Nimeanzisha biashara Kariakoo, inasuasua nifanyeje iweze kuwa kwenye hali nzuri

-Halafu mkuu mimi kama mteja kusema kweli wateja sisi asilimia kubwa kuingia underground ngumu mno yani Tunapenda maduka ya nje nje maana wakati mwingine kitu kinaweza kukuvutia tu kwakua umekiona na wala sicho unachokitafuta , ukakinunua
Lakini Kuingia underground nmeshasahau hata niliingia lini, na wengine hawajui kabisa kama kuna Maduka chini
 
Yah nauza jumla na rejareja
Ila mkuu unadhani nifanye kitu gani ama niongeze nini ili graph yangu ya biashara iweze kwenda vizuri???
Jaribu kutumia mitandao ya kijamii kama hapa JF,Insta,twiter,whatsapp na FB kutangaza biashara zako utalna mabadiliko
 
Mchawi wa Kwanza ni kuwa underground floor mkuu,ni bora frem za ndani za floor ya kawaida.

Nguo unauza jumla ronya au quality reja reja au quality jumla?
Mkuu wengi wanaonunua reja reja ndio sana huishia huku nje, ila mizigo mingi ya jumla watu wanazama chini sababu ya unafuuu...

Nimuulize mtoa mada Ariri...

Je mzigo unaenda kuchukua mwenyewe nje au unaletewa?
 
Mkuu wengi wanaonunua reja reja ndio sana huishia huku nje, ila mizigo mingi ya jumla watu wanazama chini sababu ya unafuuu...

Nimuulize mtoa mada Ariri...

Je mzigo unaenda kuchukua mwenyewe nje au unaletewa?
Imekua Ni ngumu sana kwa kipindi hiki Cha janga la corona kwenda kufuata mzigo nje...kwa sababu hiyo basi nimekua nikiagizia mzigo
 
Hapa hapa kwenye uzi kaanza kupata wateja,,angeunga juu kwa juu na kuanza kutundika bidhaa😁😁
Kwl kabisa mana hata humu wateja wapo..
Unazo boxer za kiume.?
Kama unazo niza aina gani.?
Kwa bei ya reja reja shngap kwa pic moja na bei ya jumla unauza kuanzia bunda ngapi.? Nabei ya jumla ipoje?
 
Jaribu kutafuta machinga uwape mzigo wakuuzie hapo hapo kariakoo
Ariri ndugu yangu huu ushauri wa ndugu Ndetia ukiuangalia kijuu juu unaweza ukauchukulia poa,ila nikwambie tu kitu boss hapo k.koo hao machinga unaowaona 81% bidhaa wanazouza sio zao,wanazitoa madukani wanakopewa na maboss kama wewe.

K.koo biashara mpk uzoeleke ni uwe n connection na wafanyabiashara wenzako mnaofanya biashara moja ndio utaweza ona biashara ipo,nadhani wewe n muuzaji na pia ni mteja sehemu nyingine,hivi umewahi kwenda duka flani k.koo ukakosa unachotaka kisha yule muuzaji akakwambia kaa subiri,ngoja nipige simu uletewe mzigo wako?

anashika simu anapga ndan ya dk1 tu unaletewa bidhaa uloitaka,unafkiri ile bdhaa inakua imetoka dukani kwake? la hasha! ile bidhaa kaichukua dukan kwa rafiki yake,badae jioni au ukishaondoka tu hela ya watu inapelekwa kule bdhaa ilipotolewa.

K.koo biashara ndio zinavyoenda,ukikaa peke yako dukani eti unasubiri wateja,uta china bro! k.koo kuna wateja wengi sana ila pia k.koo hamna wateja kbsa kbsa "kama hujajipanga kama wewe".

Tafuta kijana/vijana wape kazi wambie Yeyote atakae niletea mteja akanunua kitu "nampa buku" tafuta vijana wako hata 10,wahuko huko k.koo wanaweza kuwa machinga au mawinga wa maduka mengine,wape homework hiyo halafu sikilizia uone balaa lake utavyoletewa wateja hutoamini.

unauza mzigo kwa jumla na rejareja wewe una mtji mkubwa kbsa "acha ubinafsi" tafuta machinga wenye vimeza wanao uza bidhaa/nguo unazouza mwambie nakupa mzigo For free auze,kisha jioni alete hesabu kauza ngapi/kabakisha ngapi.

usikae tu dukani usubiri wateja bro,k.koo wateja wanashikwa mikono unamwambia twende huku mteja anakuja,hivi hujawahi pita k.koo kwenye maduka ukaona mtu anakuita kama anakujua,ukienda anakwambia karibu dukani..Mimi ilishanitokea nilikua napita kwenye duka la simu mdada m1 akaninyooshea mkono kbsa ananiita,nikajua ananijua nikaenda pale kumbe eti ananiita nichague simu,Nikamshukuru (ila sikuondoka bila namba yake)

sasa hivi nipo nae chobingo moja hivi ananiitia wateja kama alivyoniitaga mimi,huo n mfano hai Mkuu,point yangu ni kwamba usikae dukani usubiri wateja,utawapata ila watakuja wakukupa hela ya kodi na matumizi ya siku ila hutoona faida ya wewe kupanuka au kufanya maendeleo mengine.

