Nimeboreka mpaka basi

Nimeboreka mpaka basi

Enny

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
962
Reaction score
130
Kuna rafiki yangu huwa ananiazima gari kwenda kwenye shughuli zake.

Lakini kama mwezi umepita gari ilikuwa haifungi boneti, nikamwambia hawezi kutembeza kwani boneti haifungi. Akaniambia haina tatizo atatengeza tu kwani tatizo dogo. Sasa jana karudi bneti imefunguka akiwa anaendesha ikagonga kioo cha mbele na show yake ya mbele kwenye boneti imetoka na haijulikani ipo wapi. Nilimuuliza kama alitengeneza akasema alikuwa bado hajatengeneza. Hapo nilikasirika sana gari ipo nyang'a nyang'a. Alichoniambia ni kuwa yaani unajali gari kuliko uzima wangu? Na hapo hana hela ya kutengeneza., sijamjibu kitu na mpaka sasa sitaki hata kumwona.
 
Pole sana ndugu,inabidi ufike sehemu ujue gari si kitu cha kumuazima kila mtu,yaan gari ni kitu cha lawama sana na hasa kwa watu kama sisi twenye uelewa mdogo,kubali lawama ya kuambiwa unaroho mbaya kuliko kutaka kumfurahisha mtu,gari ni kama simu ya mkononi au laptop huwezi kumuazimisha mtu,huo ndio ukweli..na ndio maan kuna sehemu maalumu za kukodi gari,wewe tengeneza tu mwenyewe gari yako halafu badilika.
 
Pole sana ukarimu unagharama zake.Kuna jamaa wa ofisini alikuwa akiendekeza kuwaazima gari jamaa wanazunguka wakirudi wanamtupia fungua hata asante wala kuongeza mafuta...kunasiku jamaa akamrudishia gari taa inawaka wakati gari ilikuwa na mafuta nusu tank halafu bila aibu akamuambia ununue mafuta yamisha taa inawaka, hapo ndipo ukomo wa ukarimu ulipoisha na sasa hivi haazimi mtu gari kabisa.
 
Kwa kweli, hapo ni kuwa mpole tu...Nimegundua in life nothing is straight ni lazima kila mtu at some point unafanyiwa kitu ambacho ni cha ajabu sana!
Inawezekana aliyekuazima aliitazama sana shida yake kuliko hatari ya kuendesha gari wakati hujui kama bonet itafunguka saa ngapi.
Msamehe tu utengeneze gari yako na maisha yaendelee, pia jaribu kumjulia hali kuepuka ajali kubwa hivyo si jambo la kitoto japo ni ya kujitakia-that will show a great heart...
NI kweli uchungu umeupata lakini yeye ni binadamu gari inaweza kuibiwa hata leo ila yeye anaweza kuja kukufaa zaidi ya magari kumi. Please forgive and pay the person a visit- wewe ni rafiki.

FYI: the feeling is anger not boredom. You can't be 'bored' when you are all worked up

mmmmh, hiyo gari ulipewa au ulinunua??

Kuazimana magari??? Never!

Pole lakini!

kuazimana magari ni kitu cha kawaida kama wote mnamiliki gari/magari, lkn kama mmoja hana alafu anaazima hapo ndiyo huwa noma.
 
Kama ulikuwa unashindwa kusema hapana sasa amekusaidia kukupa sababu ya msingi ya kusema hapana. Wewe itengeneza halafu akija kuomba umuazime tena mwambie asiwe anajali sana gari akumbuke ubinadamu pia ni muhimu kwenye urafiki wenu.
 
Kuna rafiki yangu huwa ananiazima gari kwenda kwenye shughuli zake.

Lakini kama mwezi umepita gari ilikuwa haifungi boneti, nikamwambia hawezi kutembeza kwani boneti haifungi. Akaniambia haina tatizo atatengeza tu kwani tatizo dogo. Sasa jana karudi bneti imefunguka akiwa anaendesha ikagonga kioo cha mbele na show yake ya mbele kwenye boneti imetoka na haijulikani ipo wapi. Nilimuuliza kama alitengeneza akasema alikuwa bado hajatengeneza. Hapo nilikasirika sana gari ipo nyang'a nyang'a. Alichoniambia ni kuwa yaani unajali gari kuliko uzima wangu? Na hapo hana hela ya kutengeneza., sijamjibu kitu na mpaka sasa sitaki hata kumwona.
Sasa haujamjibu kitu ndio itatengeneza gari lako? kwani si umwambie atengeneze na uchukue kitu chake chenye thamani kama dhamana mpaka atengeze?

sipendi au sijazoea kuazima.

Niko comfortable na kitu changu.

kuazimana magari ni kitu cha kawaida kama wote mnamiliki gari/magari, lkn kama mmoja hana alafu anaazima hapo ndiyo huwa noma.
 
Ni makosa sana kuwaazima watu vitu
ambavyo hawawezi ku 'afford' wao wenyewe
ni makosa....

muazime mtu gari kama na yeye analo lake
mtu hata baiskeli hana
we unamuazima gari
anaendesha kwa fujo,analiharibu

Naomba uniazime kamera yako
 
Hata kama una gari, unaazima la mtu la nini? Afu kuna watu mjini wanaazimana hadi viatu na nguo! Tabia mbaya kweli! Afu ukute gari yako unapelekaga kwa wachina, akaitengeneze gongo la mboto ikirudi iko kama mgongo wa kobe!

Uswahili mzigo, kha!
 
Back
Top Bottom