Nimechaguliwa kozi ya Wildlife Management. Naomba ushauri

Kozi dogo ajira zake chache sana kuna jamaa nilisoma nao paleSUA mpaka leo wanasota pia ni kozi inahuwanja mdogo wa kujiajiri hukikosa ajira
Shkran mkuu
 
Hivi Tuition fee ni sh ngapi?, ni course nzuri unaweza pata ajira kwenye Mbuga za wanyama nk.
 
hapo hakuna course, nina ndugu yangu alisoma certificate ya iyo mambo, hakupata ajira, akaenda kusoma diploma yake napo hakupata ajira, akaongeza degree yake alimaliza 2017 napo hakupata ajira, akaingia kusoma masters yake mwakani anamaliza masters aingie tena kwenye kusaka ajira (((yeye amepata fulsa ya kusoma kwa kuwa kwao ni watu wanajiweza sana))))
 
Daaaaah aseeeh
Ila haya mambo ya Ajira mda mwingine huwa Ni Bahati2
Mkuu Sina jinsi maana nimesha confirm ngoja nikapambane kiume kitaeleweka mbeleni[emoji23]
 
We kasome kwanza mambo ya ajira utayajua ukishatoka. Siku hizi wanakosa ajira waliosomea Education na nursing sembuse wildlife...ukimaliza naamini milango itakuwa imeshafunguka ila kuna wahitimu kibao tangu Magu aingie madarakani kutoka vyuo vya Udsm, Sua na Mweka bado wanasugua benchi ila hiyo isikutishe.
 
Nenda kasome asisee uje usaidie kutunza wanyappri wetu.Ajira ipo
 
Kweli mkuu itajulikana mbele kwa mbele
 
kwenye huu uzi wako ulichokuwa unataka ni kutiwa moyo na hamasa pindi utakapoanza masomo sio ushauri. Pia

kipindi unasoma focus kwenye kusoma na kupata alama nzuri hiyo inatosha kuwa Bora na kujijengea uwanja mpana wa soko ajira.


Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Asante Sana nitafata USHAURI wako be blessed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…