Funguka,Tafuta Team Kazi k.koo Patamu sana boss,umekosea kosa 1 tu ambalo itabdi upambane maana ndio ilishatokea,Kwenda kupanga frem Shimoni Yani katk blunders ulizofanya hiyo ni moja wapo,shimoni ni maduka ya wazawa wa k.koo wale ambao tyr wameshajitengenezea watejaa kwa muda mrefu na s kwa ajili ya new comers kama wewe.

mzawa hata aende frem ipo kwenye pango tyr ana wateja wako Loyal watamfata popote lipo ila wewe unae anza ulipaswa uanzie huku juu kisha ukishakamata wateja wakutosha ndio unaenda kule chini ambapo kodi nafuu na frem zake ni kubwa,ila kwakua umeshakosea Tusilaumiane saizi,wewe piga kazi Fata ushauri unao ona unakufaa.
 
Mkuu kwa sasa biashara ni ngumu kariakoo yote,mimi pia nina duka huku msimbazi ila najitia tu moyo labda huko mbele mambo yatakuwa sawa.Ila biashara kwa sasa ni ngumu
 
Mkuu kwenye biashara nadhani iko hivyo na hiyo ni khali ya kawaida,hata Mimi hii huwa inanikumba,ikizingatiwa hiki kipindi cha ugonjwa,nikiangalia trend ya mauzo kwenye ka biashara kangu kwa mwezi wa tano na sita mwaka Jana,mauzo kwa miezi hiyo yalikuwa almost 1.5M .cha ajabu mwaka huu mauzo hayafiki hata laki tano

Imefikia kipindi hadi pesa ya kulipa pango natumia kutoka sehemu ambayo haihusiani na biashara hii.kwa hiyo hiki ni kipindi cha mpito na si kwako tu Bali almost many people wanapitia hiki kipindi.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Uvumilivu! .....bila kuwa mvumilivu kwenye biashara...utabadilisha kila aina ya biashara bila mafanikio...na mwisho wake ni stress na kupoteza mtaji.....mwaka wa kwanza kwenye biashara mara nyingi ni maumivu....kwa sababu wengi tunaanza biashara bila kuwa na taarifa za kutosha kama aina ya bidhaa ...bei ya kuuzia...wapi utanunua kwa bei ya faida...kupata taarifa ni kazi ngumu sana....

Hivyo wengi huwa tunaingia kichwa kichwa.....wakati unaendelea na biashara ndipo na taarifa muhimu unaanza kuzipata kutoka kwa wadau wakiwemo wateja na baadhi ya wafanyabiashara wenzio.....cha msingi jitahidi mtaji wako usiyumbe sana...mwaka wa pili utakuwa umeishakuwa mzoefu...utaanza kuona biashara inakuwa na wateja wa kumwaga....

Tena wengine wanakuachia namba za simu mzigo ukifika uwajulishe...cha mwisho ukianza biashara mpya tenga pesa ya matumizi yako binafsi na kodi ya fremu ya mwaka mzima...kamwe usiitegemee biashara kwa matumizi ikiwa bado Changa....biashara ni kama mtoto...alelewe kwanza...faida badae...biashara ni kitu hai!
 
Uyu yupo yale maduka ya underground ambapo ukiweka speaker ya matangazo inakua ni usumbufu kwa wengne sijawahi kuona wakiweka spika kweny zile underground shops kwa uzoefu wang
Inabidi aweke ilikisud awe bold kuliko wengine. Yan mtu atapata kusikia upatikanaj wa bidhaa fulan kabla hata ya macho yake kuiona bidhaa
 
Hongera Sana mkuu ila bado unapaswa kuongeza mapambano ata Kama unaona unasuasua ila hizo ndo changamoto za biashara ko zitumie kama ngazi ya kupandia juu.

Kikubwa zaidi tumia matangazo pia toa promotion fanya ata kwa kipindi cha mwezi mmoja ila hakikisha unawafikia watu wengi baada ya hapo utaona mafuriko ya wateja
 
Usikate tamaa,komaa pia unaweza kupost bidhaa unazouza mtandaoni
 
Mkuu kwa kuwa uko K koo unajua mali unapata wapi ukipata muda fanya suvey Iringa au Dodoma ikiwezekana hamishia huko duka lako.

Ukihamia huko usione aibu kutafuta wateja maana wapo tuu ni wewe tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Embu cheki kwanza na Mshana Jr , MziziMkavu au LIKUD tuone watakusaidiaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…