Nimechoka kabisa kuona haya yakifanyika na wenzetu kwani Tanzania tumemkosea nini Mungu!!?

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
2017-02-05t213619z_129332179_mt1aci14747891_rtrmadp_3_soccer-nationscmr-egy.jpg

Jamani Tanzania na Watanzania milioni 52 sasa tuna dhambi kubwa kiasi gani, toka tuliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1980 nchini Nigeria mpaka leo mwaka 2017 hata dalili za kunusa kushiriki sizioni.

Shida kubwa hasa ni nini?
 
TFF lini Tanzania tutashiriki AFCON??
 
JK alitoa mchango mkubwa sana ambapo sasa hivi tungekuwa tuko world cup, lakini loo, lakuvunda halina ubani
 
Tatizo si TFF,bali tatizo ninaloliona na mindset zetu.Katika kila kitu hatufanyi vizuri ila kwa vile vitu vingine havina kipimo kujilinganisha na mataifa mengine,tunadhani tuko vizuri.
Kuanzia elimu,biashara,michezo,na hata siasa.
Tuna tabia ya uongo unaofikia hata kujidanganya sie wenyewe.Tunajidanganya tuko vizuri kielimu lakini angalia wasomi wetu!Wamejaa kiburi na majivuno lakini kichwani hawana lolote zaidi ya vyeti tu.Mf Rais aliwahi kushangaa idadi ya PhD pale BOT na huku akizidi kuona hawamsaidii kwenye upande wa masula ya fedha ipasavyo.
Ona aina ya biashara tunazofanya.Nyingi ni biashara za kichuuzi tu.Mtu ana mabilioni anakwenda China kufuata bidhaa ambazo hata sisi tuna uwezo wa kuzizalisha hapa!Tatizo ni nini?-Hakuna nia ya kweli ya serikali kuhimiza wazawa kufungua viwanda kwa kuwawekea mazingira mazuri.Utaona mtu akianza tu,TRA hawa na wanakuja kama vile unataka kuanzisha kiwanda cha kusindika bange!Bila huruma utaambiwa kodi ambayo hata serikali haijawahi kuipata.
Katika michezo tunadhani tunajua lakini kuna mambo mengi tunahitaji kijifunza.Hatupendi kujifunza kwa vile tunajua!
Tatizo liko kwenye akili na sio laana kama ambavyo unaweza kufikiri.
 
Kuna vyama vina laana, mkiviondoa mtapeta sana
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kuna vyama vina laana, mkiviondoa mtapeta sana
Hata hicho unachotaka kukiweka madarakani CHADEMA kinalaana zaidi ,kinameza matapishi na kujinadi nayo sikuhizi [HASHTAG]#LOWASSA[/HASHTAG],[HASHTAG]#NYARAMBAA[/HASHTAG]
 
View attachment 633302
Jamani Tanzania na Watanzania milioni 52 sasa tuna dhambi kubwa kiasi gani, toka tuliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1980 nchini Nigeria mpaka leo mwaka 2017 hata dalili za kunusa kushiriki sizioni.

Shida kubwa hasa ni nini?
Siku akili zikiwakaa sawa mbona haya yote yanawezekana kabisa.

Yaani siku akili zikiwarejea ambapo mtaacha kutumia nguvu nyingi kwenye kudhoofisha upinzani na kutambua kwamba kuliko kuwahonga wapinzani kumbe mnaweza kuwekeza fedha hizo kwenye kuendeleza sekta muhimu ya michezo na baadae tukaingia rasmi kwenye ulimwengu wa ushindani wa kimichezo na kujizolea sifa kubwa kama hao unawaona kwenye hiyo picha

Lakini kwa sasa hivi hilo unalolitaka haliwezekani kabisa kwa sababu bado mnaamini wapinzani wa kisiasa ndio mchawi wa kila kitu katika taifa na wao ndio kipaumbele namba moja.

Waziri wa michezo yuko bize kukimbizana na magazeti yanayoandika habari zisizo mpendeza boss wake, wakati huo hajui hata idadi ya timu zinazoshiriki ligi kuu halafu eti ndio anaeratibu mipango yote ya kimichezo.

Hebu acheni tuendelee kuwa watazamaji mpaka siku fahamu zikiwarejea na kuwa serious kwenye vitu vya msingi.
 
Hakuna mahusiano yoyote na mada husika
 
Believe me, yakianzishwa mashindano ya kuongea tutashika mkia.

Hata yakianzishwa mashindano ya upuuzi, tutaanguka vibaya sana
That is very true mkuu
 
Mkuu,,watanzania tunaongea mno bila vitendo hili ndio tatizo letu,,, na vile vile tumeendekeza ushirikina sana na ndio maana soka letu haliendelei,, lau tungemtanguliza Mungu mbele kwa chochote kile yani tungefika mbali sana.
 
tatizo la watanzania ni hatujitumi kila sekta ni mbovu...

timu za taifa huwa zinaundwa na wachezaji wanaocheza timu za club zao..

taifa starz 95 parcent ni wachezaji wanaotoka club mbovu...

hakuna beki timu ya taifa ambaye anacheza club ya kueleweka kuweza kumzuia hata mshambuliaji wa mazembe au al hally asifunge goli..

hakuna kiungo mkabaji wa kuzunguka dakika 90 anakimbizana na viungo wa esperance au es setif au enyimba...

sasa hao tu waafrica wenzetu hata kama hawachezi ulaya ila wanacheza club za kueleweka ambazo zinawaandaa kukabana na mchezaji anaecheza ligi yeyote..

timu zima ya taifa starz mchezajii ni wawili tu ambao ni samatta na ulimwengu...

huku wenzetu unakuta wachezaji wote 23 wa timu ya taifa wanacheza mpira wa level kubwa katika club zao..

huwezi kwenda mataifa africa kwa kutegemea wachezaji waliozoea kuwafunga maji maji na mtibwa
 
View attachment 633302
Jamani Tanzania na Watanzania milioni 52 sasa tuna dhambi kubwa kiasi gani, toka tuliposhiriki mara ya mwisho mwaka 1980 nchini Nigeria mpaka leo mwaka 2017 hata dalili za kunusa kushiriki sizioni.

Shida kubwa hasa ni nini?
sisi tuna dili vyama vya siasa vivuke boda kwa siasa si mpira kwa nchii ndugu
 
Uwekezaji kwenye soka ni mdogo sana. Juhudi zinahitajika hasa kufanya mapinduzi ya soka.
 
Back
Top Bottom