni wafanyabiashara tu na hawana nia nzuri na hii timu!na hawa watalii wanaokuja kufanya trial simba ni wabeba sembe tu!kwa maendeleo na ustawi wa simba fukuza hanspope na genge lake kwanza
 
Back
Top Bottom