Samico Tanzania
JF-Expert Member
- Feb 6, 2022
- 791
- 1,852
Barua hii nimeiandika kuiomba serikali yetu ibadilishe matumizi ya fedha AFCON Ili mafundi tupate pesa za kutalii kiufundi ulaya.
FUNDI SAMICO,
P.O.BOX.
SAMICO TANZANIA,
KWENDA: Wizara ya Michezo(TFF)
P.O.BOX
DODOMA
TANZANIA
YAH: OMBI LA KUJIONDOA KWENYE MICHUANO YA AFCON NA KUELEKEZA RASILIMALI KATIKA MAENDELEO YA UJUZI WA MAFUNDI
Ndugu wahusika,
Kwa heshima na taadhima, naandika barua hii kwa niaba ya mafundi Tanzania, chini ya jina la Fundi Samico Tanzania, kuwasilisha ombi hili muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu.
Natambua mchango mkubwa kutoka ofisi ya waziri mkuu katika kuendeleza fani za ufundi nchini.
Naomba mamlaka husika zifikirie kwa kina uwezekano wa kujiondoa katika michuano ya AFCON kwa kipindi hiki, na badala yake kuelekeza rasilimali zinazotumika katika shughuli hizo kwenye kukuza ujuzi wa mafundi wa Kitanzania.
Ninaamini kuwa uwekezaji katika maarifa na teknolojia utaleta faida ya kudumu kwa taifa letu.
Pendekezo langu ni kutumia rasilimali hizi (Fedha za Goli la mama na shirika letu pendwa la ndege) kuwawezesha mafundi kusafiri na kujifunza katika nchi zilizoendelea kiteknolojia, hususan China, ili kupata uzoefu wa moja kwa moja katika viwanda na teknolojia za kisasa. Hii itasaidia sana kuijenga Tanzania yenye uchumi wa viwanda na kujitegemea kiufundi.
Ni rahisi kwa matokeo ya michezo kufutwa, Kubadilishwa na kuumiza mashabiki LAKINI ujuzi na maarifa yatakayopatikana kwa mafundi yatabaki kuwa mtaji wa kudumu kwa taifa letu.
Tunaamini kuwa hatua hii italeta mabadiliko chanya na ya kudumu katika maendeleo ya nchi yetu hususani kipindi hiki cha mageuzi makubwa ya tehama.
Naomba kuwawasilisha.
Imeandikwa na Fundi Samico 0711756341