Nimebaki njia panda Juu ya kufanya maamuzi magumu kwenye mahusiano yangu ya mapenzi

Nimebaki njia panda Juu ya kufanya maamuzi magumu kwenye mahusiano yangu ya mapenzi

Ni kuhusu mahusiano ninayopitia, labda nianze na stori fupi ya nyuma kidogo, nikipokuwa chuo nilikuwa nikidate msichana ambae alikuwa anasoma sec, alipomaliza akaendelea na masomo ya juu yan advanced education, wakati mimi namaliza chuo 2019 yeye akawa amemaliza adv akaenda chuo 2020. Alikuwa ananipenda mno, sasa akawa chuo mim kitaani, nikawa najitafuta nimsapoti akikwama ajira hakuna ila nilijitahidi. Akiwa sec year binti akanibadilikia vby mno, muda mwing yuko bize, nikimkataza kitu anafanya, mfn sitaki kuona ukienda nightparty then asbh nakuta whatsapp status mtu yuko batani. Baadae nikaja kujua anadate na mwanachuo mwenzake, nilijaji akanambia ndo hivyo kweli na mimi sio levo yake, levo yake ni hao wanachuo wenzake mi nimekua sana 😇, ikabidi tuachane💔. Iliniuma sana maana niliwekeza kwake upendo mwingi, baada ya hapo ikanibidi nitulie tu, baadae nikaanza kudate na mwanamke mwingine but sikuwa na future naye coz bado nilikuwa na bado cjapona . Kibishi nikawa nadeti nae baadae nikawa naanza kumpenda kdgkdg, mwaka 2023 mwezi wa 6 akanijuliaha kuwa ana mimba yangu japo ckudhamiria hivyo, mwaka huohuo ex wangu akamaliza masomo yake akapata degree akaja mtaani akanitafuta akaniambia bado ananipenda na mimi ndo chaguo lake, mimi nilimwambia kuwa nina mtu ana mimba yangu, akasema sawa yeye yupo amejirekebisha sasa. 2024 mpenz akanizalia mtoto wa kiume. SHIDA YANGU NASHINDWA KUFANYA MAAMUZI YAFUATAYO:
1 ,Huyu mpenzi wangu nilienaye ameenda chuo udom pia mwaka wa pili, mi nataka kuishi na mwanamke ndani umri umeenda. Naogopa kumsubir anisaliti pia.
2. Ex anataka kurudi anaomba msamaha na yupo tayar anytime, kumbuka bado ananitetemesha japo nikikumbuka ya nyuma bado naumiaga.
3.Natamani kutafuta mwanamke mtaani huku kama vijana wenzangu wanavofanya niishi nae, tuanze upya.
NB: NATOKEA MWANZA, PROFESSION YANGU NI MWALIMU, UMRI 30YRS. samahani kama cjaandika vzr wakuu, kama utanielewa naomba mnishauri nichukue maamuzi gani..
Achana na huyo ex ikiwezekana na namba futa kabisa, kwako kwa saivi anahitaji faraja tu ukute katendwa huko anataka cha kumsaulisha maumivu akipata mtu mwingine atakutema tena, na baadae akitendwa atarudi yani we kwake ni pumziko.


Kama alivosema wewe sio level zake.
 
Nyie ndio mnafanya walimu watukanwe, ex bado anakutetemesha na unataka kumrudia(huu ni ufala) atakuendesha mpaka unye.

Baki na huyo mwenye mtoto wako usiogope usaliti sio kila mwanamke ni malaya kama alivyo huyo ex wako. Usioe mwanamke unaempenda sana na anajua kama huyo ex wako, atakutesa sana.
 
Si mmeona WAALIMU walivyo, ndio maana USAHILI wa kada za Ualimu ni LAZIMA ili kubaini sampuli kama hizi.

Uandishi na uwasilishaji wa mada ni changamoto, huyu ndio aandae notes kwa watoto huko shuleni.
 
Back
Top Bottom