Nimebaini haya kwenye uongozi, siasa na hulka za watu

Nimebaini haya kwenye uongozi, siasa na hulka za watu

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,625
Reaction score
89,385
Uongozi wowote ule haukosi upinzani hata kama uwape mahitaji watu wote kwa kutosheleza!, pili kwajinsi mpangilio wadunia ulivyo kuichumi hautoi nafasi kila mtu kuwa na uchumi sawa!, alasivyo mambo yatavurugika na wanaolijua hilo lazima walidhibiti kwa hali na mali!.

Hivyo kuwepo kwa matabaka haya ndio hapo sasa kunaleta mapingamizi n.k ila kwa ataeweza kutoka kwenye huu mtego wa panya huwa wanakaa kimya nakufanya mambo yao!.

Siasa ni sanaa ya uongozi, hivyo viongozi huenda na trend ya kile watu wanataka kusikia, kuona n.k
kama mkifikia hatua yakudanganywa mtadanganywa na yakuambiwa ukweli mtaambiwa!, vilevile kupitia siasa mnaongozwa kutokana na kiwango cha ufahamu wenu, ustaarabu na elimu!.

Taifa kama marekani ambalo watu wanaamini lina sera nzuri za nyanja karibia zote lakini bado mgombea alinusurika kuuliwa mbele ya macho yote!, hii inatakiwa ikufunze kuwa kiwango cha ustaarabu duniani bado kipo chini pili hisia na tabia kwa binadamu ni swala nyeti sana haswa linapokuja kwenye mambo makubwamakubwa!.

Unatakiwa ufahamu wewe leo unagombeza wenzako kwa uongozi mmbaya bila hata kuwa na hakika na hayo, ila wewe pia tukikupa hichohicho kiti kinaweza kikakushinda tena kikakutupa mbali mno!.

hivyo baadhi yenu punguzeni midomo uongozi una si swala lakumridhisha kila mtu hata kama tukiweka vipengele tunavyohitaji tuvifanyie kazi na tukavifanyia bado kuna watu hawataridhika!.

Nanyinyi viongozi kubadilika sio mpaka muombwe bali ni kanuni hata nyakati hubadilika hivyo hata watu malengo yao hubadilika!.

Kama hamuwezi kubadilika basi jiandaeni kubadilishwa!.

Yangu ni hayo machache tu niwatakie siku njema viumbe vizuri....
 
Umenena vyema! Hili nililiona Kwa JPM, pamoja na jitihada zake kubwa wengi walimpinga bila sababu za msingi
kila mtu na maoni yake juu ya kitu chochote kile!, hii huathiriwa na upeo, imani n.k lakini yote kwa yote tunaupimaje ukweli..?
 
kila mtu na maoni yake juu ya kitu chochote kile!, hii huathiriwa na upeo, imani n.k lakini yote kwa yote tunaupimaje ukweli..?
Ukweli unaupima kwa matokeo - results
 
Back
Top Bottom