Nimebakiza Kujua Kurudisha Gari Nyuma Tuu

Nimebakiza Kujua Kurudisha Gari Nyuma Tuu

Aisee umetumia tungo nzuri sana kuwakilisha.wale wanafunzi watakuuliza kama una driving certificate
 
Taratiibu naanza kuona chombo chaenda mrama,baharia ataka kuendesha kinyume,utazama topeni usipokua makini! Stage ya reverse ngumu mkuu
 
Nyuma ni hatari sana uwe makini unapojifunza kurudisha nyuma usije kutana na mlingoti wa umeme ukaingia kwenye kioo cha nyuma utakuumiza!
 
WanaJAMII naomba mnipe hongera,

Leo nimemaliza mafunzo ya kuendesha gari salama salimini, nimejifunza vitu vingi sana, ikiwemo:
  1. kuingiza na kubadili gear!
  2. kukanyaga mafuta!
  3. kunyoosha sterling kufuata bara bara!
  4. kukata kona
  5. kuwasha indicators
  6. kuwasha full

Mwl wangu kanambia bado vitu vichache tu, ikiwemo kupiga honi na kurudisha gari nyuma, kasema kupiga honi ni issue ya siku 1 tu, ila kurudisha gari nyuma ndio kidogo kazi, natakiwa kuwa makini kwenye kulenga!

Ahsante Mwl

mi cjaelewa, anaomba kaz au?!
 
Mada nzuri sana kwa waelewa,so kama umehitimu hivyo vingine inatosha kupiga honi na kurudi nyuma hiyo utajifunza taratibu haitaki haraka,ila kuwa makini.
 
......siku ukijifunza kurudi nyuma, sharti la kwanza ufungue mkanda na ukae upande upate kuona vizuri.


#MosKwito !
 
Unajua jinsi ya kuwasha kwa kuunganisha waya?

Kama hujui mwalimu wako feki
 
Dah mwalimu wako ni mwema anataka kukufundisha na reverse mapema tu, ila unaweza kuwa dereva mzuri, subiri tu somo likifika.
 
Back
Top Bottom