Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

majibu murua
 
=========12/02/2022=====

PIA SOMA "NIMEANZA UJENZI" Nimeanza ujenzi, kaa hapa tujenge pamoja

TUENDEE TULIPOISHIA............
bada ysa kukamilisha kwa wamu ya boma niliamu akuvuta nguvu na kujipanga kwa awamu inayo fuata na yafuatayo ilibidi yafanyike katika awamu hiyo
=== kupaua: hapa nilitumia bati kampuni ya KIBOKO baada ya kushindwa bei za alafu na ando ambayo yalikua ni machaguo yangu. jumla ya bati 120 zilitumika na bati moja iligharimu Tsh 30,000/=
zilitumika jumla ya mbao 280 kwa mgawanyo wa 2/2, 2/3, 2/4 na 1/8 kwa bei ya 2500, 4000, 5000 na 11000/= hela ya ufundi ikiwa ni Tsh 650,000/=.

=== blandering ilitumia jumla ya mbao 110 za 2/2 na na chache sana za 2/3 huku hela ya ufundi ikiwa ni Tsh 400,000/=

=== jengo lina madisha 11 (mawili kati ya hayo ni madogo) na milango miwili mbele na nyuma ambapo GRILL moja ya dirisha iligharimu Tsh 115,000/= na Tsh 45,000/= Kwa dirisha ndogo.. mlango mkubwa uligharimu 195,000/= na mdogo 115,000/= gharama za kupachika grill na kujenga hanamu 2 zilikua 120,000/=

=== kilichofuata ilikua ni kuweka miundombinu ya awali ya maji na umeme ambapo kwa miundombinu ya maji vifaaa viligharimu Tsh 270,500/= na ufundi uligharimu 50,000/= huku miundombinu ya umeme vifaa viligharimu 273.000/= na fedha ya ufundi ikiwa ni Tsh 250.000/=
NB. upauaji na kazi zingine zilianza tarehe 5/01/2022 na kukamilika tarehe 5/02/2022 huku shughuli zote zikigharimu jumla ya THS 8,422,000/=. GHARAMA HIZI NI JUMISHI KWA VIFAA VYOTE.

GHARAMA KUU=== 8,422,000+7,519,500 = 15,941,500/=

tukutane awamu ifuatayo. (mwisho kabisaa nitaweka document ikionesha gharama zote ila itabidi kusubiri document hii itaonesha kila kitu ikiwemo majina ya vifaa gharama zake).


 
Hongera sana Kwa kuwa fighter na Pia kutuhabarisha bila kuchoka. All the best
 
Napenda sana Tofali za kuchoma ila eneo langu mchanga mtupu hakuna udongo kabisa.
Samahani Wakuu, tofali za kuchoma zinapatikana wapi Jijini Dodoma? Nami napenda sana tofali za kuchoma hasa zile ndogo, ukijenga kwa kutumia English Bond zinapendeza sana.
 
Samahani Wakuu, tofali za kuchoma zinapatikana wapi Jijini Dodoma? Nami napenda sana tofali za kuchoma hasa zile ndogo, ukijenga kwa kutumia English Bond zinapendeza sana.
Nami nasubiri jibu utakalopewa🙏
 
Hongera sana kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…