Nimechoka kubeba zege, nataka kurudi shule

Nimechoka kubeba zege, nataka kurudi shule

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Wasaalam wakuu..heshima....baada ya kudunda kidato cha nne miaka kadhaa iliyopita, nikaona nikaona niingie mtaani kufukuzana na shilingi...lakini miaka yote hiyo pesa nayo imeota miguu na imenizidi kasi...kazi zenyewe ngumu na pia hazina future...nimeuza mitumba mpaka miguu imepata matege sababu ya kutembea...nikifungua kibanda askari wa jiji wanakibomoa..nikaona nibahatishe kwenye zege....nako nimebeba mpaka kichwa kimepata kipara...na mgongo umepinda....lakini nikiwacheki wenzangu angalau waliopata cheti cha form 4 mambo yao si haba na mimi nimeona bora nirudi school...wadau wa elimu mnanishauri vp..?..nawasilisha...
 
nenda mkuu na hivi kuna mpaka division 5 si haba.mambo yamebadilika sana.hongera big result now with low input
 
kukimbia shule siyo kukimbia matatizo mkuu,.

Umefanya maamuzi sahihi kama kweli umedhamiria kufanya hivyo!!
 
Back
Top Bottom