"Nimebakiza wiki moja tu ya kuishi, nisaidieni!" Hii ni kauli nzito inayoonesha kukata tamaa, kutoka kwa kijana Said Abdallah (33).
Said anapitia kipindi kigumu, siku zake za kuishi zikiwa zinahesabika kutokana na ugonjwa unaomsumbua.
Saidi anakabiliwa na uvimbe unaokua kwa kasi kubwa, na kwa mujibu wa madaktari, amepewa muda wa takribani wiki moja tu ambapo asipotibiwa, uvimbe huo unaweza kupasuka na kumsababishia kifo.
Kwa sasa anaishi katika maumivu makali, akishindwa hata kulala, kugeuka kitandani, au kufanya shughuli za kawaida.
Kupitia moyo wa huruma wa Watanzania, jitihada za kumsaidia zimeanza kuzaa matunda. Tayari jumla ya shilingi milioni 30 zimepatikana, zikiwemo michango kutoka kwa Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, Mtanzania anayeishi Uingereza aliyetoa shilingi milioni 20 na Watanzania wengine mbalimbali.
Hata hivyo, bado zinahitajika shilingi milioni 10 tu ili kukamilisha gharama za matibabu, ikiwa ni pamoja na safari ya kwenda India kwa ajili ya upasuaji unaotarajiwa kuokoa maisha yake.
Ukiguswa na ugonjwa wa Saidi, tafadhali changia au shiriki ujumbe huu ili kuwafikia watu wengi zaidi.
Michango: 0710 434416
NMB: 20310131829
(Jina: Jundani Mikidadi Abdallah)