Kama ndg. wa mkeo bado ni tegemezi (Wanafunzi) wavumilie tu, familia zetu hizi akibahatika mmoja wa familia akawa na mwanga kidogo mzigo wote unamwangukia.
Ila kama ni watu wazima na si wanafunzi na una miradi ambayo unaweza kuwaweka wakusaidie fanya hivyo. Wasibweteke tu nyumbani, wazalishe.
Kama hakuna miradi midogo midogo ya wao kukusaidia, kaa na mkeo mpe nyeusi na nyeupe, warudi kwao.
Wewe ndo unayeujua uhalisia wa maisha ya kwao. Pia kama unaweza kuwasaidia kwa kuwatafutia sehemu ya kujishikiza unaweza kufanya hivyo.