Nimeamua rasmi kufunga biashara

Acha ulaini broo, maisha yana risk na uncertainty za kila aina kupigwa tu faini unataka kugive up

Hebu negotiate nao, nenda kwa Mkurugenzi if possible jieleze most of them hao wanatakaga tu za kula ila angalia kosa hilo je lina adhabu ya namna hiyo??
No smooth road at all
 
kama kweli una nia ya biashara ishu kama hiyo haipaswi kukukatisha tamaa.....au hujui future yako imesimamia wapi....kilimo au biashara.....hakula jepesi ktk yote.......jipeleke mwenyewe municipal, kitengo cha leseni, mueleze kila kitu.....
Ila tambua leseni ni lazima na ni muhimu....pole kwa yote
 
Uliwahi kufanya biashara yoyote kabla? au iyo ndo biashara yako ya kwanza kwasababu tu uliachishwa ajira? naomba unijibu ili tuendelee na majadiliano.
 
Cheza Forex
 
Nilipigwa faini nilipokwenda baada ya mwezi nikasema nataka kufungua biashara ,nataka lesani wakaniuliza ulifuatwa na kuandikiwa uje nikasema hapana ....nimekuja tu mwenyew .nililipa leseni nikaamshaaa.

Haya maisha bro hakuna wa kukuonea huruma komaaa acha ujinga wa kufunga biashara ........nenda kawapige sound afuu uwe na maneno mengiii ya kuwaplease na kuwakwezaaaaa....usijifanye mjuaji .mapema sanaaaaa unatoka na leseni yako baada ya kulipa wiki tu unaikamata ..kiufupi maisha ya biashara ni ya kukimbizana hpo bado watu wa afya,watu wa mazingira ,Chuma ulete na wezi plus wenye roho mbaya wote hawa inabd upambane nao na sio ww tu .
 
Mie watu wa afya nilishindwana nao...nikasema easy..nikaweka biashara yangu hom...wanachosha balaa
 
Bado
Hapo bado hajakutana na wadulumati, wakopaji wanachelewesha kulipa, wezi wanavunja wanaiba, wakabaji wanakuvizia umefunga biaashara wanakutaimu uwape hela ya mauzo Yani balaa tupu. Akomae tu.
 
Hakuna haja ya mkurugenzi. Hicho huwa ni kitengo cha Afya mazingira.

Hapo azungumze na waliompiga fine kiutu uzima.
 
Unachanganya madesa sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…