Nimechanganyikiwa! Nimemsaliti GF wangu, kwa kumpa mimba mwingine..

Nimechanganyikiwa! Nimemsaliti GF wangu, kwa kumpa mimba mwingine..

Pole sana mkubwa, kweli wewe ni kidume cha mbegu unatoa mimba kama njugu duh! Mpe na huyo demu wako!

lea mtoto huwezi jua Mungu kakupangia nn yawezekana unamwona mzuri akawa sio mke wa ndoa kama unavodhani. usitende dhambi mara 2 mchukue ulompa mimba mlee na usijaribu utoa mimba,wengi waliokataa mimba zao wanajuta kutopata watoto nina mifano ya wengi, tubu dhambi zako,murudie mungu.mtoto akizaliwa utajua kama mwana ni wako mlee na kwa sasa toa matunzo ya mimba

Jamani wana jf naombeni msaada wenu nipo njia panda nasijui cha kufanya.Full stor ni kwamba kama mnavyo elewa wanaume wengi kuwa na mpenzi mmoja (girl friend) wengi tumeshindwa kilicho nikuta nimempa mimba dem ambaye sina mpango wa kumuowa kutokana na tabia zake na uwezo wake kufikiria bado ni mdogo na sijui dem wangu wa kweli akijua itakuje na kiukweli nampenda sana mpenda sana dem wangu wa ukweli kuanzia sura hadi tabia jamani nifanye nini ?
Kabla ya kukusahuri, nikuambie wazi kuwa ukweli ni kuwa sio huyo ulompa mimba anatabia mbaya na uwezo wake wa kufikiri ni mdogo, bali ni wewe ambaye una tabia mbaya na uwezo wako wa kufikiri uko chini kabisa. Ingekuwa kinyume ya hivyo, usingefanya kufanya ulofanya.
Lakini kwa kuwa maji yakimwagika hayazoleki, na katika hili unapaswa ubebe mslaba wako, ninakushauri ufanye yafuatayo:
1. Kuwa mkweli. Mwambie mchumba wako yote yaliyotokea ili yeye aamue kubakia na wewe au la. Akikataa ni haki yake kwani ukweli ni kuwa humsthiki.
2. Ikiwa atakubali kuendelea na wewe, uwajibike na majukumu yanayokukabili kwa hicho kiumbe kitarajiwa.
3. Ikiwa atakataa na ndivyo inayotakiwa afanye (lakini uamuzi wa mwisho ni wake), rudi kwa huyo mwenye tabia mbaya wako, mchanganye akili zenu kumlea huyo mtoto ambaye hana kosa kuletwa duniani na mtu kama wewe.
Mwisho, Pole sana!

aaaaah jamani...imekuwa hayo tena....haya bana! Ngoja nitamtafuta AshaDii...nina uhakika huko nitapata mwaliko!

Weka vizuizi pale kwenye lile bonde la ufa asipite kwisha kazi yake, huwa nasikia anabeba ubwabwa kwenye shati

Ooookay..basi kwa neno lako nitajiandaa.....

Hahaha,me nilitumiwa PM kwamba Rejao kakatwa kidevu so nichangie
hela ya matibabu,ila ilikua kweli aisee

Tuschakachue sredi sana, jibaba nishapuliza ya ubelgiji natia timu mbugani sasa. Keren na Ze finest am on my way.

Bek to topik: refer to my previous posts, senkyu wazalendo

ndio ukome,kwa taarifa yako huyo wa ukweli hatavumilia upuuzi huo,umelikoroga na lazima ulinywe

Kwenye red lipo IFAKARA -KILOMBERO karibu na Mochwari ya hospitali YA Mt.Francis

Mkuu, Hawije!!!!!
Hata kama hujui kuitikia waulize 'wana-wa-pakaya' watakuelewesha. Ninaomba utununulie 'NGALANGE' (samaki watamu waliokaangwa) wa kutosha na mchele kama sehemu ya maandalizi ya wanajf ili jamaa akishajinyonga tutandike mswala tufafanye mambo; ubwabwa kwa 'ngalange' na soda.

Pole sana. Tamaa mbele mauti nyuma.

Tukiongea ule ukweli kabisa, hakika hujampenda hata mmoja wa mabinti hawa zaidi uliwatamani sana. Kama unampenda mtu kweli, utamfanyia ujinga kama huu??? Tusichanganye tamaa na Upendo hata siku moja. Hayo ndo matunda ya tamaa.

Suluhisho si kujinyonga. Ukijinyonga sanasana utakuwa umeongeza tatizo badala ya kupunguza.

Ninachoweza kukushauri ni kwamba jaribu kutumia utu wako wa kibinadamu kuyashinda matatizo kwani matatizo ni ya binadamu kuyashinda na kuyatafutia suluhisho. Wajibika kijna mwenzangu na usikimbie majikumu. Ongea ukweli ili uwe huru. Mweke wazi unayedhani kuwa wampenda. Ajue kila kinachoendele ili naye atoe maamuzi yake. Huenda hata akakusaidia kwa ushauri.

Nasema Acha kuyakimbia matatizo kama vile wewe si binadamu.

Nami nimshauri kuwa mkweli itaepusha vingi cna,uwe 2 teyar either kuachwa au kusamehewa,mtoto mlee bdae umchukue no other way

lea mtoto huwezi jua Mungu kakupangia nn yawezekana unamwona mzuri akawa sio mke wa ndoa kama unavodhani. usitende dhambi mara 2 mchukue ulompa mimba mlee na usijaribu utoa mimba,wengi waliokataa mimba zao wanajuta kutopata watoto nina mifano ya wengi, tubu dhambi zako,murudie mungu.mtoto akizaliwa utajua kama mwana ni wako mlee na kwa sasa toa matunzo ya mimba

hkn k2 km hcho!aoe anaempenda

Oa umpendae.just tel ha,akae akijua kabla hujachelewa!

Back
Top Bottom