Jaribu kutafuta machinga uwape mzigo wakuuzie hapo hapo kariakoo
Ariri ndugu yangu huu ushauri wa ndugu Ndetia ukiuangalia kijuu juu unaweza ukauchukulia poa,ila nikwambie tu kitu boss hapo k.koo hao machinga unaowaona 81% bidhaa wanazouza sio zao,wanazitoa madukani wanakopewa na maboss kama wewe.
K.koo biashara mpk uzoeleke ni uwe n connection na wafanyabiashara wenzako mnaofanya biashara moja ndio utaweza ona biashara ipo,nadhani wewe n muuzaji na pia ni mteja sehemu nyingine,hivi umewahi kwenda duka flani k.koo ukakosa unachotaka kisha yule muuzaji akakwambia kaa subiri,ngoja nipige simu uletewe mzigo wako?
anashika simu anapga ndan ya dk1 tu unaletewa bidhaa uloitaka,unafkiri ile bdhaa inakua imetoka dukani kwake? la hasha! ile bidhaa kaichukua dukan kwa rafiki yake,badae jioni au ukishaondoka tu hela ya watu inapelekwa kule bdhaa ilipotolewa.
K.koo biashara ndio zinavyoenda,ukikaa peke yako dukani eti unasubiri wateja,uta china bro! k.koo kuna wateja wengi sana ila pia k.koo hamna wateja kbsa kbsa "kama hujajipanga kama wewe".
Tafuta kijana/vijana wape kazi wambie Yeyote atakae niletea mteja akanunua kitu "nampa buku" tafuta vijana wako hata 10,wahuko huko k.koo wanaweza kuwa machinga au mawinga wa maduka mengine,wape homework hiyo halafu sikilizia uone balaa lake utavyoletewa wateja hutoamini.
unauza mzigo kwa jumla na rejareja wewe una mtji mkubwa kbsa
"acha ubinafsi" tafuta machinga wenye vimeza wanao uza bidhaa/nguo unazouza mwambie nakupa mzigo For free auze,kisha jioni alete hesabu kauza ngapi/kabakisha ngapi.
usikae tu dukani usubiri wateja bro,k.koo wateja wanashikwa mikono unamwambia twende huku mteja anakuja,hivi hujawahi pita k.koo kwenye maduka ukaona mtu anakuita kama anakujua,ukienda anakwambia karibu dukani..Mimi ilishanitokea nilikua napita kwenye duka la simu mdada m1 akaninyooshea mkono kbsa ananiita,nikajua ananijua nikaenda pale kumbe eti ananiita nichague simu,Nikamshukuru (ila sikuondoka bila namba yake)
sasa hivi nipo nae chobingo moja hivi ananiitia wateja kama alivyoniitaga mimi,huo n mfano hai Mkuu,point yangu ni kwamba usikae dukani usubiri wateja,utawapata ila watakuja wakukupa hela ya kodi na matumizi ya siku ila hutoona faida ya wewe kupanuka au kufanya maendeleo mengine.
Funguka,Tafuta Team Kazi k.koo Patamu sana boss,umekosea kosa 1 tu ambalo itabdi upambane maana ndio ilishatokea,Kwenda kupanga frem Shimoni Yani katk blunders ulizofanya hiyo ni moja wapo,shimoni ni maduka ya wazawa wa k.koo wale ambao tyr wameshajitengenezea watejaa kwa muda mrefu na s kwa ajili ya new comers kama wewe.
mzawa hata aende frem ipo kwenye pango tyr ana wateja wako Loyal watamfata popote lipo ila wewe unae anza ulipaswa uanzie huku juu kisha ukishakamata wateja wakutosha ndio unaenda kule chini ambapo kodi nafuu na frem zake ni kubwa,ila kwakua umeshakosea Tusilaumiane saizi,wewe piga kazi Fata ushauri unao ona unakufaa.